'Hangover' ya propaganda za utawala wa Magufuli zitadumu kwa baadhi ya watu milele

'Hangover' ya propaganda za utawala wa Magufuli zitadumu kwa baadhi ya watu milele

Umeme Tanzania hautoshi na umeme mwingi unatumika katika viwanda. JPM, alitoa amri kwenye viwanda vipunguze uzalishaji na kufanya kazi mchana tu na kuachia matumizi ya umeme uende kwa Wananchi. Viwanda vilifungwa, watu wakakosa ajira na wawekezaji wakaondoka. Huyu ndiye JPM.

Kama ulifurahia umeme kutokatika, uje tu kuna viwanda vilifungwa na maelfu ya vijana wakapoteza ajira. Magufuli ameajiri watu gani? Amewalipa kitu gani kama kwa miaka mitano hajaongeza mshahara wala madaraja?
Ingia basi hata ajira portal uangalia?

Sasa kila kitu ukitaka tukuwekee hapa huoni tutakuwa tunarudia mambo? Unamiliki technolojia unashindwa kuji update?

Alizindua viwanda hadi mkalalamika, sijui hizi propaganda mnazipika za Nini! Tanzania ya Viwanda mmepotezea Sasa hivi kazi ni kulamba Asali tu. Kamba zimeshakatika kwa hiyo ni mwendo wa kula kokote tu.
 
No doubt Magufuli alimaster sana the art of propaganda. Alizishika media zote, hadi za nje kuna wakati ikatangazwa kwamba hazipaswi kurusha maudhui ya ndani bila kibali.

Media zote nchi, binafsi na zile za serikali hadi zile ambazo ziko tu online ambazo hazina usajili wa serikali zilijaa woga kumtaja Magufuli katika namna ambayo isingempendeza. Media nchini ziliimba mapambio ya kumsifu na kumtukuza mawizo mpaka machweo.

Propaganda za Magufuli zinanikumbusha propaganda za Adolf Hilter, Joseph Stalin na Mao Ze Dong. Hawa watu walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuaminisha mambo ambayo hayapo, walikuwa na uwezo wa kupandikiza nadharia zao na imani zao juu ya kadamnasi na ikaamini vivyo, huku nyuma ya pazia wakiwa na mauzauza yao kibao.

Magufuli alitupiga wapi? Kwanza alijifanya Rais wa wanyonge, akijua kwamba watanzania wengi over 40% tuko chini ya mstari wa umasikini wa $1 kwa siku, masikini wengi tulimpenda sana tukidhani ni mwenzetu lakini katu, hakuwa mwenzetu, JPM alikuwa tajiri sana.

Magufuli alijua kwamba watanzania hatupendi mafisadi, wengi tunadhani umasikini wetu kuna watu wanatuibia serikalini. JPM akaona atangaze nao vita kali, tukamsahau yeye ambaye alijilimbikizia mali nyingi sana, huku tukijua kwamba anapambana na mafisadi kwa ajili yetu, kumbe ni kwa ajili yake kwani kila alipotaifisha mali zao, zikawa zake na jamaa zake.

JPM master the art of public manipulation. Kwenye ziara zake alisimama barabarani, alizungumza na watu, akatoa fedha hadharani kwa watu wa hali ya chini, alitembelea hospitali na kutoa misaada hadharani kwa watu waliokuwa na hali ngumu huku kila media ikimulika. Vitendo vile vimewalevya wengi kudhani kwamba JPM was saviour, tukasahau kabisa na yeye ni mwanadamu mwenye tamaa na uchu, aliweza kufanya chochote pasi nasi kujua kuwa mali zetu zinaibwa na kuwekezwa kwenye hotels zake, real estate, mashamba na kuficha fedha nje ya nchi. Mtoto wa dada yake, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya fedha Dotto James alifanya kazi kubwa sana kusafirisha fedha za mjomba wake nje.

Naona leo wakimkumbuka sana. Nasikitika sana kuona wengi wakimkumbuka JPM pasi na wao kujua kwamba bado wamo kwenye dimbwi la mning'inio wa propaganda za JMP. Ila kama tungejua uozo na madudu aliyofanya nyuma ya pazi, pengine tungezinduka kutoka kwenye hangover hiyo. Tuishie hapo.
Getrude Mollel hivi ndio wewe O brain wa kule twitter?
 
Nonsense
 
Mbona unateseka hivi
kumtetea Mwendazake kuliko hata mahawara zake? Kwani
wewe ulikuwa nani wa
Magufuli?
Mama Janet mwenyewe
tumuona ananawiri baada ya
kumzika DIKTETA
Niteseke kwani mimi ndio mwenye hasira na maiti au ninyi ndio wenye hasira na maiti ndio maana kila siku mnafungua nyuzi kumzungumzia kuonesha hasira zenu?

Mimi nachokifanya ni kuonesha jinsi chuki zenu zilivyowaathiri kiasi kwamba akija mtu na kuwaambia chochote kibaya kuhusu Magu mnakikubali tu kisa kinamzungumzia vibaya Magu bila kujari hata kama kuna contradiction.

Huyo huyo Magufuli mlisema alichanja chanjo ya corona ya wachina kisiri siri na huyo huyo Magufuli alipokufa nyie nyie tena mnasema amekufa kwa corona kwa sababu hakuchanja alidharau corona.
Yote hayo ni chuki tu, sasa mimi nikieleza hayo ndio unaona namtetea Magufuli?
 
