Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Leo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram Mwanasiasa Hamis Kigwangalla ametoa maoni yake kuhusu uchaguzi wa mwaka huu na maandamano yaliyopangwa kufanyika nchi nzima tarehe 29 Octoba, 2015. Ameandika Na kuchapisha post kama 7 hivi zikiwa na ujumbe ufuatao
OKTOBA TUNATIKI VS OKTOBA TUNATOKA
Na Dr. Hamisi Kigwangalla,
J o b l e s s Wa Taifa.
Kwenye post zangu za hivi karibuni watu wamekuwa wakiniita “jobless wa Taifa”! Dah! Mimi huyu nimekuwa jobless wa Taifa kweli? Nimelia sana! 😂🤛🏾
Jokes aside, nina kitu serious cha kusema. Kwanza mpaka kufikia leo hapa mngepaswa mjue tu kuwa huwa sikasiriki hata mtukane vipi! Hata mponde na kubeza vipi. Sikasiriki. Mngeacha tukaishi tu, sababu I have thick skin. Unajua kwa nini? Leo ntakuambia. Twende pamoja.
Mosi, nilianza uongozi nikiwa mtoto mdogo kabisa, Chipukizi! Class Monitor! Head Prefect! President - mpaka baadaye kuingia kwenye siasa za kitaifa.
Kwa hiyo niliishapingwa na kushambuliwa sana. Niliishasemwa na kusingiziwa vitu sana. Mapito yangu ni MBA na MPA classes combined! Ukichanganya na Ph.D ya kitaa - hii package huiwezi kabisa!
Mfano, leo ntaongea reality ya Oktoba Tunatiki Vs Oktoba Tunatoka. Najua mtatukana na kupinga na kubeza mpaka baasi, lakini hii ndiyo reality. Tena mkinikera zaidi naenda kwenye live television! Mkinikera zaidi naitisha press conference. Nawaeleza ukweli mchungu kabisa. Ukitaka uuchukue, hutaki uuache!
Pili, mimi ni katika wale waumini wa kweli kabisa wa uhuru wa kuongea. Ukiona nimenyamaza unatakiwa ushangae maana usually I am too vocal. I was born and raised that much. Wengi mnaoninanga na kunisimanga hamko tayari kunipa haki yangu ya kuwa huru kusema na ama kufanya ninavyojisikia lakini nyie mnadai haki hizo kwa serikali kila siku.
Najua mnakosa pa kwenda ku-vent hasira na machungu yenu ya kuwa jobless ama ya kupoteza matumaini na mnaona sisi wachache tuliopata fursa ya kuwa kwenye system ya uongozi wa nchi tumewasaliti, na kwa kuwa viongozi wengi hawapendi kuji-expose mitandaoni basi mnamalizia hasira zenu kwangu! Hii ni story for another day.
AKAONGEZA KWENYE POST INAYOFUATA
Mimi naunga mkono Oktoba Tunatiki ✔️. Why? Sababu kubwa ya kwanza; naipenda Tanzania, nchi ya wazazi wangu na nchi ya wanangu. Hatuna nchi nyingine, tuna hii tu! Hata iweje, Tanzania ndiyo kwetu.
Pili, nchi yetu inaendeshwa kwa Katiba, Sheria, Kanuni na mila na desturi zetu. Huu ndiyo utaratibu halali kabisa tuliojiwekea. Huu ni wakati wa uchaguzi na kwa utaratibu tuliojiwekea tutachagua serikali na kuiweka madarakani.
Ukiwa unadai haki yoyote ile lazima uwe ndani ya huu utaratibu uliopo, tuliojiwekea kama Taifa.
Kuna mengi unaweza kuwa hukubaliani nayo, lakini kama yanahusu mama Tanzania, una haki ya kudai sema lazima iwe ndani ya huu utaratibu tuliojiwekea.
Unaweza kuwa humpendi mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan lakini huna option nyingine, utamheshimu kama Rais aliyepo, na kama hutaki uongozi wake, una haki ya kumkataa, lakini ndani ya utaratibu tuliojiwekea. Wewe ukiwa unamkataa, jiandae kushindana na sisi tunaomkubali. Wakati unapanga namna ya kumuangusha, jiandae kushindana na sisi tunaomlinda.
Kama ambavyo wewe unatamani kufanya unavyojisikia na unaona ni haki yako, tuachie na sisi haki ya kufanya tunavyojisikia, maana ni haki yetu.
Lakini jua pia kuwa, unaweza kuwa huamini katika uchaguzi na hutaki kushiriki. Una haki ya kuamini unavyoamini na una haki ya kuchagua kutokushiriki, lakini ndani ya utaratibu tuliojiwekea. …
AKAONGEZA KWENYE POST INAYOFUATA
Ukivunja sheria utachukuliwa hatua. Ukifanya fujo utatulizwa. Mfano: ukisema unataka kutumia haki yako ya kuandamana kwa kuwa wewe hutaki kushiriki uchaguzi, hakikisha unatumia haki hiyo bila kuwaathiri wale ambao wanashiriki uchaguzi. Maana uhuru wako wa kuandamana unaishia pale ambapo uhuru wa wengine wa kwenda kazini, kwenda msikitini, kwenda kupiga kura unapoanzia.
