Hamza Bendelladj "the smilling hacker"

Hamza Bendelladj "the smilling hacker"

The Monk

Platinum Member
Joined
Oct 12, 2012
Posts
20,242
Reaction score
45,930
Mshukiwa mmoja wa udakuzi wa komputa ambaye anasakwa na idara ya ujasusi nchini Marekani, FBI, kuhusiana na madai ya kuiba mamilioni ya madola kutoka benki za Marekani, ili kufadhili maisha ya anasa, amekamatwa mjini Bangkok Thailand.

130107175158_hamza_bendelladj__304x171_afp_nocredit.jpg

Hamza Bendelladj baada ya kukamatwa na polisi mjini Bengkok

Shirika hilo la FBI, limekuwa likimsaka mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 24, Hamza Bendelladj, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya komputa, kutoka Algreia kwa zaidi ya miaka mitatu.

Ripoti zinasema mshukiwa huyo amekuwa akiiba kutoka benki hizo za Marekani tangu alipokuwa na umri wa miaka 20.

Polisi nchini Thailand wanasema mshukiwa huyo, Bendelladj amekiri alitumia fedha hizo kuisha maisha ya starehe na anasa.

Bendelladj, anazuiliwa katika kituo kimoja cha polisi katika uwanja wa ndege mjini Bangkok baada ya kuwasilia kutoka Malaysia akiwa safarini kuelekea Misri.

Utawala wa Marekani unamtuhumu kuhusika na wizi katika akaunti za watu binafsi katika zaidi ya mabenki 217 na taasisi wa kifedha kote duniani na kusababisha hasara ya mamilioni ya madola.

Mkuu wa polisi nchini Thailand amesema mshukiwa, alikamatwa katika uwanja mkuu wa ndege ambako alisema yeye pamoja na familia yake wamekuwa likizoni.

Polisi wanasema wamenasa komputa mbili, kifaa kimoja cha tarakilisha, simu ya sate lite na vifaa vingine vya komputa kutoka kwa mshukiwa huyo.

Ripoti zinasema Bendelladj anatarajiwa kusafirishwa hadi nchini Marekani, katika Jimbo la Georgia ambako mahakama moja ilitoa kibali cha kukamatwa kwake.

Ndelladj anatarajiwa kusafirishwa hadi nchini Marekani, katika Jimbo la Georgia ambako mahakama moja ilitoa kibali cha kukamatwa kwake.

SourceBBC
 
ImageUploadedByJamiiForums1457895816.122403.jpg

Huyu kijana aliye pichani ni kijana wa Ki-Aljeria aliyesumbua sana taifa la Marekani na nchi za Ulaya.Alikuwa amesoma na kupata degree ya computer science.Alitengeneza program ya computer inayofanya kazi kwenye windows inayojulikana kama Spy Eye, ambayo ni kirusi kinachoweza kuiba taarifa za kibenki hivyo kumwezesha kufanya miamala batili kutoka akaunti za watu mbalimbali.

Aliweza kuiba ela kutoka benki mbali mbali USA na nchi za Ulaya kama Ufaransa, kiasi kinachokadiliwa kuwa $4 billions, ambazo alizigawa kwa mashirika ya kusaidia jamii Afrika na Palestina, ikiwa ela nyingi aliyapatia mashirika ya Afrika na $280mils aliyapatia mashirika ya Palestina.

Mbali na hilo alidukua system ya kutoa Visa ya Ufaransa akawapatia Visa vijana wa Algeria waliokuwa wanahitaji visa ili waweze kuingia Ufaransa.

Pia alidukua tovuti ya serikali ya Israel na kuweka ujumbe uliokuwa unapinga Israel kukalia maeneo ya Palestina.

Hamza alianza kutafutwa baada ya kujulikana pale alipomuuzia copy ya SpyEye agent wa CIA aliyejifanya naye ni hacker. Alikuwa kati ya mahacker 10 waliokuwa wakitafutwa na alikatwa akiwa Thailand akapelekwa Marekani kujibu mashitaka. Israel ilimtaka akaisaidie kutengeneza upya system yake ya tovuti zake ili zisidukuliwe kwa ahadi kwamba serikali ya Marekani itafuta mashtaka yake lakini Hamza alikataa kufanya hivyo wala kutoa ushirikiano.

