Hamornize ni lini ataacha malalamiko?

Hamornize ni lini ataacha malalamiko?

Yaani huyu jamaa kanishangaza sana na hizo post zake inaelekea hata music industry haelewi na haelewi hata Royalties zinakuwaje katika music industry yaan kifufupi yeye na team yake hawaelewi haya masuala...

1..Anasema anamiliki asilimia 100 ya kazi zake wakati hapohapo anasema anacollect kazi zake kwa distribution company(ambayo kaitaja hapo ni ziiki media) hadi hapo kashakosa uhalali wa kumiliki kazi yake kwa asilimia 100 maana hizo distribution companies music royalties zote wanakuwa wanazishikilia wao kazi yao hapa inakuwa tu kugawana rights za royalties kwa songwriters, recording artists, labels, publishers, producers kulingana na mkataba wa aslimia..sasa hatujui mkataba walioingia na hao ziiki media maana sometimes Distributors wanakuwa na hatimiliki ya asilimia mia ya kazi zako sometimes labda wanakupa kiasi ladhaa cha fedha mwanzoni ya kwamba kazi zake zilete hasara au faida hiyo itakuwa haikuhusu wewe umeshakula chako before,sasa hatujui huenda kuna malipo ya advance ya awali Harmo alipokea kajala kammalizia Mmakonde wa watu kashasahau

2.sijamuelewa anaposema anataka distribution company na publishing company..wakati kwa maelezo yake kashasaini mkataba na Ziiki wa distribution hapohapo anatangaza instagram anataka distrobution company asap,Lol! Anasema anamiliki kazi zake asilimia mia na wakati hapohapo ziiki wanafanya distribution ya kazi zake huu mkataba na ziiki kauona na kuusaini kweli huyu mmakonde au kasainiwa mbona kama haelewi anachokitaka!?
Hicho kiazi sigara zake ndio zinampalia sasa hivi.

Badala akae kwa kutulia anaanza kubatle na hadi wanaomsaidia kufanya muziki wake ufike mbali zaidi.

Aangalie asije kupotea mazima halafu aje kuingia kwenye uraibu wa unga kwa kujidanganya kuwa anapunguza stress kumbe ndio anajimaliza.
 
Namkumbuka Mwanasiasa Maarufu Kuwahi Kutokea Tanzania, Mh. Edward Ngoyai Lowassa (Mungu amsaidie Apone Haraka) aliwahi kusema kuwa, Watanzania Hatuhitaji mambo Makubwa na Mengi zaidi ya ELIMU..!!! ELIMU..!!! ELIMU…!!!

Hakuacha Kusisitiza Hilo hata alipowataka watu kuzungusha Mikono, Baada Ya Kumaliza Kuzungusha Mikono bado alisisitizia ELIMU…!!! ELIMU…!!! ELIMU…!!! kwa Watanzania.

Leo Nimemkumbuka Mh. Edward Ngoyai Lowassa baada ya Kuona Malalamiko Ya Harmonize kupitia Insta Stort Yake. Harmonize Analalamikia kutokulipwa Pesa Za Mauzo ya Mziki wake na Kutishia Kutafuta Distribution and Publucation company Mpya Kama kampuni Ya Mzikii haitaweza Kumsaidia.

Ameenda Mbali zaidi na Kusema kuwa hata Kwangwaru ambayo ilifikisha Views Millioni 100 hakupata Hata USD Dollar 1 ya Distrubution and Publication. Ameomba Mzikii wamuoneshe njia Ya Yeye kupata hizo haki zake. Back to the Point, Harmonize Anakosa ELIMU..!!! ??? Au Ameamua Maisha Yake yawe kuwa Kila Mwaka Awe na Jambo…??

Harmonize katika Maandiko yake Ameonesha Kuwaalaumu na Kuwavaa Record Lable ya Wasafi Kama Wanyonyaji na wanaendelea Kumnyonya kupitia Distribution and Publication ya Kazi Zake. Tulisha Jadiri na Kumshauri Harmonize Kuwa Sisi anao Tulalamikia Instagram hatuna Mkataba wake wala Hatuna kitu chochote kinacho Tuonesha Makubaliano waliyo yafanya Kati yake na Wasafi.

