Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya


Kwanza ulishutumu Alama Mohamed Said anamtusi Nyerere, tukakuambia nukuu hilo tusi, ukashindwa kunukuu. Ukarudia tena shutuma hizo zaidi ya mara moja, tukakuuliza hayo matusi unayaona wewe tu? Hata Moderator s hawayaoni? Kimya, ukakosa jibu.

Sasa umerukia kuwa eti mimi nnatukana. Tafadhali niambie post namba ipi niliyotukana? Au nukuu hayo matusi yangu kama u mkweli. Hayo matusi yangu uyaone wewe tu moderator asiyaone? Tafadhali msaidie Moderator kwa kubofya "Report Post" ili moderator wanipe adhabu stahiki kwa mujibu wa kanuni za JF.

Ukishindwa yote hayo, unajijuwa u mnafiki kiasi gani.
 
Mudeer Mohamed Said,

Ramadhan Mubarak! Nipo safarini lakini napata muda kiduchu nachungulia darsa lako murua!

Endelea kutoa darsa watu wanajifunza mengi kutoka kwako.

Allah akujaze kheri.
Sharif,
Allahuma Amin.
Maalim Faiza anasema: Elimu bila khiyana.
 
Tangawizi,
Tabu kunipuuza wewe uneshindwa kuachana na mimi umekuja
kunisoma na umeandika.
Kama hukuweza kupata unachotaka miaka 10 iliyopita...sasa hivi sahau kabisa. Endelea na hadithi maana ni sehemu ya maisha ya mwanadamu....wenyewe wanaziita riwaya sababu hakuna ushahidi hata kiduchu. Ni hadithi za kufikirika
 
Uncle...
Ikiwa nitasema kuwa Nyerere si lolote ''credibility,'' yangu itaathrika
vibaya wale waliokuwa wananichukulia mimi kama msomi makini
watanipuuza.

Nimemuonya Nanren kuhusu kuandika mambo ya kuzua.
Nadhani umesoma hiyo post.
 
Kama hukuweza kupata unachotaka miaka 10 iliyopita...sasa hivi sahau kabisa. Endelea na hadithi maana ni sehemu ya maisha ya mwanadamu....wenyewe wanaziita riwaya sababu hakuna ushahidi hata kiduchu. Ni hadithi za kufikirika
Tangawizi,
Sipati wala sitegemei chochote kutoka kwa binadamu.

Allah amenipa zaidi ya nilichotegemea maishani.
Alhamdulilah.

Hakika ni hadithi wala hujakosea.
Hii ndiyo staili yangu ya uandishi na imependwa.

Ama kuhusu ushahidi inategemea msomaji.
Hakuna shida ndugu yangu.

Ikiwa nakukera kwa riwaya zangu unaweza kuacha
kunisoma hutopelekwa polisi.

Nilipokuwa kijana nilimpenda sana mwandishi wa riwaya
Irving Wallace.
 
Nguruvi3,
Mimi siwezi kusema Abdul alimfundisha Nyerere siasa sina ujinga huo.
Tuko hapa kwa kughitilafiana katika uasisi wa TANU.

Baada ya kusoma ile historia ya Kivukoni na kuona jina la Abdul alipo
ndipo nilipoandika kitabu.

Hapana haja ya kusutana katika hili.
Tuje kwa Nyerere kutambulishwa TAA na Hamza Mwapachu.

Uongozi wa TAA nwaka wa 1949 pale New Street Rais alikuwa Mwalimu
Thomas Plantan na katibu Clement Mtamila.

Mimi katika utafiti wangu sijaona popote pale kuwa Nyerere alikutana na
Mwalimu Thomas Plantan au na Clement Mtamila.

Lakini ikiwa yeyote yule anataka kuamini kuwa Mwalimu Thomas Plantan
na Nyerere walikutana mwaka wa 1949 hakuna tatizo.

Ukifanya utafiti haitakuwa tabu kwako kujua historia ya TAA na viongozi wake.
Baada ya kuandika kitabu suala hili hakika kwangu halina umuhimu tena.
 
Mudeer...
Salaam aleykum...

Ulipo Tupooo...

I can see kama kawaida yako...floating like a butterfly and sting like a bee...

Burudaaaani...
Tangawizi,
In deed kaka hamna kitu.
Ni bahati tu hata kujua kuandika.

Mwenyewe ''ambition,'' yangu nilipokuwa nakua
mitaa ta Gerezani nicheze mpira Sunderland
(sasa Simba) kisha timu ya taifa.

Sikufanikiwa.
 
Uncle...
Hakika naandika historia ya Waislam jinsi walivyopigania uhuru
wa Tanganyika.

Angalia anuani ya kitabu hilo liko wazi.
 
Uncle...
Ikiwa nitasema kuwa Nyerere si lolote ''credibility,'' yangu itaathrika
vibaya wale waliokuwa wananichukulia mimi kama msomi makini
watanipuuza.

Nimemuonya Nanren kuhusu kuandika mambo ya kuzua.
Nadhani umesoma hiyo post.


Soma post yako #35 ikiwa ni majibu kwa Kwezisho:

Kwezisho,
Nasikitika kukufahamisha kuwa baada ya mimi kuandika
kitabu cha Abdul Sykes kumeingia ''disinterest'' kwa hii
historia ya Nyerere kwetu sote.

Nyerere amekuwa sasa si muhimu tena baada ya ukweli
kujulikana katika historia ya AA, TAA na TANU.

