Hamna sehemu watu wanauana na kufa Afrika kama Ethiopia

Hamna sehemu watu wanauana na kufa Afrika kama Ethiopia

watu walikua wanapeana michongo kiundugu , ni obvious ni obvious watashea kabila au dini ila usitake kuaminisha umma kwamba ni hali ya hatari kama kenya au ethiopia , angalia tu hata uchaguz wetu mtu hapigiwi kura sababu ya kabila lake au dini yake unless unaongelea visiwani huku bara ukabila na udini upo kiwango kidogo mno

Hao wakenya hawakufika tu hapo ghafla.
Lazima kulikuwa na viashiria na siajabu walidharau kama hivi mpaka wakafika huko.

Hatuwezi kusema tatizo halipo wakati lipo, halijalishi ni kiwango gani tayari ni virus.
 
Jidanganye tu mkuu

Unafiki maana yake ni stage yakulifikia tatizo, ili usilifikie tatizo inabidi ukomeshe huo unafiki.

Stage tuliyopo waliipitia pia hao tunaowasema.
Mkuu kuwa muwazi umeropoka sion cha maana ulichoandka ni wewe ni wale watu mnapenda kuibiza Tz kwa kila jambo
 
Ukabila Tanzania upo sana nafikili ungepitia upya kucheki kwann baba wa taifa aliyakata majina ya watu Fulani waliokuwa na ushawishi kipindi hicho adi wengine wakakimbia nchi eti kisa makabila yao lengo wasigombee urais
 
Ukitoa DRC au Congo ambayo hadi sasa zaidi ya watu million 12 wameuliwa. Sehemu nyingine ni Ethiopia

Ethiopia watu wanauana kama Kuku kisa ukabila. Serikali ya watigray iliyoongoza kwa miaka 30 ilisababisha ukabila uwe mkubwa kwa kutengeneza serikali au vyama vya kikabila vya majimbo.

Kuna chama cha Watigray na jeshi lake
Kuna chama cha Oromo na jeshi lake
Kuna Amhara na jeshi lake, na majimbo mengine hivyo hivyo
Halafu ndio kuna geshi la Muungano.

Abiy Ahmed kaja kutaka kubadilisha hilo kwa kuweka chama kisicho na ukabila au kisicho cha kikanda ! upinzani mkali ukaanza hasa tigray ambao ndo wameongoza nchi kabla yake.

Vita ya Tigray ilipoisha vikundi vingine kama Fano na Oromo liberation front vikaanza. Kifupi kuleta nchi pamoja ambao wameishi kwa ukabila kwa muda mrefu vita lazima itokee kwani kuna viongozi walikuwa wanafaidika na mgawanyo huo.

Majeshi ya Oromo na Fano yamekuwa yakivamia na kuua raia. Ethiopia imebaki kidogo kumeguka vipande vipande.
"Let us agreed that Blacks cannot rule themselves, Whites are born in order to rule and Blacks are born to be ruled."

Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.
 
Ukabila ni sumu sana , tena hatari sana kama siku Tanzania ikiweka serikali za majimbo basi ijiandae kwa ukabila.

Hapa TZ ni wapuuzi wachache ndio wakabila hata baadhi ya nyuzi utawaona kujiona bora ya wenzao ..
Wakiongozwa na wapuuzi wakuu chadema
 
Kule nchini Venezuela wana taka kuleta uzanzibati
 
Sisi ni wanafiki sio wastaarabu, Tanzania ukabila upo sana, na udini pia upo.
Kama ilivyo kwa watu wengine sio kwa watu wote pia huo ukabila na udini.

Tanzania yapo maeneo ajira zinatolewa Kwa ukabila na udini, hutaambiwa ila kwa siri sana ndio Iko hivyo.
H
Kwa jinsi tulivyochangamana sio rahisi hilo kutokea.
Hata ile ya usioe mtu kabila tofauti na wewe siku hizi haipo, watu wa huku wanaoa kule.
 