Haki yako ya kukusanyika ina utaratibu wa kufuatwa, ina mipaka yake, haiwi automatic tu!
Hebu fikiria mfano siku ya uchaguzi unataka kwenda kuandamana, halafu CCM, ACT, CHAUMMA, CUF, ADP etc nao wakasema wanaandamana mpaka kwenye vituo vya kupigia kura, na kwamba wakikutana na wewe unayetaka kupinga uchaguzi wakushughulikie! Ama wakasema wataweka ulinzi wao binafsi, kwamba yeyote atakayekuwa kwenye ile slogan ya ‘oktoba tunatoka’ watamshughulikia, itakuaje? Tutakuwa na nchi?
Kuna siku nilimsikiliza mtu mmoja akielezea idadi ya askari waliopo akikadiria kwa intake zao etc. nikasema huyu ana taarifa nusu nusu sana kuhusu vurugu na kifo na dola!
Hivi unadhani kuna serikali itakubali jeshi lichezewe? Labda siyo Tanzania. Sisi kwanza intelijensia yetu iko juu sana kuliko unavyofikiria. Kabla hujafika lami hapo ulipo tayari utakuwa ushavunjwa mguu ili kupunguza jam, ikatokea mguu haujavunjika, utakuwa una sprain chungu sana unakandwa ghetto na wife! Utavurugwa na kuachiwa kiasi kwamba atakayekuona hatokutambua, na atakula chochoro kurudi kujifungia ghetto!
Idadi ya askari has nothing to do na manundu utakayopata kabla haujafika barabara yoyote ile ya lami! Combat strategy haihitaji uwingi wa askari zaidi ni battle tactics na timing! Hatuna jeshi hata moja la hovyo hovyo. Hii ni Tanzania na ina Askari mahiri. ….
AKAONGEZA KWENYE POST INAYOFUATA
Usije ukasahau hii nchi ina asili ya kijamaa. Ujamaa unaweza kutoweka kote huko lakini siyo kwenye Majeshi yetu. Haya yanalinda misingi. Moja kati ya misingi imara ya Taifa letu ni Uhuru! Uhuru unaanzia kwenye kuilinda demokrasia ya uchaguzi.
Unajua unaweza kuwa hukubaliani na maamuzi, na wakati mwingine yamekuumiza sana, lakini la muhimu ni kuheshimu maamuzi. Kama ambavyo wewe unataka maamuzi yako yaheshimiwe, vivyo hivyo na wengine nao wanataka iwe.
Kwa hakika amani ni tunda la haki. Ila hakunaga haki isiyo na mipaka. Uko huru mpaka pale utaratibu unapoanzia. Una haki mpaka pale mipaka yake inapoanzia.
Watanzania wanayajua haya vizuri sana; wanaheshimu Katiba, Sheria, Kanuni, na mila na desturi tulizojiwekea kama Taifa, na ndiyo maana tuko hapa “Tunasonga mbele!” Najua hawatotoka hii Oktoba! Why?
1. Watanzania hawaaminiani. Kila mtanzania ni shushushu!
2. Hakuna wa kuwahamasisha na kuwatoa hofu, sababu kila mmoja anamuogopa mwenzake.
3. Watanzania hawajapata sababu ya msingi kabisa ya kuandamana. Zinazotolewa wanaona ni kama sababu binafsi za watu wachache wenye maslahi yao binafsi ama ya kisiasa.
4. Watanzania wamejifunza kwamba hata hao wanasiasa wa upinzani wengi ni ‘yarabb nafsi’, wenye kupigania matumbo yao binafsi, siyo watetezi wa kweli wa haki za wanyonge. Maana wapinzani wengi nao walikuja kuhamia CCM na walipewa vyeo wakanyamaza. Na waliobaki upinzani walikuwa wanagombania ruzuku tu! Mfano kaka yangu aliyenusurika kuuwawa alipopata ahueni alionekana akipambania kulipwa hela zake tu!
AKAONGEZA KWENYE POST INAYOFUATA
Watanzania wameishapoteza interest na siasa na wanasiasa. Wanatuona sisi wanasiasa wote miyeyusho tu! Tuna kazi kubwa ya kufanya kurudisha imani ya wananchi kwenye mfumo wetu wa siasa na uongozi. Utaona voter turn out ya mwaka huu itakuwa ndogo sana! Watu hawatoenda kupiga kura.
6. Wanaohamasisha maandamano hawako Tanzania, hawana reality ya maisha ya watanzania na hawana ujuzi wala uzoefu wa kufanya harakati za uasi. Sisi tulipokuwa tunaongoza migomo tulikuwa na ushawishi mkali sana lakini tulifeli mara nyingi zote.
