Haniulizi kwa lolote

Haniulizi kwa lolote

That's my kind of woman. Mkuu, umeokota almasi ila hujui tu maana sisi wengine,hayo malalamiko huwa tunajisikia kuyatoa pale tunapokutana na mwanamke mwenye wivu na tatizo la kufuatilia sana.
 
Habari
Naomba nianzie mbali kidogo, mimi ni mwanaume wa miaka 43. Sijaoa ila niko mbioni kuoa. Wakati nilipomaliza kidato cha nne, nilijikuta katika mahusiano yaliyoniletea mtoto wa ujanani mapema sana. Mama wa mtoto huyu tuliachana nilipoingia chuo kikuu, hivyo nikawa kwenye mahusiano ya hapa na pale ambayo hayakudumu kwa kweli kiasi cha kufikia kuoana.

Mtoto wangu alipofikisha miaka 10 nilimchukua toka kwa mama yake na kuanza kuishi naye wakati huo nikiwa naishi kwa wazazi na hata nilipoanza kujitegemea niliondoka naye na niko naye hadi sasa na ni binti mkubwa tu. Kuna wakati tulikwaruzana sana na binti yangu. nadhani katika zile hatua za ukuaji. Akawa mtukutu sana na mwenye maendeleo mabaya shuleni.

Sasa katika kutafuta mahusiano nikajikuta katika mahusiano na mwanamke mmoja ambaye nimemzidi miaka 10. Mwanadada huyu tulikutana katika halfa fulani. Tukafahamiana na taratibu tukawa marafiki. Kiukweli nilivutiwa naye sana sio tu kwa mvuto alionao, bali pia namna alivyokuwa amejiweka. Msomi, mjasiriamali, muelewa na msikivu.

Nikawa nasita kidogo kumtokea nikihofia tofauti ya umri lakini siku moja akaamua mwenyewe kunieleza hisia zake. Nilishangaa sana mwanamke kunitokea.

Hivyo ndivyo tukajikuta katika mahusiano, Nakiri kwanza kuwa amenisaida mno kumnyoosha binti yangu kitabia na kitaaluma. Hivi ninavyoandika binti yangu anafanya vizuri darasani na ana nidhamu kwangu.

Ni miaka miwili tangu niwe na huyu dada inaelekea watatu lakini kinachonifanya niombe ushauri ni mambo madogo madogo ambayo nayaona kwa huyu dada na yananipa msongo kwa kiasi fulani, sielewi tatizo ni mimi au huyu dada.

Kwasasa tunaishi pamoja, ingawa ana kwake pia ila muda mwingi yuko nyumbani kwangu. Huyu dada hajui kubembelezana na mtu. yaani hana zile hulka za kike kike za mkikosana abembeleze au anune nune hivi. Huyu hana kabisa. Akikosea ataomba radhi hapo hapo na amemaliza. Ukimkaushia imekula kwako kwa kuwa akikutafuta mara mbili tatu ukamchunia ni mpaka utakapoamua wewe kumtafuta na utamkuta poa tu wala hakuulizi kwanini ulimkaushia.

Pili, Ukimkosea hana zile analia au kusema mpenzi wangu umeniumiza na vitu kama hivyo, yeye atakwambia abcd zake na amemaliza. Uombe radhi au upotezee hana habari. Hili jambo ndio huwa linaniacha hoi kabisa. Kuna wakati nilikuwa karibu na mwanamke fulani kazini. Akafuma meseji zenye utata kidogo. Alichofanya aliuliza na mimi nikajitetea kizembe sana ikawa basi, akaingia jikoni kupika na alipotoka uko akawa kama hakuona chochote.

Ni kama vile hana wivu ingawa pia akiona kitu tata anahoji kwa ukali kwelikweli na alishaniambia akichoka vituko atasepa kimoja, na mimi sitaki hilo litokee

Kuna wakati niliamua tu kumjaribu nikamkalia kimya, aliponitafuta nikamwambia nahitaji muda wa kuwa peke yangu. Nilijua labda atanibembeleza nimueleze tatizo. Aliitikia na kukubaliana nami. Huwezi amini alikaa wiki mbili kimya kabisa mpaka nilipoamua kumtafuta. Nikamuuliza kisa cha ukimya, akajibu ulisema unahitaji muda wa kuwa mwenyewe. Nilishangaa mno! Nikamwambia nimerudi. Akajibu karibu hakuuliza tatizo langu wala nini, Nilipomhoji kwanini haulizi hata kwanini nilikuwa kimya. Akanijibu we ni mtu mzima ukiamua utasema. Akaishia hapo.

