Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Mohamed una ufahamu na ulichoandika? Soma aya za mwanzo halafu za mwisho uone kama zina wiana.

Tulisema kuwa Nyerere ndiye aliandika katiba ya kwanza ya chama cha siasa nchini. Mkasema ilikuwepo ya Abdul Sykes, ndiyo tunauliza.
Mkasema ilikuwa Dodoma imepotea katika mciro film

Sasa mnatulaumu kusema katiba, mnataka twende kwenye document !

Hapana watu wanadai kuona katiba au draft ya Abdul Sykes, kama haipo tubakie na ukweli kuwa hilo ni moja ya transformation alizofanya Nyerere

Halafu utenganishe vitu viwili, katiba ya Tanganyika na katiba ya Chama
 
Moja ya conclusion zake ni kuwa Abdul Sykes ndiye aliyemfundisha Nyerere siasa. Na ili hilo lifanikiwe kuwa kweli, basi ujio wa Nyerere mzobe mzobe kwa kuletwa na Kasela Bantu kutoka Makerere ulikuwa mwaka 1952 akutane na Abdul

Tulijua si kweli kwasababu Nyerere alikuwa katibu wa tawi Tabora
Alihudhuria mkutano mkuu uliokuwa na viongozi wakuu

Kwavile alifanya makusudi ili amhdalilishe Nyerere 'hana umuhimu tena' kama anavyosema akajikuta amesahau na kukiuka kanuni ya uongo i.e usiwe msahaulifu

Ndipo Juma Mwapachu katunong'oneza kwamba aliyemtabulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA kabla ya kuondoka ni Hamza

Mohamed anaruka kimanga anasema, uongozi aliokutana nao ni wa Platan

Haijulikani TAA ngapi zilikuwepo Dar!

You can see he is everywhere, fumbled with lock!
 
Nguruvi3,
Kitabu kimetoka 1998.

Wasomaji wote wameelewa topic ya TAA katika suala la katiba.
Bahati mbaya wewe hujaweza kuelewa.

Hakuna tatizo.
Watu wameumbwa na uwezo tofauti.

Kwako wewe katiba kuandikwa na Nyerere ndiyo suala muhimu.

Wengine katika kitabu changu hakuna kinachowasisimua kama
Part Three: Conspiracy Against Islam.

Hivi sasa nawekwa kwenye shinikizo niandike kitabu kingine
nieleze nini kimetokea baada ya kutoka kitabu.
 
Nguruvi3,
Mimi si muongo.

Nimeiandika historia ya TANU kwa kadri Allah alivyoniwezesha
kiasi hata hao wahusika wenyewe waliokuwa TAA na TANU
wamenipongeza.

Prof. Haroub Othman hakuniita muongo yeye kataka kusikia
upande wa pili wanasemaje.
Je, Juma Mwapachu ni muongo?

Hatuwezi kuwa na situation moja ikawa na majibu mawili tofauti.

Ni ima wewe ni muongo kwa mujibu wa Juma Mwapachu
Au Juma Mwapachu ni Muongo kwa mujibu wa Mohamed Said

Ndiyo maana tunatafuta ukweli, ili tuweze kujua position ya Nyerere mbele ya safari
 
Nguruvi3,
Uongo kwa kusema lipi?
Sikiliza kwa makini dakika 51-53, Mohamed Said anena hakuna aliyewahi kumsikia au kumjua Nyerere TAA kabla ya kujulishwa kwa Abdulwahid Sykes 1952 https://soundcloud.com/mwinyimadi/sheikh-hassan-bin-amir-nur-fm

Juma anasema hivi

''I still recall the visit vividly. I was a standard three pupil then and together with my brother Bakari had to sleep in the sitting room leaving our bedroom to the two guests.

Abdul Sykes was then President of TAA and the TAA leadership plus Dar-based political activists who were predominantly Moslems wanted Abdul Sykes to retain the Presidency.

Abdul was eager to secure Hamza's position on the matter given the fact that it was Hamza who introduced Nyerere to the TAA leadership in Dar back in 1949 before Nyerere left for Edinburgh University''


Mohamed Said

Kaombe radio radhi ili nayo iombe wasikilizaji radhi. Ni uungwana

La sivyo mwambie Juma Mwapachu yeye ndiye mrongo

Kama yote mawili ni magumu, fanya jepesi kabisa liombe jamvi radhi
 
Maalim Mohamed Said please endelea kutusomesha tunakusikia vyema Allah a kuongezea uhai in shaa Allah. Mkuu Nguruvi3 endelea kuwepo jukwaani kwani ni mtu muhimu sana kwa sisi tunao tafuta ilmu
 
Mkuu Nguruvi3 majina na matukio ni vitu vya muhimu sana katika historia. Vinasaidia kutupa mtiliriko mzuri na burdani ya kutosha. Nimesema haya kwa kuwa kuna sehemu umesema majina sio kitu kikubwa. Samahani maana mimi mwanafunzi...
 