Alikubali mashtaka mpaka sasa hajahukumiwa ila hukumu yake inaweza kuwa kifungo mpaka cha miaka 30.Huyu ndiye Hamza ambaye kwa wengine wanamuona shujaa wakati wengine wakimuona mwizi.Aliwahi kusema kuwa yeye haoni maana ya kuwa na pesa nyingi wakati kuna watu wana uhitaji wa pesa kwa ajili ya chakula.

UPDATE
Mwaka jana alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela na miaka mitatu ya uangalizi atakapoachiwa.
 
View attachment 329536

Aje TZ tunaibiwa sana na Mabepari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Robin Hood of our Time
 
2d05378715b470840a71694cee5ecc1e.jpg
ff6c66c2d3908b1f028bc4341dfc230b.jpg
mkuu mbona wamarekani walishamuuwa siku nyingi walimpiga kitanzi hiyo kufungwa miaka 15 umetoa wapi sasa hiv ni mifupa tu akuna kitu tena
Siyo kweli hakuuawa na hakuna adhabu ya kuua mtu kwa kosa na wizi wa kimtandao hiyo ni habari ya uongo ilikuwa hoax.
Hiyo picha uliyoweka iko edited siyo picha halisi.

Hacker Hamza Bendelladj sentenced to 15 years

Social Media Spammed with Hamza Bendelladj Death Sentence

US bank hackers get long jail term - BBC News

Haya nimekuwekea links tatu moja ya aljazeera nyingine bbc na nyingine ni ya kukuonyesha kuwa habari za kunyongwa zilikuwa ni uongo tu wa kimtandao.
Hakuna adhabu kama hiyo Marekani kwa kosa la wizi wa kimtandao adhabu kubwa ambayo angepata ilikuwa kifungo cha miaka 65 na kulipa faini.
 
n

nadhani wamarekan naskia walifoji kifo chake
Hakuna cha kufoji kifo na hawakuwahi foji jamaa alifungwa miaka 15 yeye na mwenzake waliyekuwa wanashiriliana ambaye ni mrusi naye akala mvua 9.
Hizi habari za kunyongwa zilizagaa mtandaoni kabla hata ya hukumu yake ambapo wahusika walizikanusha.
 
Vichwa kama hv haviuliwagi, wenzetu wanavitumia kwenye shughuli zao za kisayansi.
 
0fd8e369bd0a48fbb1852d5f6bf90a00_18

"Siku ya tarehe isiyojulikana, lakini inaweza kuwa tarehe 21-02-2011 mpaka tarehe 24-02-2011 , tarehe kamili haifamiki na mahakama ya Grand Jurry katika wilaya ya Georgia and sehemu nyingine, Mtuhumiwa HAMZA BENDELLADJ aka Bx1 alisaidiana na kusababisha na wenzake wanaojulikana na wasiojulikana na Mahakama, kwa akili zake timamu na kwa hiari yake alidukua kompyuta bila kuruhusiwa na akapata taarifa kutoka kwenye kumpyuta inayolindwa kwa lengo la kujinufaisha kiuchumi"-Maneno hayo yakisema na hakimu mahakama ya Georgia chini ya Sally Quillian Yates

Mwishoni hukumu inatoka baada ya HAMZA BENDELLADJ kuwa na makosa 14 yaliyomtia hatiani huku akihukumiwa miaka 15 jela pamoja na mshirika wake aliyejulikana kwa jina la Aleksander Andreevich Panin aka Gribodemon kuhukumiwa miaka tisa jela.

JE HAMZA BENDELLADJ NI NANI?

1b33c319000005dc-3497928-image-a-83_1458257525323

Siku ya Ijumaa ya tarehe 3 June 1988 katika eneo la Tizi Ouzou, Kouba, nchini Algeria ndio DANIEL HAMZA BENDELLADJ elimu yake alisomea katika nchi yake ya Algeria na alikuwa na Stashahda ya Uhandisi wa Kompyuta, Lakini katika kuhitimu Stashahada yake aliwahi kufanya kazi ya Kompyuta maintainance kwa muda wa miaka mitatu. Jina lake la Code ni Bx1, pia waandishi wa habari walimpa jina la Smilling hacker kwa kuwa muda wote anatabasamu japokuwa alikuwa chini ya polisi.

Hamza alikuwa na mke pamoja na mtoto mmoja lakini haijulikani wanaishi wapi.

Baada ya kutoka kufanya kazi kama computer maintainance baadae Hamza alianza kazi ya kudukua (hack) kompyuta za mabenki mbalimbali na kuiba pesa za kusafirisha kwenye akaunti yake, Aliwezeje kufanya hivyo?