Ni vyema Harmonize Akaenda Mahakamani na Kufanya Mambo Yake kimya Kimya Bila Kuwatishia Mzikii kuwa aanaondoka Au ata fight na mtu kama anahisi Ana Haki ya Kupata Anacho stahili. Ni vyema sana hawa wasanii wakawa na ELIMU…!!! Ya Sheria Kuelewa Kwa Undani Mikataba wanayo ingia badala ya kuja Public na kutafuta Huruma Ya watu Wa Instagram kuhisi unanyonywa wakati Sio. Nacho elewa ni kuwa Ukiwa Chini Ya Record label Au Kampuni Yoyote kuna Vitu vingi kisheria unakuwa hauhisiki moja Kwa Moja na Badala Yakd kampuni inakuwa inakusimamia.

Ni wakati sasa Wa Harmonize kukubari kuwa kuna Pahala Alikosea na Hayupo Tena Wasafi. Otherwise afanye Publication ya Makubaliano waliyo yafanya Ili wale waliobobea Sheria Wamsaidie. Management ya Harmonize inakosea Vitu vingi sana na Ipo siku watakuja Kulipa Gharama kubwa sana kama wenye Hizi Kampuni anazo Zishambulia Public wakiamua Kutafuta Heshima Yao mahakamani na Kuchoshwa Kuuliwa Brand Yao. Harmonize Hajafikia Level ya Kuwatishia Mzikii au Wasafi kwasababu Alikotokea Kila Mmoja Anakujua.

Ni wakati sasa wa yeye kuacha Wachumba zake kuwa Ma-manager na Kuwatafuta watu wenye uweledi wamsaidie katika management ya Mziki wake. Huwezi Ukamuweka Mpenzi wako ambaye hata hamjaoana kuwa Manager wako ukategemea mafanikio.View attachment 2525256
View attachment 2525257
View attachment 2525258
Kila mtu huwa analalamika kwa njia zake hata hao anaowalalamikia nao walikuwa wanalalamikia clouds lakini hawakuwahi kwenda mahakaman.
So kulalamika ni jambo la kawaida
 
WCB waliilamikia clouds kwasababu clouds walikuwa pia wana waattack WCB sasa Harmonize nani anamzungumzia? Ile issue ya airport aliongea Sana hakujibiwa na hii pia Wasafi hawajamjibu pia kwanini asimove on? Kama anaona anaonewa si aende mahakamani kitendo chake chakubaki kulalamika tu insta inaonesha lengo lake kuu ni kutafuta attention
 
Mkuu hivi clouds waliwahi waattack wcb hadharani kabisa au kuwasema? Ruge mwenyewe sikuwahi kusikia akijibu tuhuma alizokuwa anarushiwa japo wcb walikuwa wakiwatuhumu mara kwa mara.
So japo hawajibu huenda wanachezeana michezo behind the scene wao ndio wanajua.
Ila hebu tukiachana na harmo kupenda attention hata mm nakubali ni mpenda attention, kwani msanii akiondoka kwemye label akalipa bado label inabaki na haki za publishing au inakuaje. Nauliza tu nipewe elimu ya haya mambo maana mambk ya muziki yako complicated.
Nilishangaa kusoma french montana alilipa $300k kwa ajili ya wimbo wa unforgettable kabla ya kuutoa kama malipo ya sampling fulani imetumika humo.
 
Diamond alifanya interview Times fm akihojiwa na lily ommy ni baada ya kuona japo wamegoma kupiga ngoma zake lakini wanatumia radio yao kumzungumzia vibaya kwenye kipindi Cha shilawadu, kwenye page za clouds pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa clouds kama Diva the boss n.k

Tukija kwenye hiyo issue ya harmonize kwenye mziki kuna vitu viwili mkuu ambapo ni vyamsingi Sana kwenye operation ya label unapoachana na label before ya Muda wako kuisha mlikubaliana na hiyo label kuna kitu unachokifanya ni kununua mkataba na pia kununua haki zako zote, msanii anaweza akanunua mkataba lakini akashindwa kununua haki zake zote za kazi au akanunua baadhi ya haki zake zote unaposhindwa kufanya hivyo inamaana kuwa label ndio anakuwa mmiliki halali wa hizo kazi
 
Yaani huyu jamaa kanishangaza sana na hizo post zake inaelekea hata music industry haelewi na haelewi hata Royalties zinakuwaje katika music industry yaan kifufupi yeye na team yake hawaelewi haya masuala...

