Hamisi Heri: Kutoka Uasisi wa TANU 1954 Hadi Azimio la Arusha 1967

Hamisi Heri: Kutoka Uasisi wa TANU 1954 Hadi Azimio la Arusha 1967

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HAMISI HERI KUTOKA UASISI WA TANU 1954, KURA TATU 1958 HADI AZIMIO LA ARUSHA 1967

Familia ya Hamisi Heri imeipatia Maktaba picha ya Hamisi Heri mmoja wa waasisi wa TANU, Tanga.

Picha imepigwa Korogwe mwaka wa 1967 wakati huo Hamisi Heri akiwa Mwenyekiti wa TANU wa Mkoa wa Tanga akikagua miradi ya maendeleo katika siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Tanga kuna Mtaa unaitwa Maua lakini Hamisi Heri hana mtaa.

Ukiuliza nini maana ya Mtaa wa Maua Ngamiani walipotoka wazalendo kama Hamisi Heri, Rashid Sembe, Mohamed Kajembe waliopigania uhuru wa Tanganyika hupati jibu.

Tanga amkeni muokoe historia ya mji wenu.
 
Attachments

  • Screenshot_20240703-220455_Photos.jpg
    Screenshot_20240703-220455_Photos.jpg
    340.6 KB · Views: 12
Sasa mtaa Maua si wamepewa wote walioasisi TANU
 
Sasa mtaa Maua si wamepewa wote walioasisi TANU
Babu....
Kama ni hivyo kwa nini wauite "Maua?"

Jina ambalo lingekuwa na maana ni kama, "Mtaa wa Waasisi" au "Mtaa wa Wapigania Uhuru," jina mfano wa haya.
 
Babu yangu alipigania uhuru mpake kesho hana mtaa.Mimi Ngongo ambaye sikuona utawala wa Mwingereza nina mitaa minne mmoja upo Arusha Njiro na mwingine upo Babati stand ya mabus,Kilema barabara ya kuelekea kanisa Catholic & Morogoro dakawa barabara ya kuelekea kiwanda cha sukari Mbigiri magereza.

Si lazima kila mtaa unasibishwe na wapigania uhuru.Kwanza waliopigania uhuru wametuachia katiba mbaya inayowawezesha watawala kutuibia rasilimali zetu pasipo kushtakiwa.

Walipigania uhuru wa kuwaondoa wazungu lakini wakajivika kilemba cha utukufu wa kizungu.Nchi hii inahitaji uhuru wa kweli.
 
Bora mkoloni mzungu kuliko mkolononi mkora ccm.Mkoloccm ni mwizi,mbinafsi na mchawi.
 
Back
Top Bottom