Hamza alitengeneza Trojan Horse Virus, ambapo alikuwa anaingia kwenye kompuyta yoyote ile na kuiba taarifa za watumiaji (username & password) baadae alikuwa na system ya ATS(Automated Transfer System-along Zues trojan) ambayo kazi yake ni kuhamisha pesa automatically mara moja tu atakapo ingia (account login).

Inahamika kuwa alifanikiwa kudukua benk na taasisi nyingine za kifedha jumla 217 na aliiba zaidi ya dola million mia tatu, lakini katika akaunti yake alikutwa na dola million kumi. Pia Hamza alikuwa ni moja ya unethical hacker (wadukuzi wasio na maadili) ambayo orodha ilitolewa na MICROSOFT kuwapa polisi wa Marekani.

MAISHA YA HAMZA
Hamza alikuwa anaishi katika Grand hotels lakini pia alikuwa anaishi maisha ya kifahari ambapo alikuwa anasafiri na ndege siti za first class. Baada ya kuanza kutafutwa na maaskari wa kimarekani Hamza alikuwa kila siku anafanya kazi ya kubadili IMEI namba ya simu yake aina ya Iphone na kubakia anonymous.

Hamza alikutana na rafiki yake mwenye asili ya kirusi Aleksander Andreevich Panin kwa kushirikiana wakatengeneza software iliyojulikana kama SPYEYE ambayo ilikuwa inaiba pesa, Pia alikuwa anawauzia wadukuzi (hackers) wengine na ilikuwa inatiumika kama BOTNET.

Nini BOTNET? Kwa lugha ya kompyuta bot maana kifupi cha ROBOT na net ni NETWORK kwahiyo botnet ni mtandao wa maroboti ambao unaunga idadi ya watu mfano kumi halafu wanakuwa controlled na server/computer moja.
Kirusi hiki cha SPYEYE inahaminika kilidukua na kuathiri zaidi ya kompyuta million hamsini. Lakini mpaka leo hii software ipo katika black market inauzwa kwa dola elfu kumi.

Kwa pamoja Hamza na rafiki yake Panin walikuwa na kundi la chini (underground group) ambalo ni kikundi cha hackers ambao ni unethical inaitwa Darkode.com, pia wawili hawa walijulikana kama legend katika dark world (rejea hapa kuhusu dark world).

PESA ZA HAMZA ZIKO WAPI?
Hamza aliiba taasisi karibu 217 lakini alikuwa na utajiri wa dola million kumi, pesa nyingi alikuwa anaopeleka Algeria, sehemu yenye vita Syria, Palestina nk kwahiyo yeye chache tu ndio alikuwa anatumia kati ya nyingi alizoiba..

KUKAMATWA KWA HAMZA

hacker-algc3a9rien-hamza-bendelladj-jpg

Hamza alikamatwa nchini Thailand katika uwanja wa ndege wa SUVARNABHUMI ambapo alikuwa na safari ya kutoka Malaysia kwenda Algeria, ambapo makubaliano kati ya Marekani na Thailand yalifanyika na kumpeleka Hamza mpaka nchini Marekani, ilikuwa vipi mpaka jamaa kukamatwa? Kuna ajenti wa alijifanya yeye ni underground hacker kwahiyo anataka kununua SPYEYE ndio alikuwa anaweza kuongea na Hamza na alifanikisha kukamatwa kwa Hamza.

Panin pia alikamatwa mwaka 2013 katika uwanja wa ndege wa Georgia International Airpot na wote kwa pamoja wakakutwa wapo chini ya polisi.

Baada ya kukamatwa HAMZA baadhi ya watu ambao wanamsapoti wali-hack website ya Air France pamoja na ile ya Virginia University, wakiwa wanashinikiza kuwa Hamza aachiwe huru, na katika mitandao ya kijamii kulikuwa na hashtag kama Freepalestine na ile ya FreeHamzaBendelladj, na vyuo vya nchini Algeria wanampongeza na kumsapoti huku wakimchukulia kama shujaa wao.

HAMZA AMENYONGWA?

Crist%25C3%25A2o

Hukumu ilikuwa inaonyesha kuwa Hamza ataenda jela kwa muda wa miaka 15, lakini baadae ukaja uvumi kuwa Hamza kanyongwa, Lakini balozi wa Marekani nchini Algeria alikanusha madai hayo na kusema kuwa kuna adhabu ya capital kwa kosa kama hilo kutokana na sheria za Marekani.
 
Back
Top Bottom