Nguruvi3,
Ukweli wangu unakutatiza na kutafiti ukweli mimi nimefanya utafiti
na wewe ni shahidi kwa habari ambazo hakuna aliyekuwa anazijua
mimi nimezileta jamvini.

Sasa na wewe fanya utafiti uje na ukweli wako.
Nakuwekea picha niliyopiga na Juma Mwapachu 1967:


Kulia: Mwandishi wa tatu ni Juma Mwapachu birthday party ya binamu yake
 
Maalim Mohamed Said please endelea kutusomesha tunakusikia vyema Allah a kuongezea uhai in shaa Allah. Mkuu Nguruvi3 endelea kuwepo jukwaani kwani ni mtu muhimu sana kwa sisi tunao tafuta ilmu
Kolorama,
Allahuma Amin.

Nguruvi3 ananisaidia katika kusomesha ni mtu muhimu sana kwetu.
Mengi niliyoeleza ni kwa ajili ya maswali yake.
 
Ngongo,
Uwanja wa huu huru ikiwa na wewe unalo la kueleza ahlan wasaalan
andika tutasoma na ukiwa na picha zibandike tutaziangalia.

Hayo mengine nimeyasoma ni fikra zako na binadamu hatuwezi sote
tukawa na fikra sawa.

Ukubali ukatae wewe unaandika simulizi kwa mlengo wa dini zaidi Kisha unaziita historia ya kweli halafu ukiulizwa au kupewa changamoto unakimbilia kusema "kaandike yako nasi tutasoma" ungekuwa msomi wa kweli usingeweza kujibu majibu ya namna hiyo kamwe!!
 
Mkuu hapa bado hujajibu hoja

Kwa utafiti wako Nyerere alijulishwa kwa Abdul mwaka 1952.
Ukasimama katika redio na kusema Nyerere hakujulikana au kufahamika kabla ya hapo

Juma anasema Nyerere alijulishwa kwa uongozi wa TAA 1949 na Hamza kabla ya kwenda Masomoni

Hatuwezi kuwa na Nyerere mmoja katika nafasi mbili tofauti kwa jambo moja

Kuna uwezekano maneno yako si kweli kwa mujibu wa Juma Mwapchu
Au Juma Mwapachu hakusema ukweli kwa mujibu wako

Tutakuwa tunamdhulum sana Nyerere kama tutaendelea kumhukumu tu kila mmoja na lake. Ifike mahali tujue nini kilitokea tusije ishia kivukoni

Ndio maana nasema, nani muongo baina yenu? Mohamed Said au Juma Mwapachu?
 

Hao wanaosisimuka ni lazima wasisimuke sababu umewaandikia wao na hayo ndo wapendayo kuyasikia "uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa na waislam" hivyo lazima wakupigie makofi na kukushangilia! Ndio, lazima wafanye hivyo ikiwa wao hawajui na wewe mzee wao umewaambia Nyerere amefundishwa siasa na Abdulwahid Sykes mwaka 1952!?! Kwanini wasikushangilie!? Unasema Nyerere si lolote si chochote katika historia ya Tanganyika ila kina Sykes family na Waislam wa Dar es Salaam enzi hizo ndo wenyewe, kwanini wasikupigie makofi!?
 
Mkuu Nguruvi3 majina na matukio ni vitu vya muhimu sana katika historia. Vinasaidia kutupa mtiliriko mzuri na burdani ya kutosha. Nimesema haya kwa kuwa kuna sehemu umesema majina sio kitu kikubwa. Samahani maana mimi mwanafunzi...
Mkuu nilichosema ni kuwa kujua majina si kujua historia.

Ulilonukuu ni kauli ya Mohamed Said wakati anafanya spinning ya maneno yangu na hakika kapata watu.

Spinning nyingine ni ile ya mimi kuomba 'document' hakusema document gani akaweka mazungumzo ambayo , namshukuru mungu ndiyo yaliyotufikisha hapa ambapo hawezi kumeza au kutema maneno yake.

