'Hangover' ya propaganda za utawala wa Magufuli zitadumu kwa baadhi ya watu milele

'Hangover' ya propaganda za utawala wa Magufuli zitadumu kwa baadhi ya watu milele

JMP ameondoa shida gani kwa Wananchi? Magufuli ameondoka watu hawana fedha, deni la ndani limekuwa zaidi kwa kuchukua fedha za watu na kuwekeza katika miradi mikubwa ambayo haina faida ya moja kwa moja kwa watu.

Ndani ya miaka mitano amekopa over 10 trillion, wewe huogopi? Ndege, SGR, Mwendokasi na miradi yote mikubwa amekopa nje bila approval ya Bunge. Kupeleka mji Mkuu Dodoma ni mpango wake wa kutoa zabuni kwa makampuni ya ujenzi ya Kichina ili apate 10%, acheni upuuzi huyu jamaa was filthy thief.
Mama ndani ya mwaka mmoja amekopa ngapi?
 
Kwan bunge la Sasa lina afhadhal gan
Bunge hili linatokana na uchaguzi uliivurugwa na Magufuli Oktoba 2020. Magufuli aliweka wabunge wake ambao wangekuja kubadili Katiba atawale milele. Ila Mungu akafanya yake Machi 2021
 
Niteseke kwani mimi ndio mwenye hasira na maiti au ninyi ndio wenye hasira na maiti ndio maana kila siku mnafungua nyuzi kumzungumzia kuonesha hasira zenu?

Mimi nachokifanya ni kuonesha jinsi chuki zenu zilivyowaathiri kiasi kwamba akija mtu na kuwaambia chochote kibaya kuhusu Magu mnakikubali tu kisa kinamzungumzia vibaya Magu bila kujari hata kama kuna contradiction.

Huyo huyo Magufuli mlisema alichanja chanjo ya corona ya wachina kisiri siri na huyo huyo Magufuli alipokufa nyie nyie tena mnasema amekufa kwa corona kwa sababu hakuchanja alidharau corona.
Yote hayo ni chuki tu, sasa mimi nikieleza hayo ndio unaona namtetea Magufuli?
Wahi Chato kachimbe Kaburi uzikwe karibu yake
 
Man himself, he live beyond the grave. Mtu uliye hai unahangaikaje na maiti wakati una mambo mengi ya kufanya ku prove wrong . Udhaifu wa fikra zako au uvivu tu wa kufikiri kila siku kuandika mara hivi mara vile, his ideology will stand regardless of his weaknesses . He has done his duty do yours. Huwezi badili chochote kilichotokea . Kila utawala una siasa zake na maumivu yake pia issue ni kuangali maumivu mnaya chagua . Lakini hakuna uhuru wa kiuchumi unao kuja direct bila maumivu na sucrifices. The bad thing is to be poritically right in world system we are in.
Kwahiyo wanaohangaika na kifo cha yesu tuwaitaje? Na wale wa mauaji ya kimbari je??
 
Aliajiri bana acha uongo. Na madaraja alipandisha. Na PAYE alishusha.

Acha propaganda uchwara. Hata internet inasema aliajiri.


Lambda useme si kwa kiwango Cha kutosha.


Matatizo ya Umeme yalipungua Sana. Na maji yalikuwa hayakatiki ovyoovyo.

Maendeleo yalikuwa kwa kasi mno.
Fuatilia ilikuaje umeme ukatosha? Ulitosha hadi viwandani?.

Anyways, Sina tatizo na JPM kwa sababu kuna mambo alifanya kwa vitendo yenye manufaa halafu yupo kwenye nyumba yake ya milele, asifiwe au apondwe hana direct impact kwenye TZ ya sasa. Maamuzi ya hii nchi ni juu ya walio hai.
 
Ingia basi hata ajira portal uangalia?

Sasa kila kitu ukitaka tukuwekee hapa huoni tutakuwa tunarudia mambo? Unamiliki technolojia unashindwa kuji update?

