Remote,
Tatizo kipaji nilikuwa sina sikuweza kufikia viwango.
Lakini wenzangu wengi walifika hadi kileleni kabisa.
Ikawa wao wakitoka timu ya taifa na Adidas mpya
mie wananitupia za zamani na bukta zao.
Wengi wa rafiki zangu hawa wametangulia mbele
ya haki.
Wapumzike kwa amani.Remote,
Tatizo kipaji nilikuwa sina sikuweza kufikia viwango.
Lakini wenzangu wengi walifika hadi kileleni kabisa.
Ikawa wao wakitoka timu ya taifa na Adidas mpya
mie wananitupia za zamani na bukta zao.
Wengi wa rafiki zangu hawa wametangulia mbele
ya haki.
Remote.Wapumzike kwa amani.
Kashata,Mzee Muhammed nimekupata juu ya lengo la uzi wako ni kuonyesha ulimwengu mchango wa akina sykes ktk kupigania uhuru ambapo walisahaulika kwa bahati mbaya au maksudi
Mzee ms nimekuelewa vema, mimi naona uje utupatie hostoria na michango yao katika kupigania uhuru wanaharakati wote uliowataja apo juu ili tuweze kuwafahamu kwa undani zaidiKashata,
Historia hii si ya akina Sykes peke yao.
Unajua katika historia ya uhuru na historia ya asili ya vyama vya siasa
Tanganyika huwezi ukaitafiti na kuandika kwa uhakika bila kuitaja AA.
Huwezi kuitaja African Association bila kumtaja Kleist Sykes.
Huwezi kumataja Kleist bila kuwataja watoto wake kwa kuwa wote
walishiriki katika uongozi wa African Association na kisha kuasisi TANU.
Lakini pia ukiwaleta hawa wanae itakubidi uwalete vijana wenzao wa
wakati wao waliokuwa katika siasa kama Hamza Mwapachu, Dr.
Kyaruzi,Tewa Said Tewa, Zuberi Mtemvu, Dr. Michael Lugazia,
Dossa Azizi, Dr. Wilbard Mwanjisi, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dustan
Omari, Dr. Luciano Tsere, Kasella Bantu kutaja majina machache.
Lakini tena na hili lina nafasi ya peke yake hutoweza kuwafikia wazee
kama Jumbe Tambaza, Mwinjuma Mwinyikambi, Mshume Kiyate,
Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Bi. Tatu
biti Mzee, Bi. Titi Mohamed na wengineo bila kupita kwa Abdul Sykes.
Haya yote ni kwa kuwa kwa wakati ule Tanganyika inaamka katika siasa
za utaifa hawa ndiyo walikuwa katika uongozi wa TAA na walikuwa watu
maarufu katika mji wa Dar es Salaam.
Dar es Salaam ya wakati ule Uislam ulikuwa na nguvu sana mgeni yoyote
asingeweza kufanya lolote bila ya kuungwa mkono na watu hawa.
Ukweli ni kuwa bila Abdul, Nyerere asingepokelewa.
Nitakupa mifano miwili.
Erika Fiah
Mwaka wa 1933 Kleist aligombana na Erika Fiah katika uongozi wa AA
na Kleist akajiuzulu uongozi na Fiah akachukua nafasi ya Kleist ya katibu.
Rais alikuwa Mzee bin Sudi.
African Association haikuweza kufanya kazi kwa ufanisi na Mzee bin Sudi
ilibidi amwandikia Kleist barua kumsihi arudi katika uongozi.
Barua hii ya mwaka wa 1933 mimi nimeisoma na Mzee bin Sudi ameandika
kwa kuanza na ''Bismillah Rahman Rahim.''
Kleist alirudi katika uongozi.
Mwaka wa 1953 Nyerere alipochukua uongozi wa TAA kutoka kwa Abdul
Sykes chama kilikufa ikabidi juhudi zifanyike kukiweka chama katika hali
madhubuti hadi kufikia kuunda TANU.
Kwa kuhitimisha.
Chuo Cha Kivukoni kilipoandika historia ya TANU haya waliyajua na ndiyo
maana kitabu kizima Abdul Sykes alikwepwa kutajwa na historia ikaanza na
Nyerere kwani walitambua wakimtaja Abdul na kueleza historia yake itabidi
wamtaje na baba yake na wengine wote kama nilivyoeleza.
Hili hawakulitaka.
Kashata,Mzee ms nimekuelewa vema, mimi naona uje utupatie hostoria na michango yao katika kupigania uhuru wanaharakati wote uliowataja apo juu ili tuweze kuwafahamu kwa undani zaidi
Maalim Faiza,Alama Mohamed Said, katika kupitia kwangu maandiko yako mbali mbali mtandaoni na kwingineko nnaona ni kina mama wa Kiislam tu, hata picha hapo juu inadhihirisha hilo, kuwa ndiyo walikuwa mstari wa mbele katika harakati za kisiasa wakati huo, jee hawa kina mama ambao si Waislam walikuwepo katika harakati na wametengwa na kusahauliwa au walikuwa hawajihusishi kabisa na harakati za kisiasa?
