kumbe zamani mtu ukiwa na certificate unaweza kufanya masters? zamani maisha yalikuwa mtemremko.His intelligence was quickly recognized by the Roman Catholic fathers who taught him. He went on, with their help, to train as a teacher at Makerere University in Kampala (Uganda). On gaining his Certificate, he taught for three years and then went on a government scholarship to study history and political economy for his Master of Arts at the University of Edinburgh
Huwa nnawasiwasi mkubwa na huyo kijana ajiitae Yericko Nyerere, wasiwasi wangu ni kuwa ana maradhi ya nafsi, ambayo ni mabaya kuliko maradhi ya akili.
Inaitwa bellow the belt ndio ukweli wenyewe kijana mwenzetu Yericko Nyerere ana maradhi ya nafsi.Huwa nnawasiwasi mkubwa na huyo kijana ajiitae Yericko Nyerere, wasiwasi wangu ni kuwa ana maradhi ya nafsi, ambayo ni mabaya kuliko maradhi ya akili.
KedrickMmmh kuna harufu ya udini humu [emoji124]
Leymooh,Ukisoma kitabu kimoja "Uislam na Uhuru wa Tanganyika" utapata jibu
Ww ndio unataka kuleta udini maana binafsi hta sijui udini unatoka wapi hapaKedrick
Hebu rudi utuambie siku hizi herufi zinatoa harufu!
Mudeer Mohamed Said,Onyx,
Nakushauri usome kitabu cha Ali Muhsin, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,''
yote yamo ndani.
Mohamed Shamte serikali yake ilipinduliwa na akafungwa Bara.
Nakuwekea picha hapo chini nikifanya mahojiano ya televisheni na
mtoto wa Sheikh Mohamed Shamte, Baraka Shamte kada mkubwa
wa CCM Zanzibar.
Baraka alinieleza mengi kuhusu baba yake wakati akiwa kifungoni hadi
kufikia umauti wake akiwa uhamishoni Arabuni:
Shariff,
Mudeer Mohamed Said,Shariff,
Umekinunua wapi na kiasi gani?
Jana kanipigia mmoja katika mabalozi wetu wa muda mrefu sasa
mstaafu kuniuliza habari za Ali Muhsin.
Kakisoma kitabu kwa siku tatu kakimaliza na kasema kaelimika sana.

Nkuba25,Salaam Mzee Mohamed Saidi.
Kwanza kabla ya yote ningependa kumshukuru Mungu kwa kukuweka hai mpaka sasa, kukupa moyo na hali ya kufuatilia haya mambo ya ki historia na mwisho namshukuru Mungu kwa kukupa uvumilivu na subira unapokuwa kwenye mijadala ambayo inahusisha watu mbalimbali na wenye mitazamo tofauti.
Mwanzoni niseme kweli kabisa hata Mimi binafsi nilikuona na nilidhani u mmoja wao wanaofanya harakati za kiislam. na maanisha yale Mambo ya "mfumo kristo"
Lakini nimefuatilia sana sana mijadala yako na hoja zako, niseme ukweli kabisa kutoka moyoni, umejitahidi sana sana kuweka pembeni Mambo ya dini na harakati za ukombozi wa Tanganyika. Kusema ukweli sijaona ukisema paala kuwa "waislaam ndio wametafuta uhuru". Kwa hilo naomba nikupongeze.
Ni ukweli usiopingika kuwa hizi harakati za uhuru zilifanywa na wazee wetu "saa zingine tunapenda kuwaita waswahili" hili halina ubishi na hata mtu akitazama vizuri, wazee wengi wa ccm ni hawa hawa wazee wetu waswahili.
Sasa kinacholeta mgongano au kinachotokea hapa ni kwamba hawa wazee wetu wengi wao ni waislaam na hilo halina ubishi, sasa wewe Mzee Said unaposema hawa wazee wetu ambao ni waislaam wao ndio walikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru, hilo jambo watu hawataki kulisikia, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hawa wazee ndio wamepigania uhuru.
Watu humu wakielezwa ukweli kuwa hawa wazee wetu wa kariakoo/magomeni etc ndio wametafuta uhuru hawataki kusikia kwa sababu tu ni wazee wa ki islaam huo ndio ukweli.
Pia nakushukuru sana kwa namna unavyojenga hoja zako with evidences. Kwa mfano unasema nilikuwa Chuoni Iowa nikitoa Seminar na kweli unaweka evidence. Hilo ni jambo zuri sana. Sasa pamoja na hayo ma evidence yote lakini bado mtu ana kubishia? Elewa hapo kuwa unayefanya naye mdahalo ana matatizo makubwa sana. Pia watu yatupasa kuwa ni watu wa kujifunza kuliko kuwa wabishi wabishi tu.
Mimi ni Roman Catholic, lakini kwa vile wazee wa ki Islam ndio walipigania uhuru hilo halinifanyi nione ni uhongo ama kuwachukia. Kama ndiyo hivyo basi na iwe hivyo, historia ni historia tu, you cannot alter it.
Na kuanzia Leo nakuahidi nitakuwa positive kuhusu wewe na nakuahidi nitatafute vitabu vyako nianze kuvisoma. Kwa maana vinafundisha Mambo ambayo sikuwahi kuyajua kabisa Maishani, mpaka nilipoanza kukufuatia humu JF.
Rehema na Baraka za Mungu ziwe Juu yako wewe na Mungu akupe maisha marefu sana mzee wangu.
Nkuba25.Salaam Mzee Mohamed Saidi.

