Hamza Johari aapishwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Rais Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 5, 2025, amemuapisha Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Uapisho huo umefanyika Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Hamza Johari aliteuliwa na Rais Samia kushika wadhifa huo Novemba 3, 2025.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye mshauri mkuu wa Serikali katika masuala yote ya kisheria.

Ndo unaenda kupitia shauri la heche la ugaidi ashauri serikali?
 
Back
Top Bottom