Niliwahi kumkutanisha na dada yangu, masaa tu aliyokaa naye, aliniuliza huyu dada tutamuweza? Mbona hana bashasha za kiwifi wifi akimaanisha hazoeleki haraka. Marafiki zake ninaowajua ni watatu na sijawazoea kivile maana hata wao hawaelekei kunizoea.

Nikahisi labda anafanya hivi kwa kutafuta ndoa na angenionyesha makucha yake baadaye, nikamwambia mikakati ya ndoa tusitishe kwa sasa. Akajibu sawa wewe ndio muoaji, hakushtuka wala kukasirika. Baadae nikamwambia basi tuharakishe kufunga ndoa, akaniambia naonekana sijui nataka nini hivyo nitulize akili nijiulize kama kweli nataka kuoa na nataka kumuoa nani.

Nimekuwa nikichunguza kama ana mahusiano mengine ya nje, kwa miezi mitatu nilimfuatilia sana na sikugundua kitu chochote zaidi ya kuwa ana ukaribu na watu wenye pesa zao na hadhi kubwa kubwa. nahisi kama ananicontrol bila kujua najikuta namfanyia visa na vituko vya kitoto kila mara mradi tu anipe attention yake hata kama ni kunionyesha hasira ila wapi.

Anaweza akaamua kutokupika, na ukimuuliza anakujibu straight mimi sio wife hapa kwako ni mpenzi tu, nina uhuru wa kuamua kupika au lah. Majibu kama hayo nachoka kabisa ukizingatia nimemzidi miaka 10!

Ana mtoto mmoja ambaye, anaishi kwake pamoja na mdogo wake. Mtoto wa huyu baba yake ni mtu wa nje na hawana hata mawasiliano kwa kuwa hilo nimechunguza pia. Kama ni kunipenda alinitamkia mwenyewe japo mimi pia nilishampenda lakini sielewi kwanini yuko hivi alivyo.

Nifanye nini anionee wivu hata kidogo tu, au awe na hulka za kike, au kama wanawake wengine wanaonyenyekea waume zao aache uandava alionao… nikisema nitumie pesa kumhandle hata yeye anazo kiasi chake na huwa haombi chochote kile na hajawahi kuomba hata senti na nilitegemea na umri wake huo angenipapatikia kidogo ili nimuoe matokeo ni tofauti. Ila nampenda sana huyu dada maana kwenye sekta zingine kama mwanamke sio mtu wa mchezo.
Nitumie namba yake. Kuna jambo nataka kumuuliza anisaidie mkuu.

Tafadhali sana.
 
Anaona kuwa nyie wanaume sio oxygen kwa hiyo anaweza kuishi bila Nyie!!
 
Huyo ni mali na mimi ninapenda kuoa mwanamke wa aina hiyo kwani spendi kubembelezwa.
 
ngoja niwe kama yeye..nimempenda bure.wewe unavyotaka ufanyiwe ni kutiana stress
 
She is smart Lady!!!Yes I call her LADY..

Hataki kona kona..Jielewe..jiheshimu..U win her heart
 
Mkuu tafadhari naomba uniachie huyo broo pls nakuomba, [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
nakupa makavu live bila chenga...

1, umetongozwa ukakubali.. tukitongozwa maana yake me ni dereva.
2. jinga wewe unaact kama demu unamletea vituko vituko mambo ya kike.
3, haupo kama mwanaume umelegea legea hata uandishi wako unaonyesha kitu cha paragraph mbili umeandika kumi.

that woman she is controlling frick chukua au acha.

NB: KUWA MWANAUME
Wanawake wa kichagga wababe kweli,
Oa mchagga uone mziki wake....humo ndani.
Utafikiri wacheza boxer ( mike Tyson )
 
Ki ukweli wewe ni mwanaume mwenye wasi wasi mwingi,
Na ina onesha huna experience ya wanawake.
Mwanamke wa namna hiyo mara zote ni mzuri kiasi na mmbaya kiasi.
So naamini utayazingatia mwenyewe mambo mengine sio kila mtu ajue,
Ili mradi mambo yaende.