1..Anasema anamiliki asilimia 100 ya kazi zake wakati hapohapo anasema anacollect kazi zake kwa distribution company(ambayo kaitaja hapo ni ziiki media) hadi hapo kashakosa uhalali wa kumiliki kazi yake kwa asilimia 100 maana hizo distribution companies music royalties zote wanakuwa wanazishikilia wao kazi yao hapa inakuwa tu kugawana rights za royalties kwa songwriters, recording artists, labels, publishers, producers kulingana na mkataba wa aslimia..sasa hatujui mkataba walioingia na hao ziiki media maana sometimes Distributors wanakuwa na hatimiliki ya asilimia mia ya kazi zako sometimes labda wanakupa kiasi ladhaa cha fedha mwanzoni ya kwamba kazi zake zilete hasara au faida hiyo itakuwa haikuhusu wewe umeshakula chako before,sasa hatujui huenda kuna malipo ya advance ya awali Harmo alipokea kajala kammalizia Mmakonde wa watu kashasahau

2.sijamuelewa anaposema anataka distribution company na publishing company..wakati kwa maelezo yake kashasaini mkataba na Ziiki wa distribution hapohapo anatangaza instagram anataka distrobution company asap,Lol! Anasema anamiliki kazi zake asilimia mia na wakati hapohapo ziiki wanafanya distribution ya kazi zake huu mkataba na ziiki kauona na kuusaini kweli huyu mmakonde au kasainiwa mbona kama haelewi anachokitaka!?
Bado hatujamuelewa mmqkonde
Labda kesho
 
Nilivyomuelewa Harmonise ni kwamba alilipa 600m ili amiliki haki ya nyimbo zake alizozitoa akiwa "Dabliyusibii" ,kumiliki haki means mapato yanayotokana na kazi hizo ambazo tayari ni haki zake zisiwe zinaenda full "Dabliyusibii" ,hao wabaki kama distributor tu na washare % according mkataba wa kusambaza kazi unavyosema na ndio maana anasema kama wameshindwa kazi ya distrubution aachane nao atafute distributor mwingine.

Kinachofanyika ni kwamba dabliyu wanaendelea kupiga fedha kwa kazi za harmnonise as if kama bado yupo kwenye lebo yao wakati tayari alishawalipa 600m kuvunja mkataba nao wa kuwa kwenye lebo na kuendelea nao kama distributor.
 
Huyu bwana mdogo naona mwisho wake kuwa mbaya na inaoneka hana hela za kumiliki hayo marangeL kumbuka ili nyumba aliyokuwa akiishi alikuwa anajitapa nayo Sana lakini mwisho alikimbia bila kulipa kodi
Daaaaaah,yaani hela alizokuwa anaziteketeza kwenye bata zake,sasa hv anazikumbuka.

Unajua ukiwa mjini inatakiwa uishi kwa akili sana.

Ukiwa nazo ishi kama boya.

Starehe za mjini huwezi kuzimaliza.
 
Nilivyomuelewa Harmonise ni kwamba alilipa 600m ili amiliki haki ya nyimbo zake alizozitoa akiwa "Dabliyusibii" ,kumiliki haki means mapato yanayotokana na kazi hizo ambazo tayari ni haki zake zisiwe zinaenda full "Dabliyusibii" ,hao wabaki kama distributor tu na washare % according mkataba wa kusambaza kazi unavyosema na ndio maana anasema kama wameshindwa kazi ya distrubution aachane nao atafute distributor mwingine.

Kinachofanyika ni kwamba dabliyu wanaendelea kupiga fedha kwa kazi za harmnonise as if kama bado yupo kwenye lebo yao wakati tayari alishawalipa 600m kuvunja mkataba nao wa kuwa kwenye lebo na kuendelea nao kama distributor.
Kuna kununua mkataba na kununua haki za kazi kafanya vyote viwili? au alinunua mkataba akasahau kununua haki za kazi ili ndio swali la msingi maana naona kwenye maandiko yake kachanganya mambo mengi kwa watu mmoja na kuna wakati anaconfuse hoja zake za malalamiko
 
Ndiyo mkuu ,ndiyo maana akatoa mil 600 na akakabidhiwa hadi accounts zake za social media azirun mwenyewe means alipewa hadi haki miliki za kazi zake alizotoa dabliyusibi.
 
Back
Top Bottom