Hamas Waridhia Mpango wa Trump wa Kukomesha Vita Gaza

Hamas Waridhia Mpango wa Trump wa Kukomesha Vita Gaza

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Hamas wametoa jibu kwa mpango wa Trump wa kukomesha vita Gaza. Hamas wamesema kuwa kimsingi wanakubaliana na mpango huo, wanachohitaji ni kujadili undani wa utekelezaji.

Mpango wa Trump wa kumaliza vita Gaza, unawataka Hamas kuwaachilia mateka wote ndani ya masaa 72 tangu wakubali, Israel kusimamisha vita mara moja, japo wanajeshi wataendelea kusalia ndani ya Gaza mpaka kikosi cha kimataifa kitakapokuwa tayari. Mpango huo unawataka Hamas kusalimisha silaha zao, kisha watapewa msamaha, na wanaotaka kuondoka watapewa njia salama ya kuondokea, Hamas kutohusika kwa namna yoyote ile katika uongozi wa Gaza, na Gaza itakuwa chini ya utawala wa wasomi wa kipalestina wakiongozwa na Tony Blair na baadhi ya watu watakaoteuliwa toka mataifa ya kiarabu. Kisha Trump atasimamia mpango wa mahusiano ya kirafiki kati ya Israel na nchi zote za Mashariki ya kati, ukiacha Iran iliyotengwa na Dunia.

ALJAZEERA​

Updates: Israel bombs Gaza homes; Hamas responds to Trump proposal​

Hamas has accepted core elements of US President Donald Trump’s plan for Gaza, including the return of all Israeli captives.

LIVE: Trump says Hamas ‘ready for peace’, tells Israel to stop bombing Gaza​

 
Trump na hao Hamas siwezi waamini kwa lolote wanalosema wameafikiana...wote wajanja wajanja tu.
 
Back
Top Bottom