mkonowapaka
JF-Expert Member
- Feb 19, 2010
- 1,492
- 768

Mwanadafada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto ameamua kumwanika mwandani wake baada ya kumuweka kwenye mitandao ya kijamii huku akimmwagia sifa kemkem.
Hamisa alisema mwanaume huyo ni mtu ambaye anampenda sana na wana malengo ya kuoana muda wowote kuanzia sasa na jina lake ataliweka hadharani soon! (Dj Majey tunamjua)
"Ni kweli ni mpenzi wangu ambaye tunapendana sana na muda wowote kuanzia sasa tutafunga pingu za maisha kama mipango yetu ikikaa vizuri," alisema Hamisa.
Aliendelea kusema kuwa wana miezi sita mpaka sasa na amekuwa mtu ambaye anajua nini thamani ya mapenzi kwani muda wowote akimuhitaji anakuwa karibu yake

KWA MSIOMFAHAMU;UYO JAMAA NI DJ MAJEY WA E FM NA MAISHA...KULA VITU KAKAA