Swali hili pia ni kwa Pasco, Nguruvi3, Nanren, Yericko Nyerere (and the likes).
Yan saizi unarudi n I'd ya pili kujisifiaduuh hostoria nzuri kweli kweli hakika Mzee Mohamedi Saidi unatudadavulia watu tusiyoyajua hongera sana Mzee
Nimejaribu sana kujiuliza na kufuatilia hilo suala ila jibu linakuwa haba kulipata. Bahati mbaya sana limeanzishwa katikati ya uzi. Hili jambo linahitaji mjadala mpana ili kuwatambua na pia wenye kufahamu kama wapo kina mama wa dini nyingine ni vipi nao walishiriki katika harakati za ukombozi wa Tanganyika.Alama Mohamed Said, katika kupitia kwangu maandiko yako mbali mbali mtandaoni na kwingineko nnaona ni kina mama wa Kiislam tu, hata picha hapo juu inadhihirisha hilo, kuwa ndiyo walikuwa mstari wa mbele katika harakati za kisiasa wakati huo, jee hawa kina mama ambao si Waislam walikuwepo katika harakati na wametengwa na kusahauliwa au walikuwa hawajihusishi kabisa na harakati za kisiasa?
Swali hili pia ni kwa Pasco, Nguruvi3, Nanren, Yericko Nyerere (and the likes).
Mohamed Said analaumu historia ya Kivukoni kuacha majina ya watu muhimu. Wakati huo huo anafanya kosa lile lile analolaani.Kashata,
Historia hii si ya akina Sykes peke yao.
Unajua katika historia ya uhuru na historia ya asili ya vyama vya siasa
Tanganyika huwezi ukaitafiti na kuandika kwa uhakika bila kuitaja AA.
Huwezi kuitaja African Association bila kumtaja Kleist Sykes.
Huwezi kumataja Kleist bila kuwataja watoto wake kwa kuwa wote
walishiriki katika uongozi wa African Association na kisha kuasisi TANU.
Lakini pia ukiwaleta hawa wanae itakubidi uwalete vijana wenzao wa
wakati wao waliokuwa katika siasa kama Hamza Mwapachu, Dr.
Kyaruzi,Tewa Said Tewa, Zuberi Mtemvu, Dr. Michael Lugazia,
Dossa Azizi, Dr. Wilbard Mwanjisi, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dustan
Omari, Dr. Luciano Tsere, Kasella Bantu kutaja majina machache.
Lakini tena na hili lina nafasi ya peke yake hutoweza kuwafikia wazee
kama Jumbe Tambaza, Mwinjuma Mwinyikambi, Mshume Kiyate,
Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Bi. Tatu
biti Mzee, Bi. Titi Mohamed na wengineo bila kupita kwa Abdul Sykes.
Haya yote ni kwa kuwa kwa wakati ule Tanganyika inaamka katika siasa
za utaifa hawa ndiyo walikuwa katika uongozi wa TAA na walikuwa watu
maarufu katika mji wa Dar es Salaam.
Dar es Salaam ya wakati ule Uislam ulikuwa na nguvu sana mgeni yoyote
asingeweza kufanya lolote bila ya kuungwa mkono na watu hawa.
Ukweli ni kuwa bila Abdul, Nyerere asingepokelewa.
Nitakupa mifano miwili.
Mwaka wa 1933 Kleist aligombana na Erika Fiah katika uongozi wa AA
na Kleist akajiuzulu uongozi na Fiah akachukua nafasi ya Kleist ya katibu.
Rais alikuwa Mzee bin Sudi.
African Association haikuweza kufanya kazi kwa ufanisi na Mzee bin Sudi
ilibidi amwandikia Kleist barua kumsihi arudi katika uongozi.
Barua hii ya mwaka wa 1933 mimi nimeisoma na Mzee bin Sudi ameandika
kwa kuanza na ''Bismillah Rahman Rahim.''
Kleist alirudi katika uongozi.
Mwaka wa 1953 Nyerere alipochukua uongozi wa TAA kutoka kwa Abdul
Sykes chama kilikufa ikabidi juhudi zifanyike kukiweka chama katika hali
madhubuti hadi kufikia kuunda TANU.
Kwa kuhitimisha.
Chuo Cha Kivukoni kilipoandika historia ya TANU haya waliyajua na ndiyo
maana kitabu kizima Abdul Sykes alikwepwa kutajwa na historia ikaanza na
Nyerere kwani walitambua wakimtaja Abdul na kueleza historia yake itabidi
wamtaje na baba yake na wengine wote kama nilivyoeleza.
Hili hawakulitaka.
Mohamed Said analaumu historia ya Kivukoni kuacha majina ya watu muhimu. Wakati huo huo anafanya kosa lile lile analolaani.
