Hamuwezi mkatangaza Maandamano mapya Desemba 9, 2025 halafu mtake Lissu aachiwe. Jaribuni kuwa Strategical katika Mipango yenu

Hamuwezi mkatangaza Maandamano mapya Desemba 9, 2025 halafu mtake Lissu aachiwe. Jaribuni kuwa Strategical katika Mipango yenu

Umenikumbusha jamaa mmoja hivi hapa jf anajiita mtibeli. Kabla ya MO29 alijifanya mchambuzi wa masuala ya maandamano kama wewe. Sasa hivi simuoni
Usinifananishe na huyo Mpumbavu mwenzako tafadhali.
 
Nikiwa nawachana kwa kuwaambia Ukweli badala ya Kukubali makosa yenu na Kunielewa mnakimbilia Kunitukana, Kunidhihaki na Kunishambulia.

Hivi Logically tu baada ya kutangaza Maandamano mengine tarehe 9 Desemba, 2025 tena huku mkitishia na kuweka mikakati yenu wazi Mitandaoni mlitegemea kweli leo hii Tundu Lissu aachiwe? Mbona mnakuwa hamna Akili hivi?

Hivi mnajua kuwa msingeanza tena haya Matangazo yenu ya Kuandamana tarehe 9 Desemba, 2025 huenda mngerahisisha hata Tundu Lissu kuachiwa leo kama ambavyo Yeye mwenyewe pia alikuwa akitegemea?

Kwakuwa hamna Akili sasa ngojeni leo niwachane kwa kuwapa Ukweli Mchungu ili mbadilike.

Kwa taarifa yenu kama kuna Kosa kubwa mnalolifanya ni kupanga Mikakati yenu Kiuwazi kabisa ya kupambana na Dola kitu ambacho technically kinawarahisishia Wao kujua jinsi ya Kuwakabili.

Lingine hata katika huo Upangaji wenu wa hii mikakati yenu ambayo kila mara Inabuma tu pasipo kujua Kwenu mnawajumuisha hata na Maadui zenu ndani kitu ambacho mmeshindwa kukijua.

Kwa mfano Mitandaoni kote sasa kuna Watu wa Mikakati wamepandikizwa na wanachokifanya ni kuja na Mada za Maandamano yenu hayo na kutia Chuki ili tu kupata Maoni ya wale Team Mihemko na Bendera Fuata Upepo kisha wao wanajua kila mlipangalo.

Mlichobahatika hasa ni kuwa tu Wahamasishaji hodari wa Maandamano na kutoa Matamko ya Mikwara Mbuzi ila bado hamna Strategists wa kufanikisha Mipango yenu hiyo.

Hakuna ambaye hajui kuwa Tundu Lissu ana Ushawishi mkubwa mno na kwa kilichotokea tarehe 29 Oktoba, 2025 kama leo angeachiwa basi angeweza kusababisha Jambo lingine Kubwa (Zuri au Baya) kutokea ambalo pengine pia lingeweza kuwa baya Kwake binafsi hivyo kwa maana nyingine hata hii Kesi yake Kuahirishwa ina faida fulani Kwake japo ukiwa Mvivu wa Kufikiri (Mpumbavu) huwezi kuliona kwa hii Angle nyingine ya Kifikra.

Ushauri wa bure na wa Thamani kabisa nawapeni leo kuwa acheni kutangaza au kuweka wazi mikakati yenu, tafuteni Strategists wa uhakika, acheni kutoa Matamko ya Vitisho na yaliyojaa Visasi vya Mihemko (kutoka kwa Keyboard Warriors) bali Hekima na Busara zinahitajika zaidi kukabiliana na Jambo mnalolitaka na kamwe siyo Vurugu, Fujo na Vita hata kama limewagharimu ama kwa bahati mbaya au kwa makusudi au kwa kutokujua Wenzetu ambao mpaka sasa idadi yao kila Mtu anayo yake Kichwani mwake.

Kwa wale mtakaonielewa Asanteni na tupo pamoja na kwa wale ambao hamtanielewa na mtatanguliza Chuki, Hasira na Mihemko juu yangu na kuamua Kunitukana nanyi pia nitawashukuruni ila nina uhakika hii Dozi itawasaidia na mkitulia kabisa na kuelewa yote niliyoyaelezea hapa basi nawahakikishieni hii Vita ya Kihaki mtaishinda Kiurahisi bila ya hata ya Kuwatajirisha bure Wauza Majeneza Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Iringa, Morogoro na Dodoma.

Nimemaliza.
Maandamano ni lazima, Samia na mwanawe Abdul waondoke na washtakiwe kwa crime against humanity. Suala la Lissu kuachiwa halihusiani na maandamano. Acheni ujinga. Kwani Lissu alikamatwa kwa ajili ya maandamano? Tutaandamana hadi kieleweke, mkitupiga, safari hii mtapokea kipigo kikali. TUMEWACHOKA.
 
Umenikumbusha jamaa mmoja hivi hapa jf anajiita mtibeli. Kabla ya MO29 alijifanya mchambuzi wa masuala ya maandamano kama wewe. Sasa hivi simuoni
Bado yupo. Still spewing his nonsense while pretending to know everything. Narcistic Personality Disorder is a hell of a disease!
 
Uzi wa mlamba asali.
Kipindi hiki ni kigumu sana kwa waliozoea kuishi kwa kulamba matako ya watawala.
Wanatapatapa sana.
 
Me sijamsikia kiongozi wa Chadema hata mmoja akiitisha maandamano.
Mbinu yao ni kuifungamanisha CHADEMA na maandamano ili wakitaka kutumia nguvu au maridhiano feki wawashurutishe au wawaite mezani CHADEMA.

Sasa safari hii maandamano yanaratibiwa na wananchi kuyazuia ni kutimiza matakwa ya wananchi. Wanashindwa kukubali ukweli kwamba umefika wakati wa watanzania kuamka. Badala ya kutekeleza matakwa ya wananchi wanabaki kupoint watu tu mara CHADEMA mara Mange kimambi
 
Ifike muda hawa wahenga wa JF wastaafishwe kinguvu, wengi wao machizi km hili cenge
 
kwanini Maandamano ya wananchi mnayaita ya chadema kwa nini kwamba wananchi hawajui haki zao kwamba wananchi ni mazuzu sometimes watu wanamuaga kutulia kuona kama mtabadilika ila wakichoka Mfano Magufuli alifungua ufahamu wa watu Pale aliposema hii Nchi ina pesa nzudugu zangu sema wizi tumefanya miradi mingi ya maendeleo mnainona Utumishi kwa watumishi wa Umma mnauona uwajibikaji Wananchi wanajua sema waliona mtabadilika baada ya kueleza Polepole aliongea vitu watanzania walimuelewa
 
Lissu anahusiana vipi na haya maandamano?
 
Aliyekuambia kua Lissu alitegema kuacjiwa ni nani?

Mtu kaja mahakamani kajiandaa na kaweka mapingamizi nna kajiandaa mpaka mwisho wa kesi, wewe unakuja na ngonjera za kipumbavu
 
Back
Top Bottom