Gaza kumekucha huko wananchi wanazurura mitaani wakiimba na kumshukuru Mungu baada ya Hamas kukubali masharti ya Israel muda huu.
Kwakweli Mungu ni mwema anajibu wamekufa wengi sana na sasa tuseme imetosha waliobakia waendelee na maisha ila adabu wamekipata walichokitafuta.
======
Kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh ametuma neno la kundi hilo kukubali pendekezo la wapatanishi, Qatar na Misri kusitisha mapigano.
- Maelfu ya watu wamekimbia mashariki mwa Rafah baada ya Israel kuwataka kuondoka ikijiandaa na mpango wa mashambulizi kwenye mji huo
- Hamas imesema mashambulizi ya Majeshi ya Israel haitakuwa 'Picnic' na imejiandaa kuwalinda raia wa Palestina.
Chanzo ndani ya Jeshi la Israel kimenukuliwa na Reuters kikisema Hamas wamekubali pendekezo laini la Misri ambalo halikubaliki kwa Israel. Vyombo vya habari vya Israel pia vimesema Serikali ya Israel havijakubali mpango huo.