Haniulizi kwa lolote

mkuu marry her and build an empire, dada anajielewa na umesema ana connection na watu wazito hapo ndo pazuri
 
Mkuu mbona hiyo issue ya mwezetu na mapenzi wake mda si mrefu nimeisikia mawingu Fm dada mmoja anaitwa Diva ameisoma kama ilivyo au jamaa kaifikisha huko??
Achana na yule malaya ndio zake kila siku kutoa story huku na kuzipeleka kwenye kipindi chake.
Members wa huku wamekuwa wakiilalamikia sana hii tabia yake.
 
Achana na yule malaya ndio zake kila siku kutoa story huku na kuzipeleka kwenye kipindi chake.
Members wa huku wamekuwa wakiilalamikia sana hii tabia yake.
Kiukweli na mimi imenishtua ndo nilikuwa nimemaliza kusikiliza kipindi cha sport extra mda kidogo nasikia huyo dada anaisoma!!!!
 
Mkuu ulitaka afanye nini? Akubembeleze? Wewe tayari unajitambua, hivyo ukimwambia kitu anajua unamaanisha nini? Kweli watu wawili wawili hata kwa tabia si kufanana sura tu. Ahahahahahahaa
 
Huyo dada alilelewa na wadhungu..... !! western system..

Yeah hili ndio jibu la mtu anaye fkiria fasta na sharp mind..maana me pia nmepasua sana kichwa apo ckuelewa uyo mwanamke ni wa aina gan ad baada ya kusoma hii comment .kwa iyo apo akili kumkichwa you either enjoy the moment with her..ila kama umempenda just be careful maana kumpoteza mtu kama huyo ni dkk 2 mbele..tena yuko vzuri uyo ndo wa kuoa..anakupa adi chance ata week no kukutafuta.c ndio pakujiachia apo..sio madem wa system za kibongo wanabana adi penati..
 
hii story imesomwa kama ilivo clouds fm mda huu, kumbe ndo zake huyu
Achana na yule malaya ndio zake kila siku kutoa story huku na kuzipeleka kwenye kipindi chake.
Members wa huku wamekuwa wakiilalamikia sana hii tabia yake.
 
Kaka sikufichi huwa natamani sana kuwa na mwanamke wa namna hii na katika maisha yangu yote sijawahi kumpata. Huyu dada ukimchunguza vizuri ana mengi aliyopitia ambayo yamemfanya yeye kuwa hivyo leo. Anajitambua, anajielewa na anajua thamani yake. Anajua wanaume tukoje na tunataka nini. Anaendeshwa na akili zaidi kuliko mihemko ya hisia ambayo ukiendekeza utakufa kwa presha. Siku hizi katika mapenzi watu watakukosea bahati mbaya na wakiona upo kimya watakukosea makusudi na hilo ndilo unalolifanya bro.unaonekana mtoto mbele yake. Ila ukiona humuelewi jua hapo ndio unakaribia kumuelewa sasa. Ushauri wangu ni huu kaka oa huyo mwanamke.
 
43 Years umeshindwa kumwelewa vema kwa mda ulokaa nae?
 
Umechambua vizuri sana, kazi kwake bigmomkipipa
 
Ningepata moyo wa huyo dada maisha yangu ya mapenzi yasingenitesa kabisa. Huyo dada ana moyo wa kiume. Inaitwa ukitaka kaa ukichoka wasalimie.
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Nimecheka sana jinsi ulivyohadithia. Huyo dada umemzidi umri tu lakini kwenye maswala ya mahusiano amepevuka kwa kiwango cha juu. Hayo unayotaka afanye alishayafanya sana akaishia kwenye maumivu ndo akafika hapo alipo sasa. Hapo alipofikia ni mtu mwenye kujitambua, ana uhakika na anachokitaka kwako, hana ubadhirifu wa moyo-anatumia akili aliyopewa na muumba wake na ndiyo maana amekuchagua akifikiri kwa ukomavu wako mtaweza kuendesha mahusiano lakini unataka kuleta mambo ya watoto.

