Hawa ni watu ambao wengi wao wametoka familia duni kiuchumi na kielimu lakini kwa uweza wa Mungu wakainuliwa kupitia vipaji vyao. Ukiondoa vipaji walivyo navyo karibu wasanii wote hawana taaluma yoyote ya kuweza kuingiza kipato. Wanajipatia riziki kupitia vipaji. KUWALAUMU NA KUWASHAMBULIA KWA MANENO MAKALI sio sahihi na ni dhambi kubwa sana kisa tu wamesimama na CCM.
Isitoshe wao kama raia wengine wa Tanzania wana haki ya kikatiba ya kusimama na chama chochote cha kisiasa wanachotaka. Sio lazima wawe CHADEMA ndo waonekane wako sahihi. Ikumbukwe pia CCM ndo chama chenye kazi nyingi na hawa wasanii ambapo huwalipa. Msanii aache hela za CCM akapige miayo CHADEMA si atakuwa kalogwa? Wasanii na wanamichezo kazi zao ni za kustaafu mapema hivyo wanatakiwa wapigane sana kusaka hela mapema bila kuvunja sheria. Juma Nature aliyekuwa the top musician leo hii hata top 50 ya wanaotajwa hayupo. Wasanii mliopo CCM mnafanya kitu sahihi kwa wakati sahihi.
Cha mwisho ni kuwa hizi serikali zetu za kijamaa huwa ndo kila kitu kwenye nchi. Serikali ipo kwenye kila sehemu. Serikali zetu za kiafrika zikiamua kukuzingua utapata taabu. Na msanii kama mtu mwenye ushawishi kwenye jamii atakuwa mjanja endapo atakuwa upande wa serikali. HUU NI UKWELI MCHUNGU. Muulizeni Koffi Olomide alivyoshushwa kwenye Mercedes benz na kucharazwa viboko hadharani. Sio poa