Magufuli kaua hilo halina ubishi. Siyo kwa sababu wewe uko hai na kwenu hakuna aliyeuliwa ndiyo useme hakuna! Jiulize tu kwa nini hatumuandiki Kikwette au Mwinyi na Mkapa kwa habari hizi? Kwa nini yeye tu!!
Iv waliouliwa Zanzibar alikuwa ni magufuli acha akili za kibwabwa
 
Hata mumchfue vp yeye atabaki kuwa rais bora na mzalendo kuwahi kutokea nchi hii ukimtoa nyerere.. tumeshaamini hivi na ww amin mama ako ndo rais bora
 
Magu ni mtu mwizi sugu wa siku nyingi. Prof Assad alikagua akakuta Trillion 1.5 haijulikani ulipo, hazina haipo na wala haina maelezo ya matumizi. CAG Uttoh juzi amesema kuna Trillion 1.2 hazionekani. Lakin pia huyu jamaa ana historia ya wizi toka yupo wizara ya ujenzi, ni mabilioni na mabilioni yameibiwaga kipindi chake. Na aliposhika madaraka ndo akawa anaua anavyotaka yoyote ambae anaenda kinyume nae
Screenshot_20220726-155140_1.jpg

Screenshot_20220726-155151_1.jpg

Screenshot_20220726-154651_1.jpg

Screenshot_20220726-154953_1.jpg
 
Mbona vifo vya namna hivyo
havijawahi kutokea wakati mwingine bali wakati wake
pekee?
Ndio maana ni vizuri kujua uhusiano wa hivyo vifo na Magufuli ila tukisema tu kwamba tumuhusishe Magufuli kwa sababu hivyo vifo vilikuwa vinatokea katika kipindi chake basi pia endapo sasa hivi kutatokea vifo vya aina nyengine ambavyo havikuwai kuwepo tutasema anayeuwa ni Samia kwa sababu hivyo vifo havikuwepo vimetokea kipindi chake.

Hata kama una msimamo wa kwamba Magufuli alikuwa muuwaji ila haingii akilini kwamba et unaweza kumuhusisha na kifo chochote tu kisa yeye ni muuwaji.
 
Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika
Kabisa!

Na sasa tunainjoi maisha tunapumua!

Hakika sasa mahela yamejaa mifukoni!

Bei za bidhaa chini!

Democrasia kila kona!

Hakika tunapumua

Hata kama ulivyotaja kwa uchuro havipo, ni mara elfu kuliko kipindi cha dhalimu.
 
Umeliweka vizuri sana.

Vile vile akalidhoofisha Bunge kwa kumgeuza Spika kuwa wakala wake. Sijawahi kuona Spika ambaye ni puppet wa Rais hata enzi za chama kimoja. Akaitishia Mahakama isifanye maamuzi kwa uhuru.

Alijuwa pia kuwa 80% ya Watanzania ni wajinga, yaani hawana uwezo wa kuchambua ukweli na uwongo, hivyo basi kila alichosema wakakiamini na wanakiamini hadi leo. Kuna wajinga wanaamini eti aliishinda COVID-19 wakati yeye mwenyewe na akina Kikazi wamekufa kwa COVID-19 kwa jinsi walivyoipuuza.

Magufuli amefanya UFISADI mkubwa sana na kikundi cha wateule wake wachache lakini bado Watanzania wanamuona ni "shujaa" licha ya CAG kuonyesha discrepancies kubwa kwenye Ripoti ya 2020/21.

Magufuli aliiba mpaka uchaguzi wa vitongoji wa 2019 na uchaguzi Mkuu wote still watu wamesahau wanasema eti alikuwa mzalendo.

Kuna maeneo alisema kwa kuwa walichagua wapinzani basi hapeleki miradi ya maendeleo, nako kuna wajinga wakiambiwa eti mafuta yamepanda bei, wanasema angekuwako Magufuli yasingepanda. UJINGA ni tatizo la Watanzania
Kwan bunge la Sasa lina afhadhal gan
 
Naona Mnapambania Watu shibe zao.

Wengine wapo kazini mkiwajibu wanapata walau kitu[emoji23] ( Hii andiko ni la kimkakati)
 
Ona huyu pimbi! Kazikwe nae Chato, mbwa Wewe, nilimkula
Acha uzwazwa!

Magufuli vile, Magufuli hivi,

Jengeni nchi acheni kujificha kwenye kivuli chake mataahira nyie
 
Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika

Hata kama ulivyotaja kwa uchuro havipo, ni mara elfu kuliko kipindi cha dhalimu.
Si kwa mabwana zenu kina mbowe walizibiwa milango ya kuramba asali
 
Marehemu 7 vs 0 WalioHai

Ni marehemu , alafu yuko mmoja , ila anawagaragaza sana
 
Ingia basi hata ajira portal uangalia?

Sasa kila kitu ukitaka tukuwekee hapa huoni tutakuwa tunarudia mambo? Unamiliki technolojia unashindwa kuji update?

Alizindua viwanda hadi mkalalamika, sijui hizi propaganda mnazipika za Nini! Tanzania ya Viwanda mmepotezea Sasa hivi kazi ni kulamba Asali tu. Kamba zimeshakatika kwa hiyo ni mwendo wa kula kokote tu.
Kama ni vile viwanda vya cherehani tatu sawa.
 
Back
Top Bottom