Carlos...Nkuba25.
Nakubaliana na wewe sehemu kubwa ya bandiko lako lakini napinga na wewe hapo kwenye wazee wengi wa CCM ni waswahili.
Mzee Mohamed, atanisahisha wazee wa TANU wale waasisi wengi wao wamefariki hata CCM haijazaliwa na wengine baada ya uhuru na kutofautiana na Nyerere waliachana kabisa na siasa mpaka wametangulia mbele ya haki.
Hii CCM ina wazee karibia mikoa yote ya Tanzania hawa wazee wachache unaowaona CCM hawa hamna hata mmoja alikuwemo kwenye harakati za TANU.
CCM ilibakia na Nyerere na wenzake, baada ya uhuru watu wote waliyokuwa wanatawaliwa walingia CCM baada ya kugeuzwa jina kutoka TANU kulikuwa hamna chama chochote cha siasa baada Nyerere kupiga marufuku vyama vya siasa.
Asante sana mkuu kwa kunisahihisha.Nkuba25.

Salaam Mzee wangu Mohamed SaidUncle...
Inawezekana ukaona kosa kuandika historia ya Waislam wa Tanganyika.
Ndiyo ubinadamu ulivyo, ''one man's meat is another man's poison.''
Mimi kwangu si kosa na ndiyo maana nikakujibu kuwa soma anuani ya
kitabu changu.
Inawezekana wewe hujui lakini kuna vitabu vingi tu vilivyoandika historia
na mengi ya Waislam wa Tanganyika.
Katika vitabu maarufu ni hiki cha Augustus Nimitz: Islam and Politics in
East Africa.
Kipo pia kitabu cha P van Bergen: Religion and Development in Tanzania.
Kipo kitabu kinachoeleza habari za Kanisa Katoliki cha John Sivalon: Kanisa
Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985.
Hapana ubaya kuandika historia kama niliyoandika mimi kwani ni jambo la
kawaida katika usomi.
Asikutishe mtu.
Hayo mengine sitoyagusa kwa kuwa unaandika kitu usichokijua.
Muulize Dr. Mkanachi kuhusu historia hii.
Wakati alipokuwa anaandika tasnifu yake alikuja kujadiliana na mimi.
Mengine itapendeza yatoke kinywani kwake.
Salaam Mzee MohamedWanamajlis,
Naomba mtazame hii video hapo chini kipindi nilichofanya na Azam TV
Nyerere Day 2015:
<iframe width="560" height="315" src="" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>
Nkuba25,Salaam Mzee Mohamed
Sasa hivi nipo naangalia video ya mahojiano yako kuhusu historia ya mzee Abdul Sykes
Lakini niseme jambo moja tu, Serikali imefanya makosa mkubwa sana, iwe kwa makusudi au kwa Bahati mbaya kuachia hizi nyumba ambazo wazee wetu walikuwa wanakutana kwa ajili ya harakati zao za kisiasa zibomolewe na pasiwepo alama yoyote ya kumbukumbu.
Hizi nyumba zilitakiwa kuwa makumbusho mahususi sana. Hili ni kosa kubwa kubwa sana kuwahi kufanyika katika nchi yetu. National Museum wangezichukua na kuzifanya sehemu ya utalii na kujifunza.
Yaani nipo hapa naangalia wazee wetu walikotokea, hizi nyumba zingetunzwa pamoja na hizo picha mbalimbali za wakati huo, hakika ingekuwa jambo zuri sana.
Kusema kweli imeniuma sana sana kwa serikali kushindwa kutunza hizi kumbukumbu.
Mzee Wangu Mohamed Said asalaam alaykum. Nimekuwa kimya kwa muda ila uzi haujanipita. Nakushukuru nimepata vitabu kwenye duka la ibn hamza. Hakika haya ni madini kama wasemavyo watoto wa mjini. Mungu akupe uhai mrefu uzidi kutupa ilm sisi vijana wako na wengine wengi ambao wanasoma kimyakimyaNkuba25,
Si kama hayo yalifanywa kwa bahati mbaya.
Kuna watu hawakuitaka historia hii.
Historia hii ilikuwa inawatisha sana na ndiyo
kisa cha kuja na historia ya Kuvukoni College.