Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mwanamitindo na mfanyabiashara Hamisa Mobetto amefunguka kuhusu sababu za kutomhusisha mzazi mwenzake kwenye malezi ya mtoto wao Dylan, akibainisha kuwa alikataa mfumo wa malezi uliotawaliwa na masharti yasiyo ya haki pamoja na unyanyasaji wa hisia.
Akieleza hali halisi ya uhusiano wao, Hamisa alisema kuwa hakusita kumweleza mwanaye ukweli tangu mapema kwamba baba yake ni yule yule, ingawa mzazi huyo ndiye aliyemkataa mtoto huyo tangu awali.
"mwanangu Dylan hana baba tofauti na yule, na yeye mwenyewe nilisha muambia kuwa baba yako ni yule ila alikukataa, inaumiza ila inabidi tu umuweke wazi akae akijua" .
Hamisa amefafanua kuwa chanzo kikuu cha yeye kuamua kumlea mtoto mwenyewe bila msaada wa baba yake ni kukataa aina fulani ya unyanyasaji ambapo mzazi mwenzake alitaka kumtumia mtoto kama silaha. Alieleza kuwa mzazi huyo alitaka uhusiano ambao pindi anapojisikia kuwa naye humtafuta na kumtaka aende kwake, kitendo ambacho Hamisa amekitaja kama "utumwa" ambao hakuwa tayari kuukubali katika maisha yake.
"Mimi nilicho Kataa ni Ile mtu Hakupendi ila anataka siku akijisikia kuwa na wewe anakutafuta unaenda, huo ndo utumwa ambao niliukataa, Yani atumie hiyo silaha ndo aweze kumlea mwanangu, hiyo Mimi nilikataa niliona kama utumwa, acha hao alio zaa nao waendelee na utumwa huo ila mimi hapana siwezi nitamlea mwanangu bila shaka yoyote"
Msimamo wa mfanyabiashara huyo uko wazi kuwa hayuko tayari kuvumilia masharti ya aina hiyo ili tu apate ushirikiano wa malezi. Aliongeza kuwa ingawa wapo wengine waliozaa na mtu huyo na kuendelea na mfumo huo anaouita wa utumwa, yeye amechagua njia tofauti na kusisitiza kuwa ana uwezo na utulivu kamili wa kumlea mwanaye Dylan mwenyewe bila shaka wala utegemezi wowote.