Hamisa Mobeto ana mchango gani kwenye sekta ya madini? Wizara ya Madini mjitafakari sana kuelekea TMIC2024

Hamisa Mobeto ana mchango gani kwenye sekta ya madini? Wizara ya Madini mjitafakari sana kuelekea TMIC2024

Nimeona Wizara ya Nishati na Madini wameandaa mkutano wa TANZANIA MINING AND INVESTMENT CONFERENCE 2024 (TMIC2024)

Wameuita USIKU WA MADINI utakuwa 20th Nov 2024 Mlimani City Mall, DSM

Hamisa naye atakuwepo, nimeshangaa sana. Hivi kweli Wizara imekosa wachimbaji wakubwa wa kati na wadogo ili waje kutoa hamasa kwenye mkutano huo!

Kuna wanawake wengi tu wanafanya kazi kule migodini ambao walitakiwa kupewa kipaumbele.


Wapo wadada na akina mama wanaowekeza kwenye madini na wanayapambania mnakuja kubeba waigizaji?

Ajabu wametuletea Hamisa acha tuone hayo madini atakayotoa.


Na ikumbukwe huu ni mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini.

Nikiwa kama mdau wa hii sekta hili jambo limenishangaza sana.

View attachment 3155006


Hili taifa linaendeshwa kishikaji sana
Duh mdangaji kaitwa mkutanoni
Hii nchi kweli kiboko

Ova
 
Back
Top Bottom