Shida vijana /watu wengi hasa Watanzania tunajua kurukia tu na kutoa sababu ambazo tunatunga,hiki ndio tunapata shida hapa Tanzania na kuona watu wanaonewa,tatizo uelewa na elimu yetu ni mgogoro,tunafikiria kwa kuangalia siasa,mahaba kwa watu fulani,duniani kokote kuna taratibu mbalimbali kuhusu viza ambazo karibu zinafanana,ni hapa tu Tanzania ambapo watu hufanya wanavyotaka,unapoomba viza ya kwenda kutembea au kutalii hutakiwi kwenda huko kufanya shughuli yoyote inayoingiza pesa au shughuli ambayo ni ya kikazi,lakini kama unaenda kwenda kufanya maonyesha au kwenda kikazi inabidi uombe viza ya kikazi ambayo ina tozo maalumu.Nawashauri vijana wa Kitanzania kabla hujaomba viza jaribu kusoma maelezo ya hiyo viza,kwenye kuomba viza hakuna mchawi bali mchawi unakuwa wewe mwenyewe ,hawa watu wa kutoa viza na wale wa border control ni watu wazoefu na unapodanganya hujua mapema.Pia jaribu kuangalia vipindi kwenye DStv vinaitwa Border Control ,ukikosea masharti ya viza hata kama ni mmarekani utakataliwa kuingia nchi unayotaka kwenda kwa kosa dogo tu,huku unaweza kupata viza lakini ukanyimwa entry na ukarudi na ndege uliyoenda nayo na kuishia kuona magorofa ukiwa dirishani.