Hamkani si shwari ndani ya klabu yetu ya Simba ila nachojua Mangungu anapigishwa shoti na wasiompenda

Hamkani si shwari ndani ya klabu yetu ya Simba ila nachojua Mangungu anapigishwa shoti na wasiompenda

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
473
Reaction score
1,682
Mimi sio mshabiki wa Murtaza Mangungu na simpendi kabisa kabisa, kwa sababu hana lugha nzuri, hata sijui kwa wananchi wake jimboni pale Kilwa Kaskazini anawajibu kama anavyowajibu wanachama, viongozi na mashabiki au vip.

Najua kesho Mangungu atakuwa Kilwa kuchukua fomu, tumuombee kwa mungu safari hii asikatwe jina, akikatwa jina bado tunae na asipokatwa anaweza kuwaachia Simba yenu.

Mambo ni mengi sana, uswahili umejaa sana Simba.Very unprofessional

Kila msimu lazima tugombane, tuvurugane, very unprofessional

Murtaza Mangungu ni mwenyekiti wa Simba wala hana shida, ila ukweli ni kuwa marafiki wa Simba ndio hawampendi, hawa marafiki wanajifanya wako naye, wanashirikiana naye na yeye Mangungu anajua wako pamoja kumbe wapi.

Kundi lile la akina poti halina ukweli hata kidogo.

Kundi lile linaona Simba ikipata mafanikio wao wataonekana hawana maana.

Kundi lile la marafiki wa Simba ni watu wabaya sana, sema mashabiki hawajui tu.

Kundi lile limeazimia hakuna mechi ya Simba vs Yanga itachezwa halafu Simba atatoboa, ndio azimio Lao.

Kwanini? Kwa sababu kundi hilo linaamini Simba akifungwa na Yanga mihemko inakuwa mingi sana.

Leo hata Ahmed Ally haeleweki tena kwa mashabiki, imefikia hatua Ahmed anajibizana na mashabiki kwenye page yake baada ya kuona anafedheheshwa.

Mangungu hana baya, wenye ubaya ni waasi ndani ya timu hiyo wasiomtakia mama katika uongozi wake.

Hawampendi Mangungu kwa sababu hana kona kona nao, ss baadhi yao wanajiingiza kwenye timu kiaina, wanashirikishwa kwenye mikakati na baadae wanakwenda kuuza ishu.

Mangungu ni kiongozi, hawezi toka hadharani na kuwasema wanaohujum timu ila anawajua.

Mm nalia sana na hawa akina Poti, wanamzunguka sana Mo, mhindi wa watu anajitoa kweli halafu wajanja wanaenda kumleta Ahoua, Chamou nk.

Hebu fikirieni Simba kweli ni ya kushindwa usajili na Singida Utd, yaan Singida isajili wachezaji wa maana kuliko Simba? Inakuingia akili kweli?

Kwahiyo mchezo ndani ya Simba uko hivyo, Mangungu anafungishwa tu na wale marafiki, marafiki ni watu wabaya sana, hawaonekani lakini wao ndio wauaji wakubwa ndani ya Simba.

Wao ukifanya jambo bila kuwashirikisha wanajitenga.

Mangungu anaongoza Simba katika kipindi kigumu mnooo, ushirikiano kutoka kwa marafiki ni wa kinafiki.

Hatokuja kuifunga Yanga hata siku moja kwa sababu ya umafia anaofanyiwa, kila zuri akifanya anaharibiwa na maadui zake.

Rai yangu kwa mashabiki msikimbilie kufoka foka tu, Mangungu ni jeuri, mkimletea uhuni atawafanyia uhuni.

Cha msingi watafutwe wazee wamuite wamwambie gemu imekukataa, una maadui wengi ndani ya taasisi, huwezi fanikiwq, wewe ni mwenzetu tunakupenda lakin kwa hali ilivyo wapishe wengine tu waendelee, tumuombee kwa mungu kesho jumamosi anachukua fomu pale Kilwa Kaskazini akishinda jina lisikatwe tumuombe
 
Back
Top Bottom