Na nadhani baada ya Abdul na Ally Sykes kupewa nishani
katika kumbukumbu ya miaka 50 wa uhuru wa Tanganyika
kutambua mchango wao katika kupambana wa ukoloni sasa
hakuna tena jipya.

Imekuwa kama vile katika ''show,'' pazia limeshushwa.
 
Mudeer eeeh...

Watu kama nguruvi3 daima wasikupotezee muda wako...tokea tumeweka nae mnakasha miaka mitatu sasa imepita na alisema atakwenda andika kijitabu chake kuelimisha jamiii...tumesubiri weee hadi hiv sasa chambilecho hata arifu beee teeeh hajaweza kuumba...ni mtu mwenye mfadhaiko wa akili kama yule mwenzake yericko mdandia nasaba ya nyerere....

Wewe tufundishe history sisi...watu kama nguruvi hawawez kuwa na furaha wakiona vyuma kama hiviii...

Haina jjnsiii...hawawez ifuta history hiii...wavumilie tuuh...ndivyo haqi ilivyooo.
 
Ok, kwahiyo hapa tunasema hivi

Nyerere alikutana na viongozi wa TAA mwaka 1949.
Bila kujali ni akina nani, ukweli kuwa alikutana nao umesimama dhahri shahiri.

Juma Mwapachu yupo sahihi kwa maoni yake na kushadidiwa na Mohamed Said
Ushahidi wa maneno ya J.Mwapachu upo katika ukweli kuwa Nyerere alikuwa katibu wa tawi kubwa la siasa nchini -Tabora.

Na alihudhuria mkutano mkuu. Protocol tu ziliruhusu kutajwa

Pili, Nyerere alikutana na Abdul Sykes mwaka 1952 kwa mujibu wa Mohamed Said, Abdul akiwa kiongozi wa TAA

Hili halina maana uwepo wa Sykes unafuta mkutano wa Nyerere na TAA

Kwa mintaarafu hiyo, iwepo katika kumbu kumbu kuwa

1. Kauli ya Mohamed Said akizungumza na Nur haikuwa kweli au sahihi

2. Kwamba, hakuna aliyemsikia au kumjua Nyerere kabla ya Abdul, ni uongo

3. Kwamba, madai ya Mohamed Said yamelenga au yalilenga kupotosha umma

4. Kwamba, makusudi yalitendeka kumdhalilisha Nyerere kwa faida ya A.Sykes

5.Kwamba, madai ya historia ya kivukoni kusahihishwa na hii ya MS yanahitaji fikra na mtazamo mpya (neutral) kwa kutambua makosa ya historia zote

6. Kwamba, Prof Shivj na Prof Saida wawe waangalifu sana wasijeharibu legacy na heshima zao wakiandika historia upya wakaifanyia reference maandiko ya MS.

7. Kwamba, Redio Nur iombe radhi wasikilizaji kwa upotoshaji uliofanywa na mgeni wao Mohamed Said, au yeye awaombe radhi radio Nur

Hivyo basi, kwa pamoja tuseme kuwa; nia, dhamira na mtazamo wa Mohamed kwa Nyerere umejaa chuki. Na kwamba chuki hizo zimepenyezwa katika historia

Redio Nur imetumika kusambaza habari za uongo na uzushi
 
Big Show,
Niko natoa elimu bila khiyana.

Wallahi brother Ritz ndie kanistua...

Nilikuwa napitwaaa na hii ilm ya bure bure...

Naenda zangu salatul insha insha allah nitaunganisha na tarawehe nikirejea naweka kambi hapaaa...

Hao jamaa zetu hata kama hawapendi na inawachoma wavumilie tuuuh...

Ndivyo Haqqi ilivyooo...

Mwaga Nyukii mudeer...
 
Prof Ngongo,

Sikupata kulijua hilo kuwa Cecil Matola, alikuwa Mwanamama shukran kwa darsa!
 
Mimi huwa nakusoma kule kwenye duru za kisiasa kwa kweli hadi nakuonea huruma umekuwa kama mtu ulierukwa na akili hivii...

It has been three years now since you promised to come with your book...

What happened?...

Tulikuambia wewe ni wa humu humu tuh..

Na Utabakia kuwa wa hum hum tuh...

 
Ah mufti ahlan wahsalan, nijalie za mikandani. Ramadhani Karim hapo mikindani, mwatunyima nini! Stareh ya ifta dafu la mikindani sheikh

Naona umekuja na ghadhabu, tuliza moyo, kaa kitako mzee anapata dozi
Mkipiga kelele mnatuchanganya na twaweza ongeza dozi kwa mzee bila sababu

Ndugu yangu hakuna hata siku moja nilisema nitaandika kitabu cha historia
Hayo umeniwekea kinywani 'mpe mbwa jina uweze kumuadhibu'

Pili, Mohamed aendelee na kutoa shule yake, wanaotaka kusikia hadithi waendelee.

Sisi wengine tupo kuweka rekodi sawa ili wasomao kwa ufahamu (comprehension) wasitatizike wala wasijekula mashudu.

Nijaalie
 
Niliahidi lini na kitabu gani? Unaweza kutuletea uzi.

Ni kweli nitabaki humu humu, niliombwa na gazeti fulani nikawaambia mimi ni wa humu humu JF. Lengo ni kuwafikia watu, elimu ni haki yao.

Hata Mohamed kaandika mabuku, kanywa chai na wazungu n.k. bado yupo humu humu

Ah kule duru kumbe unasoma, nakushangaa sasa wewe unasoma habari za mwendawazimu si utakuwa na hali mbaya kuliko yeye!
sheikh inakuwaje hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…