Hamisa Mobetto; Nilishamwambia mwanangu baba yako ni yule yule ila alikukataa

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mwanamitindo na mfanyabiashara Hamisa Mobetto amefunguka kuhusu sababu za kutomhusisha mzazi mwenzake kwenye malezi ya mtoto wao Dylan, akibainisha kuwa alikataa mfumo wa malezi uliotawaliwa na masharti yasiyo ya haki pamoja na unyanyasaji wa hisia.

Akieleza hali halisi ya uhusiano wao, Hamisa alisema kuwa hakusita kumweleza mwanaye ukweli tangu mapema kwamba baba yake ni yule yule, ingawa mzazi huyo ndiye aliyemkataa mtoto huyo tangu awali.

"mwanangu Dylan hana baba tofauti na yule, na yeye mwenyewe nilisha muambia kuwa baba yako ni yule ila alikukataa, inaumiza ila inabidi tu umuweke wazi akae akijua" .

Hamisa amefafanua kuwa chanzo kikuu cha yeye kuamua kumlea mtoto mwenyewe bila msaada wa baba yake ni kukataa aina fulani ya unyanyasaji ambapo mzazi mwenzake alitaka kumtumia mtoto kama silaha. Alieleza kuwa mzazi huyo alitaka uhusiano ambao pindi anapojisikia kuwa naye humtafuta na kumtaka aende kwake, kitendo ambacho Hamisa amekitaja kama "utumwa" ambao hakuwa tayari kuukubali katika maisha yake.


"Mimi nilicho Kataa ni Ile mtu Hakupendi ila anataka siku akijisikia kuwa na wewe anakutafuta unaenda, huo ndo utumwa ambao niliukataa, Yani atumie hiyo silaha ndo aweze kumlea mwanangu, hiyo Mimi nilikataa niliona kama utumwa, acha hao alio zaa nao waendelee na utumwa huo ila mimi hapana siwezi nitamlea mwanangu bila shaka yoyote"

Msimamo wa mfanyabiashara huyo uko wazi kuwa hayuko tayari kuvumilia masharti ya aina hiyo ili tu apate ushirikiano wa malezi. Aliongeza kuwa ingawa wapo wengine waliozaa na mtu huyo na kuendelea na mfumo huo anaouita wa utumwa, yeye amechagua njia tofauti na kusisitiza kuwa ana uwezo na utulivu kamili wa kumlea mwanaye Dylan mwenyewe bila shaka wala utegemezi wowote.
 
Hapa unataka kusema Tanasha na Ze Boss LEDI huwa wakihitajika wanaitwa kwenda KUTEMBEZEWA RUNGU?
 
" Mandatory DNA test " hii kitu wanawake walio wengi hawaitaki,ila kutwa huwaita wanaume wahuni.

Huyu demu amwambie tu mwanae ukweli, ila wanawake ndio walivyo akiwa na wanaume watano, basi mtoto atapewa mwanaume mwenye hela.

Watu siku hizi hawataki kulea mabao ya watu na haya maswala ya kitanda hakizai haramu hawataki hata kiyasikia.
 
Mimba za kutegesha Wanaume zinawatesa sana
 
Yeye amlee mtoto kama alivyoamua, asimfitinishe mtoto na baba yake. Kusema alimkataa na wakati hapo hapo anasema alikataa masharti, ni fitna hiyo.
Nampa pongezi kumwambia mtoto bba yake halisi, angeweza mwambia vinginevyo tatizo likawa kubwa zaidi kwa mtoto.
 
kashasema mtoto ni wa mond ila we umekazana kusema amwambie mtoto ukweli, Kwani siku alotungishwa mimba ulikuepo kuzuia goli lisimfikie hamisa ndo maan unampinga?
 
Tangu Mwanzo Hamisa alitaka kutumia Mimba na Mtoto kama chanzo cha Mapato, Simba akamruka kimanga🤣
 
Wanawake kwa kulisha sumu watoto ni hatari zaidi ya nyoka. Sasa kuombwa k ndo utangaze mtandaoni?
Mbona mwanzo hukutangaza Hadi umezaa nae? Sasa ni Azizi Ki ndo anakupa kiburi kwa kukubali kulea mabao ya wanaume wenzake walio hai.
 
kashasema mtoto ni wa mond ila we umekazana kusema amwambie mtoto ukweli, Kwani siku alotungishwa mimba ulikuepo kuzuia goli lisimfikie hamisa ndo maan unampinga?
Halafu kusema haina maana kweli mtoto ndio wako,aache kutafuta huruma awajibike basi.

Hakafu hata hawa wachini walisema kama alivyo sema yeye, so kusema haimanishi kama kweli mtoto wa Mond.

View: https://m.youtube.com/watch?v=JfmzXsWH65U&pp=ygUWeW91IGFyZSBub3QgdGhlIGZhdGhlcg%3D%3D
Hii sheria ya Mandatory DNA test US wanaifanyia review ikipita, najua itakuja mpaka nchi za Africa na wanawake wengi mtaumbuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…