Spinning aliifanya kwasababu niliomba katiba iliyoandikwa na Abdul Sykes kama anavyaoaminisha umma.

Ukitaka kujua huyu mzee ni master wa spinning, kuna mahali kasema eti nimechanganya katiba ya Twinning ya Tanganyika na TAA.

Hakuna mahali niliongelea Tanganyika na katiba.
Nilichosema ni katiba ya TAA ambayo sasa anakiri haipo!

Msomeni kwa umakini Mohamed Said, anajua sana kucheza na akili za watu

Ataulizwa swali utashangaa yanazuka yasiyokuwepo na mapicha n.k.
Hajibu swali moja kwa moja, na hakawii kugeuza kauli za mtu

Anafanya spinning kwa maneno ya watu.
Kwa ufupi he is disingenuous katika discussions.

Ndiyo spinning ambazo leo hawezi kutetea maaandiko na kauli zake redioni

Nani alijua kuna tofauti ya miaka 3 kati ya 1949 na 1952 ambayo ina impact kubwa sana katika historia?

Tupo hapa kusaidia umma
 
Na sasa ukweli upo wazi, Juma Mwapachu kasema si kweli Nyerere alikutana na uongozi wa TAA 1949.

Lengo la redioni ni kumdhalilisha Nyerere na kumfanya Abdul the master.

Si kweli! J.Mwapachu anatueleze jambo ambalo Mohame hawezi kulikanusha.

Hii maana yake ni kuwa ima hakujua hilo, ingawa tulijadiliana mwaka 2010 au anafanya makusudi katika kufikia lengo la kuandika historia ya Familia ya sykes kama historia ya Tanganyika kwa gharama za dhalili kwa Nyerere

Hawezi kusema nani muongo, Mohamed Said au Juma Mwapachu!

Hatuwezi kusahihisha historia ya kivukoni kwa makosa makubwa kama haya
 
Mudeer Mohamed Said,

Ramadhan Mubarak! Nipo safarini lakini napata muda kiduchu nachungulia darsa lako murua!

Endelea kutoa darsa watu wanajifunza mengi kutoka kwako.

Allah akujaze kheri.
 
Achana na story teller. ...
 
Nguruvi3,
Nami nakuwekea majibu yangu hapo chini:
Nguruvi3,
Ama ingekuwa si kwa kuwa naburudika kufanya mjadala na wewe
mie muda mrefu ningelikwisha nyanyua mikono juu lakini nastarehe
kuongea na wewe.

Allah amekupa kipaji cha aina yake.

Majibu nimekupa kuhusu katiba ya TAA Political Subcommittee kuwa
nyaraka na microfilm zote hazionekani Maktaba ya CCM Ddodoma
na TNA.

Sikuishia hapo nimekueleza kuwa kabla yangu katiba hiyo ilitajwa na
Listowel mwaka wa 1965 na Pratt 1976.

Bado unataka nikuletee hiyo document.
Kama wewe hodari sana mbona huwauliza CCM nyaraka hizo zilipo?

Lakini ninastarehe katika mnakasha huu kwa kuwa natoa darsa na
wengi wansoma historia ambapo hawakupatapo kuisikia hata kwa
mbali.

Ndiyo maana narudi hapa tena na tena na tena.
Nakushukuru sana kwa hili.

Sasa nisikikize kwa makini na tuliza ubongo wako nikufunze mbinu
za ''critical analysis'' na kujifunza kusoma katikati ya mistari.

Sitakujibu hayo yote uliyoandika nitakujibu hayo tu ambayo umeweka
rangi nyekundu.

Hamza Mwapachu alimjulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA 1949.

Akili yako mara moja imekwenda kuwa walikuja hadi New Street na
kuzungumza na Mwalimu Thomas Saudtz Plantan aliyekuwa rais na
Clement Mohamed Mtamila aliyekuwa katiibu wa TAA wakati ule.

Lakini ukweli ni kuwa Mwalimu Thomas Plantan na Clement Mtamila
walikuwa hawajapata kukutana na Nyerere hadi alipokuja kwa Abdul
Sykes
1952.

Inawezekana ujulisho huo ulikuwa wa salam za mdomo au wa barua.

Nakuwekea picha nikifanya mahojiano na Bi. Maunda Thoams Plantan
mtangazaji wa kwanza wa kike Tanganyika Sauti ya Dar es Salaam 1952
na mwalimu wa shule.

Mjukuu wa Affande Plantan na mtoto wa Mwalimu Thomas Saudtz
Plantan
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…