SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Inahitaji jicho la kiinteligensia kujua baadhi ya mambo yanayoendelea nchi hii.
Watu wameshangaa inakuwaje Aziz Ki akatae zaidi ya milioni 90 kwa mwezi, tofauti labda ya zaidi ya milioni 60 ya pesa anayolipwa sasa. Likatengenezwa picha eti mlimbwende Hamisa Mobeto ndiyo kama kamshawishi abaki kwa sababu tu ya "penzi".
Kwa Deportivo de Utopolo ninayoijua mimi na kwa jicho langu la kiinteligensia, ninachojua mimi hawajataka kuweka wazi malipo sahihi wanayomlipa huyu Mbukinabe ili isije kuwaletea shida katika mahusiano kati ya wachezaji wenyewe katika kikosi au kumpa pressure kubwa mbele ya mashabiki. Pia hawakutaka aibu ya kuondokewa na mchezaji mwingine kwa sababu ya kuzidiwa kete na timu nyingine. Mobeto katumika kama kiini macho tu kuwahadaa Waswahili wasiopenda kuchakata bongo zao.
Kuna watu wamechota bilioni sehemu huko wamemlipa chini ya meza kufidia zile alizoziacha za Waarabu.