Dispensary za serikali 🤣🤣wakafanye DNA nje ya nchi south Africa au nchi za ulaya maana hapa Tanzania atapigwa yanayo endelea hapo kwa mkem.. tunayajua
Oh! Anamnyonya kweli?Hongera Missa umekataa unyonge ndio maana umefanikiwa, alikua anakunyonya nyota yako
Kwani kipindi anapata mimba si alimkuta diamond na mtu.. yeye alitaka kuzaa na mtu maarufu amefanikiwa ila kulipa gharama sasa hataki kwenye hili diamond platnumz yupo sawa maana ndio mfumo wake wa watoto wake wa sasa anavyowalea akimtaka mtoto mama mtu anawaleta watoto yanayoendelea huko sisi mashabiki hatujui..hamisa akubaliane na hali aache kulisha mtoto matango pori na chuki wakati inajulikana ni slay queen na gold dagger tu.Mwanamitindo na mfanyabiashara Hamisa Mobetto amefunguka kuhusu sababu za kutomhusisha mzazi mwenzake kwenye malezi ya mtoto wao Dylan, akibainisha kuwa alikataa mfumo wa malezi uliotawaliwa na masharti yasiyo ya haki pamoja na unyanyasaji wa hisia.
Akieleza hali halisi ya uhusiano wao, Hamisa alisema kuwa hakusita kumweleza mwanaye ukweli tangu mapema kwamba baba yake ni yule yule, ingawa mzazi huyo ndiye aliyemkataa mtoto huyo tangu awali.
"mwanangu Dylan hana baba tofauti na yule, na yeye mwenyewe nilisha muambia kuwa baba yako ni yule ila alikukataa, inaumiza ila inabidi tu umuweke wazi akae akijua" .
Hamisa amefafanua kuwa chanzo kikuu cha yeye kuamua kumlea mtoto mwenyewe bila msaada wa baba yake ni kukataa aina fulani ya unyanyasaji ambapo mzazi mwenzake alitaka kumtumia mtoto kama silaha. Alieleza kuwa mzazi huyo alitaka uhusiano ambao pindi anapojisikia kuwa naye humtafuta na kumtaka aende kwake, kitendo ambacho Hamisa amekitaja kama "utumwa" ambao hakuwa tayari kuukubali katika maisha yake.
"Mimi nilicho Kataa ni Ile mtu Hakupendi ila anataka siku akijisikia kuwa na wewe anakutafuta unaenda, huo ndo utumwa ambao niliukataa, Yani atumie hiyo silaha ndo aweze kumlea mwanangu, hiyo Mimi nilikataa niliona kama utumwa, acha hao alio zaa nao waendelee na utumwa huo ila mimi hapana siwezi nitamlea mwanangu bila shaka yoyote"
Msimamo wa mfanyabiashara huyo uko wazi kuwa hayuko tayari kuvumilia masharti ya aina hiyo ili tu apate ushirikiano wa malezi. Aliongeza kuwa ingawa wapo wengine waliozaa na mtu huyo na kuendelea na mfumo huo anaouita wa utumwa, yeye amechagua njia tofauti na kusisitiza kuwa ana uwezo na utulivu kamili wa kumlea mwanaye Dylan mwenyewe bila shaka wala utegemezi wowote.
View attachment 3671669
Sijaelewa,
Huyu Hamisa si ameolewa?
Ina maana alikuwa anatumika Kitumwa akiwa kwenye ndoa?
Angekuwa diamond ni fundi viatu angepewa mtoto mwanaume yeyote mwenye pesa...Yeye amlee mtoto kama alivyoamua, asimfitinishe mtoto na baba yake. Kusema alimkataa na wakati hapo hapo anasema alikataa masharti, ni fitna hiyo.
Nampa pongezi kumwambia mtoto bba yake halisi, angeweza mwambia vinginevyo tatizo likawa kubwa zaidi kwa mtoto.
Angekuwa diamond ni fundi viatu angepewa mtoto mwanaume yeyote mwenye pesa...
Kwa mantiki hii binafsi naona bado haja move on..Anaelezea habari za kabla ya kuolewa...
Sidhani kama ni kweli. Pengine alitaka kumuonea huyu kwa sababu mnyonge ila Zari sidhani kama anaweza kukubaliana na upuuzi kama huoHapa unataka kusema Tanasha na Ze Boss LEDI huwa wakihitajika wanaitwa kwenda KUTEMBEZEWA RUNGU?
Kwa mantiki hii binafsi naona bado haja move on..
Still insane.
Kabisa, Hamisa anajuwa hata kama diamond hatunzi ila kukubali ni mtoto wake huenda kesho akajirudi na mtoto kunufaika.Nimecheka sana mkuu, huu ndio ukweli. Ndio maana bibie kinamuuma sana jamaa kuvunga. 😊