Hamna sehemu watu wanauana na kufa Afrika kama Ethiopia

Hamna sehemu watu wanauana na kufa Afrika kama Ethiopia

Mr Chromium

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2020
Posts
2,761
Reaction score
3,835
Ukitoa DRC au Congo ambayo hadi sasa zaidi ya watu million 12 wameuliwa. Sehemu nyingine ni Ethiopia

Ethiopia watu wanauana kama Kuku kisa ukabila. Serikali ya watigray iliyoongoza kwa miaka 30 ilisababisha ukabila uwe mkubwa kwa kutengeneza serikali au vyama vya kikabila vya majimbo.

Kuna chama cha Watigray na jeshi lake
Kuna chama cha Oromo na jeshi lake
Kuna Amhara na jeshi lake, na majimbo mengine hivyo hivyo
Halafu ndio kuna geshi la Muungano.

Abiy Ahmed kaja kutaka kubadilisha hilo kwa kuweka chama kisicho na ukabila au kisicho cha kikanda ! upinzani mkali ukaanza hasa tigray ambao ndo wameongoza nchi kabla yake.

Vita ya Tigray ilipoisha vikundi vingine kama Fano na Oromo liberation front vikaanza. Kifupi kuleta nchi pamoja ambao wameishi kwa ukabila kwa muda mrefu vita lazima itokee kwani kuna viongozi walikuwa wanafaidika na mgawanyo huo.

Majeshi ya Oromo na Fano yamekuwa yakivamia na kuua raia. Ethiopia imebaki kidogo kumeguka vipande vipande.
 
Attachments

  • AAB40A7B-ACC1-48EB-A5D2-6CAB9B2F8663.jpeg
    AAB40A7B-ACC1-48EB-A5D2-6CAB9B2F8663.jpeg
    592.9 KB · Views: 8
Ukabila ni sumu sana , tena hatari sana kama siku Tanzania ikiweka serikali za majimbo basi ijiandae kwa ukabila.

Hapa TZ ni wapuuzi wachache ndio wakabila hata baadhi ya nyuzi utawaona kujiona bora ya wenzao ..
aukabila na udini ni vita isiyoisha
 
Sisi ukabila wetu unahusika kwenye utani tu basi

Watanzania tumestaarabika sana kanda ya wahabeshi sio wastaarabu ndio maana yanagombana gombana

Sisi ni wanafiki sio wastaarabu, Tanzania ukabila upo sana, na udini pia upo.
Kama ilivyo kwa watu wengine sio kwa watu wote pia huo ukabila na udini.

Tanzania yapo maeneo ajira zinatolewa Kwa ukabila na udini, hutaambiwa ila kwa siri sana ndio Iko hivyo.

Hao wengine wakifanikiwa kulimaliza maana yake wanakuwa wamemaliza kabisa na sio vinginevyo, huku bado tupo kwenye stage za mwanzo za ukabila na tukifikia kwenye peak ndio tutakuwa kama hao.
 
Ukabila ni sumu sana , tena hatari sana kama siku Tanzania ikiweka serikali za majimbo basi ijiandae kwa ukabila.

Hapa TZ ni wapuuzi wachache ndio wakabila hata baadhi ya nyuzi utawaona kujiona bora ya wenzao ..
Nani kakudanganya kuwa serikali za Majimbo zitaleta tribalism?
 
Sisi ni wanafiki sio wastaarabu, Tanzania ukabila upo sana, na udini pia upo.
Kama ilivyo kwa watu wengine sio kwa watu wote pia huo ukabila na udini.

Tanzania yapo maeneo ajira zinatolewa Kwa ukabila na udini, hutaambiwa ila kwa siri sana ndio Iko hivyo.

Hao wengine wakifanikiwa kulimaliza maana yake wanakuwa wamemaliza kabisa na sio vinginevyo, huku bado tupo kwenye stage za mwanzo za ukabila na tukifikia kwenye peak ndio tutakuwa kama hao.
Acha kuongeza upumbavu. Tanzania hakuna ukabila.
 
CHADEMA na wapumbavu wengine wanaoongelea Tanganyika ndo watakaoleta hayo machafuko. Tuwakatae
 
Ukitoa DRC au Congo ambayo hadi sasa zaidi ya watu million 12 wameuliwa.
Sehemu nyingine ni Ethiopia

Ethiopia watu wanauana kama Kuku kisa ukabila. Serikali ya watigray iliyoongoza kwa miaka 30 ilisababisha ukabila uwe mkubwa kwa kutengeneza serikali au vyama vya kikabila vya majimbo.

Kuna chama cha Watigray na jeshi lake
kuna chama cha Oromo na jeshi lake
Kuna Amhara na jeshi lake
na majimbo mengine hivyo hivyo
Halafu ndio kuna geshi la muungano.

Abiy Ahmed kaja kutaka kubadilisha hilo kwa kuweka chama kisicho na ukabila au kisicho cha kikanda ! upinzani mkali ukaanza hasa tigray ambao ndo wameongoza nchi kabla yake.

Vita ya Tigray ilipoisha vikundi vingine kama Fano na Oromo liberation front vikaanza.

Kifupi kuleta nchi pamoja ambao wameishi kwa ukabila kwa muda mrefu vita lazima itokee kwani kuna viongozi walikuwa wanafaidika na mgawanyo huo.

Majeshi ya Oromo na Fano yamekuwa yakivamia na kuua raia.

Ethiopia imebaki kidogo kumeguka vipande vipande

View attachment 3056708
😭😭 Dunia uwanja wa fujo Hawa nikiangalia ni kama wamelala tu, ila aaah acha tu, binadamu tumekuwa wanyama, na wale viumbe ndo wamekuwa siku hizi Wana ubinadamu
 
Back
Top Bottom