Katika yote uliyotaja hakuna sehemu inayoonyesha ni mkorofi wala asiyejali. Hujaonyesha kama ulishakuwa na tatizo genuine halafu hakujali. Matatizo yote ni ya kutengeneza tu ili kutingisha kibiriti. Haya sasa umeshajua kibiriti kimejaa. Amua sasa. Mwenzio hataki kuyumbishwa bila sababu za msingi,na anaamini wewe ni mtu mzima mwenye uwezo wa kufanya maamuzi. Na kwa umri wako anatarajia wewe ndo umdekeze lakini ndo kwaaanza unaenda antiklokwaiz!! Yaani umepata mwanamke aliyeweza kukunyooshea mtoto wako uliyekuwa umemshindwa, si muongo, si mzinzi, si mvivu, si mnafiki eti kasoro yake ni kutokukutegemea kihisia? Kwanza hata umshukuru Mungu wako kwamba binti yako amemkubali na kumtii huyo dada. Ina maana dalili za kuwa na familia yenye umoja na kuheshimiana ipo. Huijui mitihani ya wenzio wewe. Chukua somo kwake, kisha fanya kazi ya kumpenda. Baas. Siyo kwa sababu hakuombi hela eti ndo usimnunulie hata unyunyu au kufuli au kumtoa. Hakuna biskuti ngumu kwa chai. Man up.

Hayo maneno ya dada yako yaache pale pale mlipokutana. Yaani kamuona mtu siku moja tu keshauliza kama utamuweza? Kwani kwenye hiyo miaka mitatu ulimuwezaje? Wanawake wasiojiamini ndo hujipendekeza kwa mawifi kutafuta kukubalika. Na wadada hupenda wanawake wadhaifu ili wao washike remote za ndoa za kaka zao. Huyo mpenzi wako keshajikubali mwenyewe inatosha. Sasa wewe pima misuli yako ya akili. Ukiona ngumu kuishi na huyo bibie tafuta huyo unayemtaka; wapo bwerere ila huyo uliye nae wako wachache sana.
 
Ningepata moyo wa huyo dada maisha yangu ya mapenzi yasingenitesa kabisa. Huyo dada ana moyo wa kiume. Inaitwa ukitaka kaa ukichoka wasalimie.
Hahahaa.... huyo dada ana moyo wa mwanadamu anayejitambua. Kama huo ni moyo wa kiume mbona huyu mwanaume wake hana? Ina maana huyu mwanaume ana moyo wa kike? Kidhaifu cha kike, imara cha kiume siyo?
 
Huyo mwanamke kichwani kwake tayari kushakuwana na ile akili ukimuonesha mtu unampenda sana atakuumiza kikweli huyo mwanamke anakupenda sana na hataki kukupoteza kwaiyo anachofanya ni bora afe kijerumani tu


Ila fanya uoe umri unakuacha huo
 
mkuu marry her and build an empire, dada anajielewa na umesema ana connection na watu wazito hapo ndo pazuri
Na kwa kujielewa kwake sijui kama atakubali kuolewa na mtu asiyekuwa na msimamo anabadilika kama kinyonga, anayetaka kubembelezwa, jamaa kamzidi miaka kumi bado anataka afanyiwe yale ambayo yeye ndio angemfanyia mwenza wake.
 
ila aina hiyo ya wanawake ni wale walioyaona mengi na wameyafnya mengi pia,unakuta kuna wkt alikua akipaparika let say na wazungu lkn mwisho wa siku anaona ni bull shit,sasa anaamua kuishi kivyovyote ili atimize lengo lake(kuolewa), kwa hio kwa mtu km ww haoni jipya,isitoshe umri umeenda huna choice kubwa,mwanamke anajua anachofanya.

pia lazima ujue aina hiyo ya wanawake lazima akukontro upende au usipende,na akikuchoka hawajui kupindisha maneno anakuchana live nimekuchoka. oa bro umri huo.
 
Mnachezeana sababu muda wenu muafaka umekwisha hivyo hamna budi kuishi kwa kuoneana huruma.
Shutka hakuna mapenzi hapo.
 
Kama ameeza kukupooza moyo na hana michepuko na kamrudsha mwanao kwenye mstari na anafanya vizuri darasani.
Unasubiri nini usimuoe, we subiri kudekewa ngoja akate kona hutamuona tena!
Marry her.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…