'Hangover' ya propaganda za utawala wa Magufuli zitadumu kwa baadhi ya watu milele

Hizlo zote unazoongea zilikuwa uongo was Magufuli alifanya maigizo ili wajinga wamsifu eti amegundua wizi bandarini , kweli wajinga ndo waliwao
 
Alikuwa mshamba sana au pengine mweupo kwenye nadharia na falsafa za maendeleo. Alifikiri maendeleo ni majengo, barabara, madaraja na vitu vingine vinavyoonekana; yaani maendeleo ya vitu. Upeo wake kiuongozi ulikuwa mdogo sana, hakustahili kuwa kiongozi wa nchi hii; ndiyo maana hatimaye ilibidi kutokea yaliyotokea.
 
Mimi ningependekeza itungwe sheria kali ya kuhakiki mali za viongozi wakuu wa serikali wanapoingia, na wanapotoka uongozini. Kuwe na mfumo ambao ni fool proof, na wale watakaobainika kuiba mali ya umma wapate adhabu kali hata kifungo miaka mingi gerezani.
Leo mkuu wa nchi anatamka kuna pesa za umma ziliibwa na kuhifadhiwa China, lakini si ajabu suala hili litapotezewa hivi hivi. Ni aibu kwetu kama taifa.
 
Hivi haiwezekani rais Samia alazimishwe kuweka hadharani taarifa ya ule ukaguzi alioagiza ufanywe b.o.t wa transactions za January to march 2021
 
Tangu afariki sijawahi kusikia mtu katekwa, kauawa au maiti imeokotwa ikiwa ndani ya kiroba.
 
Tangu afariki sijawahi kusikia mtu katekwa, kauawa au maiti imeokotwa ikiwa ndani ya kiroba.
Kwahiyo una maana ya kwamba uhalifu wa watu kutekwa umekuja kipindi chake tu kwamba huko nyuma hakukuwa na uhalifu wa watu kutekwa Tanzania? Kwamba Tanzania hakuna uhalifu wa watu kuuliwa?

Kama ni hivyo basi Tanzania ilihitaji kupongezwa maana ni jambo kubwa kuweza kudhibiti uhalifu wa aina hiyo kwa 100%.
 
Ukiona mtu anavunja Katiba iliyomweka madarakani,huyo siyo kiongozi bali ni mtawala,JPM aliishi kiutawala zaidi na uongo ili kuwapumbaza wasio na mawazo ya mbali katika kufikiri kwa vile eneo analotokea wajinga ni wengi sana.
 
Yah. Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa tukio lile la march '21.
 
Ndio maana tunataka hao jamaa zake ambao wapo hai wapelekwe Mahakamani na pesa zirejeshwe maana tumeshajulishwa zimewekwa huko China. ! Bila kufanya hivyo hizi zote ni porojo kama za Abunuwas !! Watanzania sio mazuzu wa kudanganywa danganywa kama ulivyoeleza !! Watanzania wana akili timamu na wanajua mchele upi na pumba ni zipi !!
 
Yah. Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa tukio lile la march '21.
Mwaka 2022 hadi huu 2023 kumekuwa na matukio ya ajabu ajabu watu wanauwana kikatili,kumekuwa na unyanyasadi na mabalaa mbalimbali mwanzo kabisa tulianza na panya road hali iliyotishia usalama wa watu na mali zao.

Hayo mabalaa na mitihani yote imetokea kipindi ambacho Magufuli ameshafariki hayupo.
 
Pumzika kwa Amani Kipenzi chetu! Mungu akusamehe makosa yako, na familia yako ipone kwa maumivu kama haya yanayosambaa kwa kasi Nchini.
 
Vile mwendakuzimu amefurahia uzi wako huu kutokea huko kuzimu😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…