Hamornize ni lini ataacha malalamiko?

Hebu nipe elimu kidogo hiyo company ya ziik inasambaza hizo kazi wapi?
 
Kampuni ya Ziiki ni kampuni inayohusika na usambazaji wa miziki, promotion na kusimamia wasanii barani Africa. Wanasambaza kazi za wasanii kupitia platforms mbalimbali kama spotify, audimack, boomplay n.k
Ok Asante sana Kwa maelekezo mazuri na YouTube pia wao ndio wanasambaza?
 
Hebu nipe elimu kidogo hiyo company ya ziik inasambaza hizo kazi wapi?
Ziiki ni distribution company kazi zake ndio kama hizo alizokutajia Hziyech22 ...sasa bwana Njomba Nchumari anadai anamiliki kazi zake asilimia mia wakati huohuo kuna kampunk ya usambazaji(ziiki) ambayo anafanya nayo kazi wao ndio wanamiliki Royalties (matunda ya kazi ya sanaa) zake na mwisho wa siku wanagawa faida ya kazi husika kufuatana na mgawanyo wa asilimia kwa labels,wasanii,producers,n.k

Sasa Njomba Nchumari anakurupuka kuichafua ziiki media ionekane wananyonya kazi za wasanii na kwenda mbali zaidi kuwa anataka distribution company😃...

Pia anasema anataka Publishing company)(company ambayo itakuwa mmiliki wa mashairi ya nyimbo zake atakazokuwa anatunga) cjui km Njomba hatambui kwamba akishaanza kufanya kazi na hizi publishing company za nje ya label hatokuwa tena na haki ya kutumia mashairi ya nyimbo zake atakazokuwa anatunga bila kuomba hizo publishing houses..kwa hili mimi namshauri afungue Publishing house/company yake mbn ni rahisi tu akienda pale COSOTA? Wasanii kibao wana publishing company zao mfano Gucci Mane ana Davis Delantic publishing LLC,Quavo ana Huncho Yrn Publishing,Nicki Minaj ana Barbie music Publishing..

COSOTA na BASATA inabidi waandae semina wawaelekeze wasanii vitu hivi, ni aibu sana ishu za mikataba ya wasanii kuleta utata kwenye tasnia wakati vyombo vya kusimamia haya vipo kbs,Marekani wasanii wengi wanacheza kwenye asilimia 12 mpk 30 za mgawo lkn huwez kusikia mizengwe ya kunyonyana
 
Tatizo elimu elimu, na huko basta ama cosota wanafikiri ni kwa ajili ya wasanii wadogo wao wakiitwa huwa hawaendi kwenye hizo semina
 
Unajiuliza kama ana mameneja wanaoshindwa kukusanya mirahaba yake hao mameneja kazi yao ni nini hasa?!

Mirahaba ya mitandaoni ndio chanzo chao kikubwa cha mapato haiingii akilini washindwe kukusanya muda wote huo. Watakuwa ni mameneja mazuzu sijapata kuona ....
 
Dogo Kuna coil hazichomi vzur...hata anachoimba sasa hivi hakieleweki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…