Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #561
Mtebetini,Swadakat Mkuu Kambaresharubu.
Maalim MS ahsante kwa kutuunganisha na kikubwa tunapata historia halisa ya wazee wetu sasa kama watu wanaumia matumbo sidhani kama hiyo ndiyo nia yetu, nimeelezwa kwamba aliyepakatwa kwenye hiyo picha mkono wa kulia ni Dada Ghania Chaurembo pia kwenye hiyo picha wapo Kaka zetu Idd Chaurembo, Mohamed Chaurembo, Salum Chaurembo,Mzee Dossa Aziz, Mohamed Ngarawa,Shariff Badawi, Mzee Abbas Sykes na mjomba Said Mahfoudh. Kama alivyoeleza Maalim MS hii picha ilipigwa Mtoni kwa Sheikh Chaurembo
Naendelea kupata maelezo na In Shaa Allah kila nitakachopata nitakileta hapa Barzani
Hiyo link niliyoweka ina picha ya Nyerere akicheza bao. Nayo huiamini? Kama ambavyo hutaki kuamini kuwa hao wazee walipomkaribisha Nyerere walikuwa tayari hata jina la TANU wameshalitunga zamani.Unajua Wikipedia nini? Naweza ku upload taarifa wewe na ritz ni mtu na mumewe ikawa validated.
...Manzese,Mohamed Said hatuwezi kwenda mbele kwa kutumia side mirror. Hizi hekaya zako zitatusaidia endapo kama taifa nia yetu ni kurudi nyuma na si kwenda mbele.
Sahimtz,Kuna kimtu kinaitwa Poscali na kijitu kinaitwa Yatco vinathubutu kusema MZEE SHEIKH ULAMAA MUHAMED SAID eti murongo.
Du vijitu vingine sijui vimesoma wapi hata kupambambanua vitu havijui.
Nasijui viko wapi muda mrefu sijaviona sijui vimekimbilia wapi Magu au Maswa?
Mkuu Ritz shukran jazirah ukipata yote tuwekee tupate kusikia kutoka kwa kiywa cha mwalim labda wenzetu wataelewa.Sahimtz,
Ngoja nimnukuu kiduchu Mwalimu Nyerere kwenye hotuba yake.
"Wakanichagua President wa African Association. Tanganyika African Association... Ndipo tukaanza sasa shughuli za kujaribu kuandika katiba mpya ya TAA kusudi tuipe madhumuni ya shahaba ya kuleta uhuru."
"Mwaka uliofuata 1954 ndio tuka, kwa kweli mimi nilidhani tutachukua katiba tu wenzangu wakasema hapana, tukibadili katiba tubadili na jina".
"Tukahaingaika sana kupata jina na hao hao kina Abdul Sykes, jina lile hatukuligundua. Wao walikuwa wamelifikiria zamani wakina Abdul Sykes hao. Walikuwa Burma alikuwa askari na kule waliwahi kufikiria kuanzisha chama..."Kusema kweli wao waliwahi kufikiria kabisa Tanganyika African National Union."Kwa hiyo wakati tunahangaika hangaika pale tuchukuwe jina gani tuchukue Tanganyika African Union wakasema hali itafanana na Kenya African Union. Watadhani nao ni Maumau. Tunataka kuanzisha Maumau yetu. Ndio wakina Abdul Sykes wakakumbuka jina lao walilokuwa wameliunda walipokuwa Burma, wakasema tuite Tanganyika African National Union, ndio tukaanzisha..."
"Wazee wa Dar es Salaam wakaniamini upesi sana, kijana mdogo nikawa na uhusiano mkubwa sana na wazee wa Dar es Salaam. Mkubwa sana, watu wazima, mimi mdogo. Wadogo wenzangu wengine walikuwa ni hao Abdul Sykes kina Abbas Sykes wakina Dossa. Lakini wengine wote walikuwa watu wazima...".
Hii hotuba ilikuwa inaendelea ngoja tufanye juhudi tuipate yote.
Wazee wetu Mwenyezi Mungu hawajaze kheri kwa nia zao nzuri kwa taifa letu.
Mgogoone,
Amin kwa sote.
Juzi nimemuona Said Mahfoudh kwenye mazishi ya Abdulrahman Lukongo
Sijui anafanya nini kwa sasa.
Mgogoone,Sheikh Mohamed Said Asante Kwa majibu Na darsa nzuri.
Bakar..,Dah hii story is so amazing yan.. Ila mbona zimefichwa jaman.?