7. Serikali mpaka sasa naamini itakuwa ishajua itaanza kuwadaka nani na nani - divide & rule, na itakuwa ishajipanga kuwatandika bakora nani na nani, wa maeneo gani! Wakati wakichapwa, mtandao utazimwa, umeme utazimwa, barabara zitafungwa. Kila atakayekamatwa hatokuwa na uwezo wa kuwasiliana na mwenzake na hatopata mwongozo wowote ule! Ni showdown ya saa moja tu na shughuli ishaisha!
8. Watanzania hawako tayari kwa mambo serious. Tunapenda sana mambo ya mzaha mzaha, mepesi mepesi (kama kuja kumtukana hapa HK! Ama kuangalia wale vijana wa kiume wanaochamba kuliko wanawake!)
9. Watanzania wengi ni wanafiki! Siyo wakweli. Movement haitaki unafiki, inataka msimamo na mshikamano thabiti.
10. Watanzania hawana njaa. Hakunaga mshikamano wa watu walioshiba. Maisha ya Tanzania ni rahisi sana. Leo mazoezini beach nimekutana na kijana graduate anavuta kokoro, hana kazi sababu mkataba wake uliisha pale NHC, amejiunga na wenzake wanavua samaki wanauza mnadani wanapata maisha! Kuna nchi hata hicho kibarua cha kuvuta kokoro hakuna! ….INAENDELEA….
11. Ni ngumu kuwagawa watanzania kwa dini zetu (tumeoleana across religions, hivyo tuna ndugu wakristo pamoja na baraghashia zetu!), kwa makabila yetu (tumeoleana across makabila-Lema yuko kule na NRNE yake, dada yake yuko Oktoba tunatiki nishamsilimsha zamani! N.k.!)
AKAONGEZA KWENYE POST INAYOFUATA
Kuna mambo mengi mimi binafsi sikubaliani nayo lakini kuyadai kwa njia ya maandamano na vitisho si sahihi. Mfano: Kwa nini hakuna Mgombea binafsi Tanzania? Kwa nini tusipunguze madaraka ya Rais kidogo-kila teuzi basi wateule wawe watatu waidhinishwe na bunge? Kwa nini ofisi ya CAG isiwe chini ya Bunge moja kwa moja? Kwa nini ofisi za MAADILI, TAKUKURU, zisiwe chini ya Bunge?
Tuulizeni sisi tuliowahi kuwa katikati ya migomo tutawaambia watanzania ni watu wa aina gani! Sekunde vijana wa FFU wakitokea utajikuta umebaki Kiongozi na wapambe wawili watatu hapo! Unaowapigania waliishakimbia zao kunusurisha miili yao!
Kuna siku palipigwa mabomu Arusha, ndiyo nilijua kwamba shemeji yangu Lema ana kipaji cha riadha basi tu!
Awamu yangu ya kwanza ya Ubunge nilipigana kwa nguvu sana kudai haki za wanaNzega, mpaka mjomba siku moja akasema “Hamisi, you have a lot of energy!…slow down kidogo!”
Hii ni siku niliandamana na chemli kuwaamsha wanaNzega kudai haki kwa wawekezaji wa dhahabu. Nilihutubia maelfu ya waandamanaji, kama zaidi ya 5000! Dakika FFU walivyopiga mabomu nilijikuta nimebaki na Msaidizi wangu mmoja tu Ndg. Peter Dafi, Katibu Mwenezi wa CCM Ndg. Mayunga, mwanahabari mmoja tu wa ITV Shinyanga, na mtu mwingine mmoja! Wengine hawakuonekana jumla! Walau Sungusungu wenzangu walipiga mwano wa kiume sasa na kuja front mpaka kituo cha polisi kunitoa!
Rai yangu jobless ni kuwa mlioko serikalini tafuteni namna ya kuzungumza na hawa watu wa NRNE tufanye uchaguzi twende kwenye mabadiliko ya Katiba tuisuke upya nchi yetu. Katiba hii imekuwa bora sana kwa kipindi chake, na sisi tunaoishi leo tutengeneze Katiba mpya itakayoishi miaka mingine zaidi ya 50! Uzuri CCM tumeweka mabadiliko ya Katiba kwenye ilani yetu. Uchaguzi uishe wazee wa NRNE waje mezani tusuke upya Taifa.
AKAONGEZA KWENYE POST INAYOFUATA
MWISHO: OKTOBA TUNATIKI VS OKTOBA TUNATOKA…Tena kama mkifikiria vizuri zaidi mtatekeleza dira ya mama Samia Suluhu Hassan ya 4Rs na slogan yake ya Kazi na Utu kwa kutafuta kifungu kitakachoisaidia mahakama kuifuta kesi inayomkabili Ndg. Tundu Antipas Mughwai Lissu.
Watanzania wamechimba mkwara, sote tunajua hawawezi kuandamana. Najua wachache watakaojitoa mhanga tutawavunja miguu, lakini sauti yao imesikika. Wamesema na tumewasikia. Tusiwapuuze. Tutoe uongozi, tuunganishe Taifa, tujenge. #HK #Fighter #NjeYaBox #OktobaTunatiki