Ukisoma habari nzima amelenga kuwataja akina Sykes.
Kaanza Mwaka 1933 chama kilikuwa chini ya Kleist na kaendelea na mgogoro na Erica
Kaanzia mwaka 1933 makusudi kabisa kwasababu huo ndio mwaka aliofaraiki mwanzililishi wa AA Mwalimu msomi Cecil Matola wa wakati huo.
Na alipofanikiwa kukwepa kutaja jina la Matola kwa makusudi akaingiza jina la Abdul kuendeleza chain ya Kleist. Halafu kaunganisha na Uislam katika azma ile ile
Unaweza kuona historia hii inaruka sehemu muhimu sana kwa vile ipo calculated.
Huwezi kzungumzia AA bila kumtaja Mwenyekiti wake Matola.
Hata hivyo historia haimtambui matola kwasababu si miongoni mwa inner circle ya Mohamed anayotaka ing'are, kamtupa pembeni
Anasema hivi 'Huwezi kutaja AA bila Kelist, na huwezi kutaja Kleist bila watoto wake'
Angalia hapa, kwamba Abdul ni muhimu sana kuliko Matola, na unaweza kuitaja AA bila Matola Mwenyekiti lakini huwezi kukwepa Kleist Katibu!
Dini ya Matola inamfanya irrelevant kwa msisitizo 'Waislam walikuwa na nguvu sana' ili kuonyesha kwanini Matola hakuwa na sababu za kutajwa
Kosa la Kigamboni linasahihishwa na kosa jingine la imani!
Wengi hawaoni hesabu zilizopo, hii haina maana kinachosemwa kila kitu ni uongo, la hasha! Isipokuwa matukio yameandikwa kwa kulenga '' familia tukufu'' ili kupitia hapo inatumbukizwa Imani, kujenga chuki na kuleta farki miongoni mwa jamii
MS usichanganye Imani na azma zako. Uislam ni dini inasimama bila usaidizi wa familia tukufu, na wala hauhitaji familia hiyo kuutangaza.
Na Imani iwajenge wananchi isitumike kuwagawa na kuleta dhalili miongoni mwao.
Lakini pia dini zinasema tuwe wakweli wa nafsi zetu na za wenzetu.
Huwezi kuona, sisi tumejadiliana na MS tunamfahamu azma , nia na lengo lake
Nanren kashata
Nguruvi3,Mohamed Said analaumu historia ya Kivukoni kuacha majina ya watu muhimu. Wakati huo huo anafanya kosa lile lile analolaani.

Kwezisho,Nimejaribu sana kujiuliza na kufuatilia hilo suala ila jibu linakuwa haba kulipata. Bahati mbaya sana limeanzishwa katikati ya uzi. Hili jambo linahitaji mjadala mpana ili kuwatambua na pia wenye kufahamu kama wapo kina mama wa dini nyingine ni vipi nao walishiriki katika harakati za ukombozi wa Tanganyika.
Mohamed katika bandiko umewataja wote na hakuna ushahidi waliacha maandiko.Nguruvi3,
Umeitia nafsi yako hofu ya bure.
Nimeanza na 1933 kwa sababu ya tukio lililotokea mwaka ule.
Sina sababu ya kumkwepa Mwalimu Cecil Matola.
Labda nikueleze jambo.
Katika waasisi wote wa African Association ni Kleist peke yake
aliyeandika maisha yake na kuacha hazina kubwa ya nyaraka
ambazo ndizo hizi zinazotujuza mambo mambo ya miaka 100
nyuma.
Labda kama Mwalimu Matola na yeye angeliandika hii leo
hapa tungekuwa tunajua habari zake kama tunavyozijua habari
za Kleist.
Ikiwa unaona mimi nimeruka habari muhimu basi tuandikie na
sisi tutasoma.
Umegusa imani.
Msikilize Kleist anasema nini kuhusu Wakristo katika siasa za wakati
ule.
Kleist katika mswada wake alioandika na ndiyo kutoka mswada huo
mjukuu wake Daisy akaandika: ‘The Townsman: Kleist Sykes’, in
Iliffe (ed) Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, pp. 95-114. anasema
Wakristo walikuwa wachache katika harakati za siasa kwa sababu
walikuwa wakiaswa na kanisa wasijiingize katika siasa.
Hata TANU ilipoundwa ilipata tabu sana kuingia majimbo ya kusini
kwa kuwa hayo ni majimbo ambayo kanisa lilikuwa na nguvu kubwa.
Hii ni histroria na haya yalikuwako hata tukifanyaje hatutoweza kufuta
ukweli huu.
Hapana chuki ipo kubwa na ya dhahiri.Si dhani kama kuna mtu anachuki na nyerere bali ukweli ndiyo unaohitajika,wapo waliopata wazo na mori wa kudai uhuru wakati wapo vitani burma,na wazo walilipata kwa bwana aggrey.tujifunze