Hananja: Changamoto za Jamii zitatuliwa kwa mazungumzo na maridhiano badala ya migogoro

Hananja: Changamoto za Jamii zitatuliwa kwa mazungumzo na maridhiano badala ya migogoro

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mchungaji Richard Hananja amesema changamoto zinazojitokeza katika jamii zinapaswa kutatuliwa kwa mazungumzo na maridhiano badala ya migogoro. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Juni 18, 2026, amesema historia inaonesha kuwa hata uhuru wa Tanzania ulipatikana kupitia mazungumzo.

Hananja amesisitiza kuwa amani ni tunu muhimu inayopaswa kulindwa na kila Mtanzania, akionya kuwa kuvunjika kwake huwaathiri zaidi watoto na wazee. Aidha, ametoa wito wa kutafuta suluhu za tofauti kwa ustaarabu huku akieleza kuwa kujenga amani ni kazi ngumu lakini kuiharibu ni jambo la muda mfupi.

 
Mchungaji Hananja yuko sahihi. Ni mchungaji mwenye akili mingi.
 
Alisema anawalea na anakaaga na wala ngada. Pia aliwahi kupigana ngumi. Ni mtu mzuri wa kumzingatia sana.
 
Back
Top Bottom