Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya


Haijawahi kutokea babuyo akaweko kwenye hizo picha kwa bahati nzuri? Zitazame vizuri...

Kuhusu bao wala isiwe mwao...
https://upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/4/4d/Nyerere_bao_butiama.jpg

Birds of a feather...
 
Mkuu Mshume Kiyate
Naweka picha ya hawa wazee wanaoitwa wacheza bao na baadhi ya majina yao ambao mi sijawahi kusoma kwenye somo la historia shuleni. Tunachosema hapa tunawekewa sawa kumbukumbu anaebisha atuambie hawa wazee hata mmoja wao katajwa wapi kwenye historia inayofundishwa shuleni
WAZEE WALIOANZISHA VUGUVUGU LA KUSAKA UHURU

Kutoka kulia waliosimama.
1. Abdallah Shomari (Tandamti no. 3)
2. Nassoro kalumbanya (simba str.)
3. Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo str.)
4. Mtoro Ally (Muhonda str.)
5. John Rupia (Misheni kota)
6. Julius Nyerere(Pugu Sekondari) 7. Said Chaurembo (Congo/ Mkunguni str.)
8. Jumbe Tambaza(Upanga)
9. Sheikh Suleiman Takadir (Mafia /Swahili)
10. Dossa Aziz (Mbaruku/Somali kipande)
11. Mshume Kiyate (Tandamti)
12. Juma Sultan (Kitchwele karibu na kanisa dogo )
13. Maalim Shubeti (Masasi/ Likoma)
14. Rajab Simba ( kiungani str.)
15. Waziri Mtonga (Kilosa no.18, Ilala)
16. Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
17. Maxi Mbwana (Aggrey/Kongo)
18. Yosia Omari(Sungwi Kisarawe)
19. Sheikh Issa Nassir ( Bagamoyo)
 
Wanaukumbi.

Mkipata wasaa japo kiduchu msikilizeni Mwalimu Nyerere, akiwaongelea hawa wazee wetu "wacheza bao" kama wanavyoitwa na ndugu zetu hapa barzani.

Ni kapande cha hotuba ya kuaga mwaka 1985 pale Diamond Jubilee, akiongea na Wazee wa Dar es Salaam...

https://m.soundcloud.com/faraj-mohammed-1/nyerere-audio.

Hicho ni kapande kidogo cha hotuba ilikuwa ndefu lakini Abdulwahid Sykes, katajwa na Mwalimu Nyerere, zaidi ya mara tano lakini humu barzani watu hawataki kabisa Abdulwahid Sykes, watu wamtaje daah!!
 
Kwanini mada za mwalimu mohd said watu wa upande flani zinawachoma sana
 
Ritz..Mwalimu Jkn ktk hii hotuba ametamka wazee wazee wazee wa DSM kama mara 10 hivi na anewataja kina sykes mara kadhaa.
Ivi hawa watu wanao sita kuamini kauli na maadishi ya Sheikh Muhamed Said wanataka wapewe ushahidi gani tena wa ukweli na ithibati zaidi ya haya?
Cha ajabu kuna mtu eti na yeye katunga kitabu kujibu vitabu vya Sheikh Muhamed sasa anajibu nini kama Mwalimu Jkn mwenyewe anatamka wazee wazee wa Dsm na kina sykes?
 
Sahimtz,

Ngoja nimnukuu kiduchu Mwalimu Nyerere kwenye hotuba yake.

"Wakanichagua President wa African Association. Tanganyika African Association... Ndipo tukaanza sasa shughuli za kujaribu kuandika katiba mpya ya TAA kusudi tuipe madhumuni ya shahaba ya kuleta uhuru."

"Mwaka uliofuata 1954 ndio tuka, kwa kweli mimi nilidhani tutachukua katiba tu wenzangu wakasema hapana, tukibadili katiba tubadili na jina".

"Tukahaingaika sana kupata jina na hao hao kina Abdul Sykes, jina lile hatukuligundua. Wao walikuwa wamelifikiria zamani wakina Abdul Sykes hao. Walikuwa Burma alikuwa askari na kule waliwahi kufikiria kuanzisha chama..."Kusema kweli wao waliwahi kufikiria kabisa Tanganyika African National Union."Kwa hiyo wakati tunahangaika hangaika pale tuchukuwe jina gani tuchukue Tanganyika African Union wakasema hali itafanana na Kenya African Union. Watadhani nao ni Maumau. Tunataka kuanzisha Maumau yetu. Ndio wakina Abdul Sykes wakakumbuka jina lao walilokuwa wameliunda walipokuwa Burma, wakasema tuite Tanganyika African National Union, ndio tukaanzisha..."