Alizindua viwanda hadi mkalalamika, sijui hizi propaganda mnazipika za Nini! Tanzania ya Viwanda mmepotezea Sasa hivi kazi ni kulamba Asali tu. Kamba zimeshakatika kwa hiyo ni mwendo wa kula kokote tu.
Viwanda vilivyojengwa 2015 to 2025 muwekee hapa kabisa avione.😀
 
No doubt Magufuli alimaster sana the art of propaganda. Alizishika media zote, hadi za nje kuna wakati ikatangazwa kwamba hazipaswi kurusha maudhui ya ndani bila kibali.

Media zote nchi, binafsi na zile za serikali hadi zile ambazo ziko tu online ambazo hazina usajili wa serikali zilijaa woga kumtaja Magufuli katika namna ambayo isingempendeza. Media nchini ziliimba mapambio ya kumsifu na kumtukuza mawizo mpaka machweo.

Propaganda za Magufuli zinanikumbusha propaganda za Adolf Hilter, Joseph Stalin na Mao Ze Dong. Hawa watu walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuaminisha mambo ambayo hayapo, walikuwa na uwezo wa kupandikiza nadharia zao na imani zao juu ya kadamnasi na ikaamini vivyo, huku nyuma ya pazia wakiwa na mauzauza yao kibao.

Magufuli alitupiga wapi? Kwanza alijifanya Rais wa wanyonge, akijua kwamba watanzania wengi over 40% tuko chini ya mstari wa umasikini wa $1 kwa siku, masikini wengi tulimpenda sana tukidhani ni mwenzetu lakini katu, hakuwa mwenzetu, JPM alikuwa tajiri sana.

Magufuli alijua kwamba watanzania hatupendi mafisadi, wengi tunadhani umasikini wetu kuna watu wanatuibia serikalini. JPM akaona atangaze nao vita kali, tukamsahau yeye ambaye alijilimbikizia mali nyingi sana, huku tukijua kwamba anapambana na mafisadi kwa ajili yetu, kumbe ni kwa ajili yake kwani kila alipotaifisha mali zao, zikawa zake na jamaa zake.

JPM master the art of public manipulation. Kwenye ziara zake alisimama barabarani, alizungumza na watu, akatoa fedha hadharani kwa watu wa hali ya chini, alitembelea hospitali na kutoa misaada hadharani kwa watu waliokuwa na hali ngumu huku kila media ikimulika. Vitendo vile vimewalevya wengi kudhani kwamba JPM was saviour, tukasahau kabisa na yeye ni mwanadamu mwenye tamaa na uchu, aliweza kufanya chochote pasi nasi kujua kuwa mali zetu zinaibwa na kuwekezwa kwenye hotels zake, real estate, mashamba na kuficha fedha nje ya nchi. Mtoto wa dada yake, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya fedha Dotto James alifanya kazi kubwa sana kusafirisha fedha za mjomba wake nje.

Naona leo wakimkumbuka sana. Nasikitika sana kuona wengi wakimkumbuka JPM pasi na wao kujua kwamba bado wamo kwenye dimbwi la mning'inio wa propaganda za JMP. Ila kama tungejua uozo na madudu aliyofanya nyuma ya pazi, pengine tungezinduka kutoka kwenye hangover hiyo. Tuishie hapo.
Kwahiyo ulitaka tuwakumbuke mafisadi na wahuni wakina msoga na chifu mafiii
 
Hii paragraph ya 5 ndio imefanya niwe na shaka KUBWA na Wewe kusema tunadhani SERKALI NA MAFISADI wanatuibia? Aisee kwahiyo ESCROW kwako ni halali, MELEMETA ni Safi kwako, upigaji bandari hadi gauge ya kupima mafuta kuchezewa ni SAWA kabisa, .
Wewe ni nani?
Huyo ni jamaa wa ROSTAM AZIZI KWA WALE MSIOMJUA ...
 
Back
Top Bottom