Hamza Mohamed Hassan azikwa makaburi ya Kisutu, Dar. Mazishi yachelewa kutoa risasi zilizokwama mwilini

Hamza Mohamed Hassan azikwa makaburi ya Kisutu, Dar. Mazishi yachelewa kutoa risasi zilizokwama mwilini

Hamza Mohamed Hassan aliyefanya mauaji pale Selender bridge anazikwa leo na waislamu na rafiki na ndugu zake.

====

Dar es Salaam. Mwili wa Hamza Mohammed aliyefariki dunia katika tukio la majibizano ya risasi kati yake na jeshi la Polisi amezikwa leo Jumapili Agosti 29, 2021 saa 2:30 usiku katika makaburi ya Kisutu.

Mwili huo umezikwa baada ya kuswaliwa katika Msikiti wa Mamuur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Awali mwili huo ulitarajiwa kuzikwa saa 7 mchana katika makaburi hayo, lakini msemaji wa familia Abdulrahm Hassan alisema mwili huo ulichelewa kwa sababu ya kazi ya kutoa risasi zilizokwama.
View attachment 1915450
Chanzo: Mwananchi Online
Hili lilipaswa kutupwa baharini kama osama au hata kutupwa porini likaliwe na fisi.
 
Mkorinto siku ile polisi baada ya kumpiga na mabomu ya machozi walikuwa wanaweza kumpiga risas ya mguu ili kumkamata.lakn wakaamua kumuuwa.msema peke mshindi.ILA HUU NI UKUMBUSHO TU KUWA JASHO LA MTU HALIENDI BURE.
Polisi walifanya ilivyotakiwa. Aishie kwa upanga atakufa kwa upanga
 
Ndio Mkuu ulisemalo ni kweli inafika muda wananchi uvumilivu unawashinda Polisi wa nchi nyingi ni Vimeo Sana Mkuu,
Kama unakumbuka Yale ya Sudan Polisi kumkingia kifua yule dhalimu Omary Albashir
Lakini mwisho wa siku wakonekana takataka wajeda wakachukua nchi Kwa nguvu
Sijui sahizi wanaishije wanafiki wale au walipinga u turn kuendana na watawala
Vizabi zabina wale hawana wanalolisimamia kazi Yao kupokea amri za wanasiasa uchwara na kuumiza wananchi bila kutafakari maumivu ya wananchi wa hali ya chini

Shame to all Policemen!

lazima ujue kuanzia leo ili usiendelee kuumia kisaikolojia.

polisi wa nchi ni meno ya utawala wowote ule,bila polisi kiongozi anapoteza amri kwa wananchi wake,lakini bina jeshi rais anapoteza amri kwa nchi nyingine.

so usiulize wanaishije baada ya nchi kupinduliwa,uliza pia wanajeshi watiifu kwa serikali wanakenda wapi baada ya serikali yao kushindwa!!!
 
Hata wewe utakufa siku iwe kwa korona ama moyo. Unawezakufa ukiwa umejikunyata kinyonge lakini haitokusaidia usife. Fikiria kuna watu waliishi zaidi ya miaka 90 kama Mugabe lakini mwishoe walikufa na kuzikwa. Chaugua tu unavyokufa - kishujaa ama kinyonge. Usimwone Hamza mjinga kwa kufa kishujaa.

kafa kishujaa kwa kuua askari,we mbuzi kweli!!

mkiitwa magaidi mnamind,kwa mtu timamu hamza amekosea,kwa magaidi na wagonjwa wa sonona hamza ni shujaa wao.
 
Ccm
Yaani sijui kwa nini tunahubiri chuki. Maoni ya humu yanachukuliwa ama kutoka ufipa au lumumba; yaani misamiti ya chuki tu, eti chagademaa, sukumaagang nk.
Nikiona mwelekeo huu nasikitika sana. Kwa nini?

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Ccm ndio asili ya chuki ya kitaifa na muasisi wa chuki ni John Joseph pombe magufuli
 
Back
Top Bottom