"Wazee wa Dar es Salaam wakaniamini upesi sana, kijana mdogo nikawa na uhusiano mkubwa sana na wazee wa Dar es Salaam. Mkubwa sana, watu wazima, mimi mdogo. Wadogo wenzangu wengine walikuwa ni hao Abdul Sykes kina Abbas Sykes wakina Dossa. Lakini wengine wote walikuwa watu wazima...".

Hii hotuba ilikuwa inaendelea ngoja tufanye juhudi tuipate yote.

Wazee wetu Mwenyezi Mungu hawajaze kheri kwa nia zao nzuri kwa taifa letu.
 
Hawa ndio Muwalimu JKN alio wataja ktk hotuba aliyo weka ustaadh Ritz.
WAZEE WAZEE WAZEE WA DSM.
 
Kuna kimtu kinaitwa Poscali na kijitu kinaitwa Yatco vinathubutu kusema MZEE SHEIKH ULAMAA MUHAMED SAID eti murongo.
Du vijitu vingine sijui vimesoma wapi hata kupambambanua vitu havijui.
Nasijui viko wapi muda mrefu sijaviona sijui vimekimbilia wapi Magu au Maswa?
 
Mohamed Said hatuwezi kwenda mbele kwa kutumia side mirror. Hizi hadithi zako zitatusaidia kama nia yetu kama taifa ni kurudi nyuma na sio kwenda mbele.
 
Mohamed Said hatuwezi kwenda mbele kwa kutumia side mirror. Hizi hekaya zako zitatusaidia endapo kama taifa nia yetu ni kurudi nyuma na si kwenda mbele.
 
Mohamed Said hatuwezi kwenda mbele kwa kutumia side mirror. Hizi hadithi zako zitatusaidia kama nia yetu kama taifa ni kurudi nyuma na sio kwenda mbele.
Unapo hitaji kwenda mbele lazima ungalie UMETOKA WP UPO WAPI UNAKWENDA WAPI.
Na unapo kuwa mtu mkamilifu lazima ujue historia ya familia yako na taifa lako.
Bila kujua haya ukamilifu wako utakuwa na mushkel/mashaka.
Ivi hujui watu wanakaa mashule na vyuoni kwa miaka kusoma haya unayo yaona ww yanaturudisha nyuma?
 
Nadhani huyu Mjomba Said Mahfoudh anaishi keko nyumbani kwake ni karibu na Natonal Hotel zamani Chang'ombe Village.
 
Nadhani huyu Mjomba Said Mahfoudh anaishi keko nyumbani kwake ni karibu na Natonal Hotel zamani Chang'ombe Village.
Swadakat Mkuu Kambaresharubu.
Maalim MS ahsante kwa kutuunganisha na kikubwa tunapata historia halisa ya wazee wetu sasa kama watu wanaumia matumbo sidhani kama hiyo ndiyo nia yetu, nimeelezwa kwamba aliyepakatwa kwenye hiyo picha mkono wa kulia ni Dada Ghania Chaurembo pia kwenye hiyo picha wapo Kaka zetu Idd Chaurembo, Mohamed Chaurembo, Salum Chaurembo,Mzee Dossa Aziz, Mohamed Ngarawa,Shariff Badawi, Mzee Abbas Sykes na mjomba Said Mahfoudh. Kama alivyoeleza Maalim MS hii picha ilipigwa Mtoni kwa Sheikh Chaurembo

Naendelea kupata maelezo na In Shaa Allah kila nitakachopata nitakileta hapa Barzani
 

Sheikh Mohamed Said akhsante Kwa darsa Inshaalah MwenyeeziMungu akuzidishie afya Na kila la kheri Kwa sadaka yako Kwa umma.
Je Saidi Mahfudhi anashughulika Na nini?
Shukran jazeelah
 
Duh Mtebetini Hii dunia ndogo.Angalia darsa inavyo kutanisha watu.
Waswahili husema Mwenyezi Mungu anashani yake, wee ukiwa na yako Mwenyezi Mungu amepanga yake huwezi kupangua mi nimejikuta naunganishwa na watu wala sikutegemea kugongana nao humu kwa ID zetu za kujibanza usijulikane,kasoro Maalim Mohamed Said yeye ni verified user.
Naomba turudi tafadhali kwenye mada tusimuharibie uzi wake na tukamkosea adabu Maalim MS
 
Sheikh Mohamed Said akhsante Kwa darsa Inshaalah MwenyeeziMungu akuzidishie afya Na kila la kheri Kwa sadaka yako Kwa umma.
Je Saidi Mahfudhi anashughulika Na nini?
Shukran jazeelah
Mgogoone,
Amin kwa sote.

Juzi nimemuona Said Mahfoudh kwenye mazishi ya Abdulrahman Lukongo
Sijui anafanya nini kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…