Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio lililobaki, maana wanaume wooote mji huu unawamiliki mie nifanyeje sasa.
Mwanaume anapoamua kujifanya mwanamke, basi mwanamke inabidi uwe mwanaume tu maana hamna namna.ha haha huyo atamwendesha vizuri tu
Na alishamwambia kabisa vituko vikizidi anasepa, so muache na hulka zake za kike kike aje azisome nyayo.Kwanza huyu dada ana economic power inayompa ujasiri flani hivi.
Habembelezi mapenzi.
Pili,amechagua kuishi free stress life,amekupenda kwa akili na sio moyo. Moyo wake kazi yake ni kusukuma damu tu,hataki ujihusishe na mengine.
Tatu mapenzi ni kubembelezana,kama yeye hakubembelezi basi mbembeleze yeye,usijenge kuwa anayetakiwa kubembelezwa ni mwanaume tu.
Mwisho kabisa acha vituko,akichoka ataondoka kweli,ninavyomjua hataniagi...
Ohooo...
Ngoja basi nikutafutie mume au nikuachie mmojaNdio lililobaki, maana wanaume wooote mji huu unawamiliki mie nifanyeje sasa.
na maisha lazima yasongeMwanaume anapoamua kujifanya mwanamke, basi mwanamke inabidi uwe mwanaume tu maana hamna namna.
Huyu sasa hajaruka stage basi kabaka stage, zile stage za wababu za gubu gubuu ndio yupo now. Atafute mzee mwenzie wabembelezane.Ndio namshangaa huyu baba anataka kubembelezwa na utu uzima huu kama mtoto eti mambo yakuanza kununia jamani kazi ipo
Pale unapokuwa unahitaji dyu dyu tu, napo sio lazima kihiiivyo!! Ndio hili sasa!na dada anamwangia kama kakinyago
Dada anasomeka sana tu, rahisi mno kumuelewa, huyu jamaa ndio jipu.Ila ni shida sana atoto...
Mtu asiyesomeka??kuishi naye ni sawa na kutumikia adhabu usiyojua kosa lake.
Hivi mwanaume anaanzaje kununa?eti anatingisha kiberiti...Na alishamuambia kabisa vituko vikizidi anasepa, so muache na hulka zake za kike kike aje azisome nyayo.
unaweza kuta dada ana dido lake usipotaka dydyu anajiongeza tuPale unapokuwa unahitaji dyu dyu tu, napo sio lazima kihiiivyo!! Ndio hili sasa!
nakupa makavu live bila chenga...
1, umetongozwa ukakubali.. tukitongozwa maana yake me ni dereva.
2. jinga wewe unaact kama demu unamletea vituko vituko mambo ya kike.
3, haupo kama mwanaume umelegea legea hata uandishi wako unaonyesha kitu cha paragraph mbili umeandika kumi.
that woman she is controlling frick chukua au acha.
NB: KUWA MWANAUME
Hapana sitaki tena.Ngoja basi nikutafutie mume au nikuachie mmoja
Huyu dada ni kama umenisema mimi tabia za huyu dada sawa na zangu, ukiwa na mimi nikagundua una mtu nikifanikiwa kukuuliza jibu utakalonipa ndo hilo sihangaiki tena kukufuatilia najua kuna kitu sina ndo umekipata huko ila najua utarudi tu na utarudi kweli, sikuulizi mimi ninachoangalia umerudi kuna kitu huko umekosa wewe ni mtu mzima hupangiwi jinsi ya kuishi, ninachotaka uuthamini uwepo wangu basiHabari
Naomba nianzie mbali kidogo, mimi ni mwanaume wa miaka 43. Sijaoa ila niko mbioni kuoa. Wakati nilipomaliza kidato cha nne, nilijikuta katika mahusiano yaliyoniletea mtoto wa ujanani mapema sana. Mama wa mtoto huyu tuliachana nilipoingia chuo kikuu, hivyo nikawa kwenye mahusiano ya hapa na pale ambayo hayakudumu kwa kweli kiasi cha kufikia kuoana.
Mtoto wangu alipofikisha miaka 10 nilimchukua toka kwa mama yake na kuanza kuishi naye wakati huo nikiwa naishi kwa wazazi na hata nilipoanza kujitegemea niliondoka naye na niko naye hadi sasa na ni binti mkubwa tu. Kuna wakati tulikwaruzana sana na binti yangu. nadhani katika zile hatua za ukuaji. Akawa mtukutu sana na mwenye maendeleo mabaya shuleni.
Sasa katika kutafuta mahusiano nikajikuta katika mahusiano na mwanamke mmoja ambaye nimemzidi miaka 10. Mwanadada huyu tulikutana katika halfa fulani. Tukafahamiana na taratibu tukawa marafiki. Kiukweli nilivutiwa naye sana sio tu kwa mvuto alionao, bali pia namna alivyokuwa amejiweka. Msomi, mjasiriamali, muelewa na msikivu.
Nikawa nasita kidogo kumtokea nikihofia tofauti ya umri lakini siku moja akaamua mwenyewe kunieleza hisia zake. Nilishangaa sana mwanamke kunitokea.
Hivyo ndivyo tukajikuta katika mahusiano, Nakiri kwanza kuwa amenisaida mno kumnyoosha binti yangu kitabia na kitaaluma. Hivi ninavyoandika binti yangu anafanya vizuri darasani na ana nidhamu kwangu.