Kwa sasa hapa nchini kwetu makabila ya watu wa kanda tofauti tofauti yanaunda umoja wa kikabila, et kuchangishana pesa kwa lengo la kusaidiana. Utakuta bango hasa maeneo ya mjini et kikundi cha wasu....., kile kikundi cha waha..... Nk. Huwa napata wasiwasi sana juu hii miungano ya kikabila. I wish I could be a government to stop this nonsense
 
CHADEMA na wapumbavu wengine wanaoongelea Tanganyika ndo watakaoleta hayo machafuko. Tuwakatae
Kuiongelea Tanganyika sio kosa, kuvunjika muungano kwa ajili ya uhai wa nchi huru Tanganyika na nchi huru Zanzibar kama mwanzo sio kosa pia.

Kosa ni kukumbatia haramu ya muungano huu.
 
Tutajie nchi ya Afrika yenye serikali za majimbo isiyo na ukabila na ukanda.

Nchi unakuta iko stable, anatokea watu eti tuigawe kikanda na kuwe na bunge la kila kanda au jimbo, na hapohapo budget ya uendeshaji iongezeke. Nchi yenyewe hata vyoo vya kutosha haina, hata kutengeneza chupi kufunikia matako haijitoshelezi. Wapuuzi.
Hivi unajua msingi wa Sera ya Majimbo? Msingi wake mkuu ni kusogeza karibu huduma, madaraka kwa wananchi, wawe na uwezo wa kujiamulia Mambo yao wenyewe
 
Hivi unajua msingi wa Sera ya Majimbo? Msingi wake mkuu ni kusogeza karibu huduma, madaraka kwa wananchi, wawe na uwezo wa kujiamulia Mambo yao wenyewe
Na hapo kila jimbo hutaka kujitawala, kuwa na jeshi, kuwa na mgombea Urais, kuwa na bunge, kuwa na polisi. Kama ni majimbo kumi kwenye nchi moja baada ya miaka 70 ni nchi 10 zilizowahi kuwa nchi moja.

Swali langu liko palepale. Taja nchi ya Afrika inayojiendesha kwa serikali za majimbo isiyo na ukabila na ukanda.
 
Pembe ya Africa (Somali Peninsula) hiyo zone sio salama lakini hutasikia hata mtu akiongelea maana haina maslahi na wazungu.
 
Na hapo kila jimbo hutaka kujitawala, kuwa na jeshi, kuwa na mgombea Urais, kuwa na bunge, kuwa na polisi. Kama ni majimbo kumi kwenye nchi moja baada ya miaka 70 ni nchi 10 zilizowahi kuwa nchi moja.

Swali langu liko palepale. Taja nchi ya Afrika inayojiendesha kwa serikali za majimbo isiyo na ukabila na ukanda.
hamna
 
Hivi unajua msingi wa Sera ya Majimbo? Msingi wake mkuu ni kusogeza karibu huduma, madaraka kwa wananchi, wawe na uwezo wa kujiamulia Mambo yao wenyewe
usilazmishe kitu usichokijua.
Kwan hamna local gvnt hazilet maendeleo
 
Na hapo kila jimbo hutaka kujitawala, kuwa na jeshi, kuwa na mgombea Urais, kuwa na bunge, kuwa na polisi. Kama ni majimbo kumi kwenye nchi moja baada ya miaka 70 ni nchi 10 zilizowahi kuwa nchi moja.

Swali langu liko palepale. Taja nchi ya Afrika inayojiendesha kwa serikali za majimbo isiyo na ukabila na ukanda.
Afrika Kusini inajiendesha kwa Serikali za Majimbo na hakuna matatizo hayo ya Ukabila na Ukanda kwenye mifumo ya Uendeshaji wa Serikali. Wamejitahidi kuvuka vikwazo hivi.
Jambo la misingi zaidi kwenye suala hili ni kuhakikisha kwamba mnaweka Katiba ya nchi iliyo nzuri, pamoja na kuweka misingi Imara zaidi ya Utungaji wa Sheria za nchi, mifumo iliyo shirikishi kwa Wananchi wote kabisa bila upendeleo, uwazi katika mifumo ya utendaji kazi za Serikali, n.k. Hii inasaidia sana katika kuondoa mitafaruku ya kijamii katika nchi kwa sababu huwa kunakuwepo na Mazingira ya Kidemokrasia na kuaminiana Kati ya Wananchi na Watawala.
 
Back
Top Bottom