Pia huyu mwanamke kwa kuwa pesa anayo kiasi basi anao uhakika ya maisha ku a mazuri hata asipoolewa au akiolewa na mtoto anaye,
Hiyo pia inachangia.
Wala usiogope muoe tu, hana shida.
 
Ki ukweli wewe ni mwanaume mwenye wasi wasi mwingi,
Na ina onesha huna experience ya wanawake.
Mwanamke wa namna hiyo mara zote ni mzuri kiasi na mmbaya kiasi.
So naamini utayazingatia mwenyewe mambo mengine sio kila mtu ajue,
Ili mradi mambo yaende.

Pia huyu mwanamke kwa kuwa pesa anayo kiasi basi anao uhakika ya maisha ku a mazuri hata asipoolewa au akiolewa na mtoto anaye,
Hiyo pia inachangia.
Wala usiogope muoe tu, hana shida.
Binafsi nimempenda huyo dada anaelements Kama zangu Labda ni baada ya kufundishwa adabu na wanaume ya kuacha kulia lia kumganda mtu maana hakuna faida ila tofauti kidogo me huwa nahitaji huduma kiasi fulani hivi maana siko stable ajira hakuna nko shambani mara umachinga shida tupu
 
Binafsi nimempenda huyo dada anaelements Kama zangu Labda ni baada ya kufundishwa adabu na wanaume ya kuacha kulia lia kumganda mtu maana hakuna faida ila tofauti kidogo me huwa nahitaji huduma kiasi fulani hivi maana siko stable ajira hakuna nko shambani mara umachinga shida tupu
Vizuri Barbra,
Muombe mungu akusimamie salama maana kazi za shamba yataka hela nyingi kiasi kufanikisha shughuli hiyo mwanzo mwisho.

Ni vizuri sasa wanawake wa karne hii kutumia mfumo huu kama huyu Dada nadhani itakuwa poa sana na kwenye ndoa nyingi zitadumu kwa muda mrefu.
 
Vizuri Barbra,
Muombe mungu akusimamie salama maana kazi za shamba yataka hela nyingi kiasi kufanikisha shughuli hiyo mwanzo mwisho.

Ni vizuri sasa wanawake wa karne hii kutumia mfumo huu kama huyu Dada nadhani itakuwa poa sana na kwenye ndoa nyingi zitadumu kwa muda mrefu.
Shambani kuna changamoto sana maana unaweka tu hela kuna muda unasema naacha tu ukifikiria ambazo umeziweka unaamua kuendelea Mungu ni mwema Bado napambana tu niwe stable na mimi
Baba wala usimuache huyo dada tena wewe ndo uache drama zako na Huko Kununa nuna utamkumbuka utakuja na uzi mwingine Am 50yrs natafuta mke tutakushangaa hakuna aliyekamilika labda umtengeneze mwenyewe utakavo
 
Shambani kuna changamoto sana maana unaweka tu hela kuna muda unasema naacha tu ukifikiria ambazo umeziweka unaamua kuendelea Mungu ni mwema Bado napambana tu niwe stable na mimi
Baba wala usimuache huyo dada tena wewe ndo uache drama zako na Huko Kununa nuna utamkumbuka utakuja na uzi mwingine Am 50yrs natafuta mke tutakushangaa hakuna aliyekamilika labda umtengeneze mwenyewe utakavo
Ni kweli kazi ya shamba yataka moyo
Ila kama mtu akiwa serious, baadae ataona faida yake tena kubwa haswa,
Kazi ya shamba inalipa mno.

[emoji1] [emoji2] [emoji2] eti miaka 50 bado anatafuta mke daaah umenivunja mbavu aiseeeee.
 
Hawa huwa hawatanii. Akisema ataondoka, atondoka kweli..

Mimi ninaye wakwangu yupo hivyo hata nikilala nimekumbatia simu anaami nipo JF..

Acha utoto chukua jiko hilo..

Anaacha kupika kwakuwa ulipostpond mambo ya ndoa...

Ni kweli hujui unachokitaka...
 
Hakuna aliyekamilika mkuu...shukuru kwa huyo alivyo...wengine hawavumiliki...yaani huyo keshaisoma hii dunia na ameona akiendekeza vitu hivyo ataumia bure...huyo amejiwekea kinga ya kisaikolojia..yaani huwezi mzingua kabisa...as long as anakupenda na anatimiza majukumu yake vyema...shukuru Mungu kaka...akina atoto hawajatulia kabisa.
Unamwonea dadangu ATOTO jmn
 
Back
Top Bottom