Ni miaka miwili tangu niwe na huyu dada inaelekea watatu lakini kinachonifanya niombe ushauri ni mambo madogo madogo ambayo nayaona kwa huyu dada na yananipa msongo kwa kiasi fulani, sielewi tatizo ni mimi au huyu dada.
Kwasasa tunaishi pamoja, ingawa ana kwake pia ila muda mwingi yuko nyumbani kwangu. Huyu dada hajui kubembelezana na mtu. yaani hana zile hulka za kike kike za mkikosana abembeleze au anune nune hivi. Huyu hana kabisa. Akikosea ataomba radhi hapo hapo na amemaliza. Ukimkaushia imekula kwako kwa kuwa akikutafuta mara mbili tatu ukamchunia ni mpaka utakapoamua wewe kumtafuta na utamkuta poa tu wala hakuulizi kwanini ulimkaushia.
Pili, Ukimkosea hana zile analia au kusema mpenzi wangu umeniumiza na vitu kama hivyo, yeye atakwambia abcd zake na amemaliza. Uombe radhi au upotezee hana habari. Hili jambo ndio huwa linaniacha hoi kabisa. Kuna wakati nilikuwa karibu na mwanamke fulani kazini. Akafuma meseji zenye utata kidogo. Alichofanya aliuliza na mimi nikajitetea kizembe sana ikawa basi, akaingia jikoni kupika na alipotoka uko akawa kama hakuona chochote.
Ni kama vile hana wivu ingawa pia akiona kitu tata anahoji kwa ukali kwelikweli na alishaniambia akichoka vituko atasepa kimoja, na mimi sitaki hilo litokee
Kuna wakati niliamua tu kumjaribu nikamkalia kimya, aliponitafuta nikamwambia nahitaji muda wa kuwa peke yangu. Nilijua labda atanibembeleza nimueleze tatizo. Aliitikia na kukubaliana nami. Huwezi amini alikaa wiki mbili kimya kabisa mpaka nilipoamua kumtafuta. Nikamuuliza kisa cha ukimya, akajibu ulisema unahitaji muda wa kuwa mwenyewe. Nilishangaa mno! Nikamwambia nimerudi. Akajibu karibu hakuuliza tatizo langu wala nini, Nilipomhoji kwanini haulizi hata kwanini nilikuwa kimya. Akanijibu we ni mtu mzima ukiamua utasema. Akaishia hapo.
Niliwahi kumkutanisha na dada yangu, masaa tu aliyokaa naye, aliniuliza huyu dada tutamuweza? Mbona hana bashasha za kiwifi wifi akimaanisha hazoeleki haraka. Marafiki zake ninaowajua ni watatu na sijawazoea kivile maana hata wao hawaelekei kunizoea.
Nikahisi labda anafanya hivi kwa kutafuta ndoa na angenionyesha makucha yake baadaye, nikamwambia mikakati ya ndoa tusitishe kwa sasa. Akajibu sawa wewe ndio muoaji, hakushtuka wala kukasirika. Baadae nikamwambia basi tuharakishe kufunga ndoa, akaniambia naonekana sijui nataka nini hivyo nitulize akili nijiulize kama kweli nataka kuoa na nataka kumuoa nani.
Nimekuwa nikichunguza kama ana mahusiano mengine ya nje, kwa miezi mitatu nilimfuatilia sana na sikugundua kitu chochote zaidi ya kuwa ana ukaribu na watu wenye pesa zao na hadhi kubwa kubwa. nahisi kama ananicontrol bila kujua najikuta namfanyia visa na vituko vya kitoto kila mara mradi tu anipe attention yake hata kama ni kunionyesha hasira ila wapi.
Anaweza akaamua kutokupika, na ukimuuliza anakujibu straight mimi sio wife hapa kwako ni mpenzi tu, nina uhuru wa kuamua kupika au lah. Majibu kama hayo nachoka kabisa ukizingatia nimemzidi miaka 10!
Ana mtoto mmoja ambaye, anaishi kwake pamoja na mdogo wake. Mtoto wa huyu baba yake ni mtu wa nje na hawana hata mawasiliano kwa kuwa hilo nimechunguza pia. Kama ni kunipenda alinitamkia mwenyewe japo mimi pia nilishampenda lakini sielewi kwanini yuko hivi alivyo.
Nifanye nini anionee wivu hata kidogo tu, au awe na hulka za kike, au kama wanawake wengine wanaonyenyekea waume zao aache uandava alionao… nikisema nitumie pesa kumhandle hata yeye anazo kiasi chake na huwa haombi chochote kile na hajawahi kuomba hata senti na nilitegemea na umri wake huo angenipapatikia kidogo ili nimuoe matokeo ni tofauti. Ila nampenda sana huyu dada maana kwenye sekta zingine kama mwanamke sio mtu wa mchezo.
Duh!!!Anyenyekewe yeye Mungu bwana!!
Yaani huyu dada nimempenda hadi nimetamani ningekuwa mwanaume.
mimi napenda kudeka .. ukinikuta nimebananishwa wewe nakuwa mpole nadeka tumiss chagga mbona na wewe nimekupenda, upo kama huyo dada very straight.....
Alafu unajinunisha kwa mtu ambae hata habari hana!! Unaweza kujitukana aiseee!!Hivi mwanaume anaanzaje kununa?eti anatingisha kiberiti...
Ni tabia za viboyfriend na vigirlfriend vya sekondari. Kwa mtu mzima kama huyu ni ujinga