Hamas yasema hawana hao mateka 40 wanaotakiwa. Kosa la nani

Kama mumewaua sasa mjiandae kipigo maana mtakua hamna kete nyingine, mlikua mnatumia mateka kama namna kupata kusikilizwa.
 
Sasa shauri yao Hamas kama hao mateka wameyeyuka, watavuna jeuri yao. Mazayuni hawana huruma wala hasara tena, ni mwendo wa kipigo tu.
ni swala la mda tu raia wa israel watamuua nyetanyahu kwa mikono yaokwa kuwaualia ndugu zao waliotekwa kule GAZA,pona yake ni ku resign na kuwekwa kolokoloni...hataki basi kabla krismas benjamin atakuwa mwendazake
 
Ndugu hata Israel pia Kuna watu wanamlaumu waziri mkuu kwa kushindwa kuwapata hao mateka hadi leo.
Wengine wanadai malengo ya vita yameshindwa,vita ikome.
The same ukienda Urusi pia Kuna watu wanapinga vita na Ukraine.
Cha ajabu zaidi wapo watu Ukraine wanailaumu nchi yao kwa hatua zake za kutaka kujiunga na NATO ndio zimeleta zahama.
Uki-dili na jamii yoyote huwa hakuna uungwaji mkono wa asilimia mia!
 
 
Walishaachiwa,mateka wasiofika 100 ndio uuwe watu wengi hivyo
Strategy ya Hamas kujificha kwenye mahandaki chini ya Nyumba za raia nako unakuongeleaje?
 
Kama kwamba Israel imewaua yenyewe halafu inawadai.Ni hadithi ya mwanakondoo na fisi.
Aliye wambia wawateke nani huku wanajua wanacheza na moto!
Kanga walio chums wanakula na watoto wao
 
Ukweli na haki daima havifichiki hata ikichukua muda.
Nakwambia ingekuwa watu wa Gaza kweli wengi wanaipinga Hamas basi wala wasingeweza kutawala na tangu vita vianze wangekwishaparurana.
Na aljazeera sidhani kuwa ina uwezo wa kuzuia hasira za watu kwa kumkwepa mzee huyo asiseme alichonacho.
kama unafuatilia vizuri watu wa Gaza hata kama wana kitu dhidi ya Hamas basi ni kidogo sana kuliko wanavyoichukia Israel.
Idadi kubwa wanaohojiwa na wanashuhudia vifo vya ndugu zao na uharibifu wa mali basi huwa wanamshukuru Mungu na halafu wanailaani Israel na si Hamas.
Mwezi uliopita Israel ilifanya jaribio la kuwakosanisha Hamas na watu wao kwa kuanzisha vikundi vya kupokea maagizo kutoka Israel.Hilo zoezi lilifeli mia kwa mia.
 
Nyinyi mnaoabudu Mungu aliyedundwa usiku kucha na yakobo mna akili sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…