peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Walimu wanaofundisha Shule ya Msingi Gole iliyopo Kata ya Kang’ata wilayani Handeni mkoani Tanga, wameiomba Serikali kuwasaidia ujenzi wa vyoo vya walimu kwa kuwa wanajisaidia na kuoga kwenye vichaka kwa kukosa vyoo bora.
Wakizungumza shuleni hapo juzi walisema kuna muda inabidi waingie kujisaidia kwenye vyoo vya wanafunzi kwa sababu choo wanachotumia kwa majira ya mchana hawawezi kuingia kwani hakina mlango rahisi mtu akipita kumuona aliye ndani.
Mwalimu Mkuu swa shule hiyo, Said Mbelwa alisema licha ya ukosefu wa bafu na vyoo vya walimu, pia kuna walimu wanne wanaoishi kwenye nyumba moja jambo linalowanyima faragha na familia zao.
Mwalimu Jackson Mwakalukwa alisema athari nyingine ambayo ipo kutokana na adha hiyo ni kukosa mwalimu wa kike kwenye shule yao,hivyo imekuwa ni changamoto kwa wanafunzi wa kike kukosa mtu wa kumueleza matatizo yao hasa yanayohusu nasuala ya kike.
Naye Ofisa Elimu Msingi wilayani hapo, Goodluck Mwampashe alikiri kuwepo changamoto ya vyoo vya walimu kwenye shule hiyo na kueleza kuwa mpango wa kujenga upo ila kwa kutumia mfuko wa wafadhili.
Akiwa katika kijiji hicho, kwenye mkutano wa hadhara Mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel Mchembe, aliendesha harambee kijijini hapo ili kupata vifaa vya kuanzia ujenzi.