Hamza Mohamed Hassan aliyefanya mauaji pale Selender bridge anazikwa leo na waislamu na rafiki na ndugu zake.
====
Dar es Salaam. Mwili wa Hamza Mohammed aliyefariki dunia katika tukio la majibizano ya risasi kati yake na jeshi la Polisi amezikwa leo Jumapili Agosti 29, 2021 saa 2:30 usiku katika makaburi ya Kisutu.
Mwili huo umezikwa baada ya kuswaliwa katika Msikiti wa Mamuur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Awali mwili huo ulitarajiwa kuzikwa saa 7 mchana katika makaburi hayo, lakini msemaji wa familia Abdulrahm Hassan alisema mwili huo ulichelewa kwa sababu ya kazi ya kutoa risasi zilizokwama.
View attachment 1915450
Chanzo: Mwananchi Digital