Onyx,Duh nazidi kuchanganyikiwa. Minadhani tumuulize na Kaunda, si bado yupo. Kwa hiyo pale Lumumba ni kwa Sykes
mkuu Ritz kwa hotuba hii wale waliokuwa wanabisha kuwa jina la TANU sio wazo la Mwalimu ila jina hilo wazee wetu walikuwa nalo kabla mwalimu hajajiunga TAA watakuwa wameshapata majibu kongole Mzee MS hakika wewe ni kisima cha historia yetu japokuwa kuna wengine wachache hawataki kuukubali ukweliWanaukumbi.
Mkipata wasaa japo kiduchu msikilizeni Mwalimu Nyerere, akiwaongelea hawa wazee wetu "wacheza bao" kama wanavyoitwa na ndugu zetu hapa barzani.
Ni kapande cha hotuba ya kuanga mwaka 1985 pale Diamond Jubilee, akiongea na Wazee wa Dar es Salaam...
https://m.soundcloud.com/faraj-mohammed-1/nyerere-audio.
Hicho ni kapande kidogo cha hotuba ilikuwa ndefu lakini Abdulwahid Sykes, katajwa na Mwalimu Nyerere, zaidi ya mara tano lakini humu barzani watu hawataki kabisa Abdulwahid Sykes, watu wamtaje daah!!
Wa Ukae,mkuu Ritz kwa hotuba hii wale waliokuwa wanabisha kuwa jina la TANU sio wazo la Mwalimu ila jina hilo wazee wetu walikuwa nalo kabla mwalimu hajajiunga TAA watakuwa wameshapata majibu kongole Mzee MS hakika wewe ni kisima cha historia yetu japokuwa kuna wengine wachache hawataki kuukubali ukweli
Mtebetini,Maalim Mohamed Said Salaam Aleykum
Nimekuwa nikikisikiliza kipande cha hotuba ya Mwalimu Nyerere ambayo hakukamilika aliyoileta
Al-alama Ritz na katika pita pita yangu humu kwenye Jamvi nikakuta uzi ambao umeandikwa na jamaa yetu, naomba niweke huo uzi hapa muone
sifa
Mwalimu Nyerere alifanya kosa kujiunga na TAA, angebaki na TAWA yake itupe UHURU
Maalim naona katika maelezo ya wachangiaji wa huo uzi wa hapo juu kulitolewa ombi la kuileta hii hotuba ya maneno badala ya maandiko,mi nauliza mleta bandiko alileta hii hotuba ya maneno Barzani? kama hakuleta naomba aombwe ailete maana ameiandika kwa urefu, badala ya Al-alama Ritz kuhangaika kuitafuta.
Akhui Mtebetini,Maalim Mohamed Said Salaam Aleykum
Nimekuwa nikikisikiliza kipande cha hotuba ya Mwalimu Nyerere ambayo hakukamilika aliyoileta
Al-alama Ritz na katika pita pita yangu humu kwenye Jamvi nikakuta uzi ambao umeandikwa na jamaa yetu, naomba niweke huo uzi hapa muone
Mwalimu Nyerere alifanya kosa kujiunga na TAA, angebaki na TAWA yake itupe UHURU
Maalim naona katika maelezo ya wachangiaji wa huo uzi wa hapo juu kulitolewa ombi la kuileta hii hotuba ya maneno badala ya maandiko,mi nauliza mleta bandiko alileta hii hotuba ya maneno Barzani? kama hakuleta naomba aombwe ailete maana ameiandika kwa urefu, badala ya Al-alama Ritz kuhangaika kuitafuta.
Maalim Mohamed Said
Nimekusoma na uliyonieleza ni dhahir shahir mleta ule uzi anabandika/anabadilisha taarifa za vyanzo vyake vya habari. Nimeleta uzi huo hapa Barzani ili kuweka kumbukumbu sawa kwani kwenye uzi huo mleta uzi aliombwa kuleta Audio mimi nakumbusha alete tuisikie,Audio iliyoletwa na Al-alam Ritz ni kipande kidogo nikilinganisha na maelezo aliyoandika mleta huo uzi.
Ritz,Akhui Mtebetini,
Ukipata wasaa pitia hapa chini kwenye huu uzi vyombo vimo humo huyu mleta mada alikimbia mwenyewe pamoja na wenzake uzi ulikua hatari.
Uchochezi wa Mohamedi Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar