GE2025 Hamis Kigwangalla ni kama anataka Maandamano lakini hawezi kusema wazi, kaweka maoni yake Instagram

GE2025 Hamis Kigwangalla ni kama anataka Maandamano lakini hawezi kusema wazi, kaweka maoni yake Instagram

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
FB_IMG_1759557878308.jpg
 
Kuna watu wengi km yaye ndani ya chama wamechoka ila mdomoni wana maji wanaogopa upepo wa kina jk usiwapeperushe mbali kwa manukaa ya matumbo yao
 
Aliyoandika Hamis Kigwangallah huko Ista


Usije ukasahau hii nchi ina asili ya kijamaa. Ujamaa unaweza kutoweka kote huko lakini siyo kwenye Majeshi yetu. Haya yanalinda misingi. Moja kati ya misingi imara ya Taifa letu ni Uhuru! Uhuru unaanzia kwenye kuilinda demokrasia ya uchaguzi.

Unajua unaweza kuwa hukubaliani na maamuzi, na wakati mwingine yamekuumiza sana, lakini la muhimu ni kuheshimu maamuzi. Kama ambavyo wewe unataka maamuzi yako yaheshimiwe, vivyo hivyo na wengine nao wanataka iwe.

Kwa hakika amani ni tunda la haki. Ila hakunaga haki isiyo na mipaka. Uko huru mpaka pale utaratibu unapoanzia. Una haki mpaka pale mipaka yake inapoanzia.

Watanzania wanayajua haya vizuri sana; wanaheshimu Katiba, Sheria, Kanuni, na mila na desturi tulizojiwekea kama Taifa, na ndiyo maana tuko hapa “Tunasonga mbele!” Najua hawatotoka hii Oktoba! Why?

1. Watanzania hawaaminiani. Kila mtanzania ni shushushu!
2. ⁠Hakuna wa kuwahamasisha na kuwatoa hofu, sababu kila mmoja anamuogopa mwenzake.
3. ⁠Watanzania hawajapata sababu ya msingi kabisa ya kuandamana. Zinazotolewa wanaona ni kama sababu binafsi za watu wachache wenye maslahi yao binafsi ama ya kisiasa.
4. ⁠Watanzania wamejifunza kwamba hata hao wanasiasa wa upinzani wengi ni ‘yarabb nafsi’, wenye kupigania matumbo yao binafsi, siyo watetezi wa kweli wa haki za wanyonge. Maana wapinzani wengi nao walikuja kuhamia CCM na walipewa vyeo wakanyamaza. Na waliobaki upinzani walikuwa wanagombania ruzuku tu! Mfano kaka yangu aliyenusurika kuuwawa alipopata ahueni alionekana akipambania kulipwa hela zake tu!
5. ⁠Watanzania wameishapoteza interest na siasa na wanasiasa. Wanatuona sisi wanasiasa wote miyeyusho tu! Tuna kazi kubwa ya kufanya kurudisha imani ya wananchi kwenye mfumo wetu wa siasa na uongozi. Utaona voter turn out ya mwaka huu itakuwa ndogo sana! Watu hawatoenda kupiga kura.
6. ⁠Wanaohamasisha maandamano hawako Tanzania, hawana reality ya maisha ya watanzania na hawana ujuzi wala uzoefu wa kufanya harakati za uasi. Sisi tulipokuwa tunaongoza migomo tulikuwa na ushawishi mkali sana lakini tulifeli mara nyingi zote.
7. ⁠Serikali mpaka sasa naamini itakuwa ishajua itaanza kuwadaka nani na nani - divide & rule, na itakuwa ishajipanga kuwatandika bakora nani na nani, wa maeneo gani! Wakati wakichapwa, mtandao utazimwa, umeme utazimwa, barabara zitafungwa. Kila atakayekamatwa hatokuwa na uwezo wa kuwasiliana na mwenzake na hatopata mwongozo wowote ule! Ni showdown ya saa moja tu na shughuli ishaisha!
8. ⁠Watanzania hawako tayari kwa mambo serious. Tunapenda sana mambo ya mzaha mzaha, mepesi mepesi (kama kuja kumtukana hapa HK! Ama kuangalia wale vijana wa kiume wanaochamba kuliko wanawake!)
9. ⁠Watanzania wengi ni wanafiki! Siyo wakweli. Movement haitaki unafiki, inataka msimamo na mshikamano thabiti.
10. ⁠Watanzania hawana njaa. Hakunaga mshikamano wa watu walioshiba. Maisha ya Tanzania ni rahisi sana. Leo mazoezini beach nimekutana na kijana graduate anavuta kokoro, hana kazi sababu mkataba wake uliisha pale NHC, amejiunga na wenzake wanavua samaki wanauza mnadani wanapata maisha! Kuna nchi hata hicho kibarua cha kuvuta kokoro hakuna! ….INAENDELEA….
11. ⁠Ni ngumu kuwagawa watanzania kwa dini zetu (tumeoleana across religions, hivyo tuna ndugu wakristo pamoja na baraghashia zetu!), kwa makabila yetu (tumeoleana across makabila-Lema yuko kule na NRNE yake, dada yake yuko Oktoba tunatiki nishamsilimsha zamani! N.k.!)
📌3📌
 
Back
Top Bottom