Kashata,
Historia hii si ya akina
Sykes peke yao.
Unajua katika historia ya uhuru na historia ya asili ya vyama vya siasa
Tanganyika huwezi ukaitafiti na kuandika kwa uhakika bila kuitaja AA.
Huwezi kuitaja African Association bila kumtaja
Kleist Sykes.
Huwezi kumataja
Kleist bila kuwataja watoto wake kwa kuwa wote
walishiriki katika uongozi wa African Association na kisha kuasisi TANU.
Lakini pia ukiwaleta hawa wanae itakubidi uwalete vijana wenzao wa
wakati wao waliokuwa katika siasa kama
Hamza Mwapachu, Dr.
Kyaruzi,Tewa Said Tewa, Zuberi Mtemvu, Dr. Michael Lugazia,
Dossa Azizi, Dr. Wilbard Mwanjisi, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dustan
Omari, Dr. Luciano Tsere, Kasella Bantu kutaja majina machache.
Lakini tena na hili lina nafasi ya peke yake hutoweza kuwafikia wazee
kama
Jumbe Tambaza, Mwinjuma Mwinyikambi, Mshume Kiyate,
Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Bi. Tatu
biti Mzee, Bi. Titi Mohamed na wengineo bila kupita kwa
Abdul Sykes.
Haya yote ni kwa kuwa kwa wakati ule Tanganyika inaamka katika siasa
za utaifa hawa ndiyo walikuwa katika uongozi wa TAA na walikuwa watu
maarufu katika mji wa Dar es Salaam.
Dar es Salaam ya wakati ule Uislam ulikuwa na nguvu sana mgeni yoyote
asingeweza kufanya lolote bila ya kuungwa mkono na watu hawa.
Ukweli ni kuwa bila
Abdul, Nyerere asingepokelewa.
Nitakupa mifano miwili.
Erika Fiah
Mwaka wa 1933
Kleist aligombana na
Erika Fiah katika uongozi wa AA
na
Kleist akajiuzulu uongozi na
Fiah akachukua nafasi ya
Kleist ya katibu.
Rais alikuwa
Mzee bin Sudi.
African Association haikuweza kufanya kazi kwa ufanisi na
Mzee bin Sudi
ilibidi amwandikia
Kleist barua kumsihi arudi katika uongozi.
Barua hii ya mwaka wa 1933 mimi nimeisoma na
Mzee bin Sudi ameandika
kwa kuanza na ''Bismillah Rahman Rahim.''
Kleist alirudi katika uongozi.
Mwaka wa 1953
Nyerere alipochukua uongozi wa TAA kutoka kwa
Abdul
Sykes chama kilikufa ikabidi juhudi zifanyike kukiweka chama katika hali
madhubuti hadi kufikia kuunda TANU.
Kwa kuhitimisha.
Chuo Cha Kivukoni kilipoandika historia ya TANU haya waliyajua na ndiyo
maana kitabu kizima
Abdul Sykes alikwepwa kutajwa na historia ikaanza na
Nyerere kwani walitambua wakimtaja
Abdul na kueleza historia yake itabidi
wamtaje na baba yake na wengine wote kama nilivyoeleza.
Hili hawakulitaka.