Hans Poppe: Hali ya kiuchumi Simba SC si nzuri

Hans Poppe: Hali ya kiuchumi Simba SC si nzuri

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba hali ya kiuchumi si nzuri katika klabu hiyo, kutokana na mapato katika mechi zao kushuka kwa zaidi ya asilimia 50.

Kwa sababu hiyo, Poppe amesema wamejikuta wanaingia kwenye migogoro ya kulipa madeni mbalimbali, lakini hawajadhamiria kumdhulumu yeyote.
"Hakuna ambaye amekataa kumlipa Tambwe (Amissi). Hayo ni makubaliao yetu sisi na yeye baada ya kumuacha, kwamba tutamlipa kiasi gani. Lakini tatizo hatuna fedha.

"Mechi zetu za Ligi Kuu kwa sababu ya kuonyeshwa kwenye Televisheni watu wanakuwa hawaji kwa wingi uwanjani. Mgawo wa mapato ya mechi zetu kwa kweli ni aibu. Huwezi kufidia gharama za siku moja tu za kambi,"amesema.

Poppe ameshauri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lijadiliane na Azam TV waliouziwa haki ya kurusha matangazo ya Televisheni ya Ligi Kuu,
ili waziongezee fedha klabu kubwa.

"Ni kweli sisi (Simba na Yanga) tumeathirika kwa sababu ndiyo tuna mashabiki wengi. Huko nyuma kabla ya Azam TV kuanza kuonyesha ligi, tulikuwa tunapata fedha nyingi hata kwenye mechi ndogo tu.

Lakini sasa hata ukicheza na timu kama Mtibwa Sugar, Kagera Sugar au Azam mambo magumu,"amesema Poppe.

Amesema si sahihi kuwapa Simba na Yanga wenye mashabiki wengi kote nchini mgawo sawa na klabu nyingine na akaishauri TFF, kukutana na Azam TV na kujadili namna ya kuzisaidia klabu hizo kongwe.

"Sisi tumeathirika mno kwa kweli. Watu hawaji mpira wanakaa tu kwenye maeneo yao wanaangalia Azam TV,"amesema.
Simba SC inakabiliwa na madeni mbaimbali kutoka kwa waajiriwa wake iliyowaondoa kazini kama kocha Mcroatia Zdravko Logarusic
ambaye anadai Sh. Milioni 112.

Logarusic alifukuzwa Simba SC Agosti mwaka jana kiasi cha mwezi mmoja baada ya kusaini Mkataba mpya na klabu hiyo, baada ya ule wa awali wa majaribio wa miezi sita ulioanza Desemba 2013 kumalizika. Na mwalimu huyo ambaye kwa sasa anafundisha AFC Leopard ya Kenya, anataka alipwe dola 6,000 ambazo ni mshahara wake wa mwezi mmoja, Agosti na dola 50,000 kwa kuvunja mkataba.

Kesi hiyo ilitarajiwa kusikilizwa juzi mbele ya Kamati Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti Richard Sinamtwa, lakini ikashindikana kutokana na mapungufu kadhaa na sasa itapangiwa siku nyingine.

Upande wa Simba SC uliowakilishwa na Katibu wake, Stephen Ally uliomba uthibitisho kwa mwakilishi wa Logarusic katika kesi hiyo kama kweli ameagizwa na kocha huyo, lakini ukakosekana.

Wakili wa Loga akaambiwa aende kupata uthibitisho wa kupewa jukumu la kumuwakilisha Mcroatia huyo na baada ya hapo, kesi itaanza kusikilizwa.
Aidha, kiungo wa Simba SC, Haroun Chanongo anayecheza kwa mkopo Stand United ya Shinyanga naye ameishitaki klabu hiyo.

Chanongo anadai wakati anapelekwa kwa mkopo Stand United Novemba mwaka jana, makubaliano yalikuwa ni kila klabu ilipe nusu katika mshahara wake. Hata hivyo, Chanongo amesema kwamba tangu anodoke Simba SC hajawahi kupewa nusu mshahara wake, wakati wa Stand anaendelea
‘kukunja' kama kawaida bila mushkeli.

Madai ya Tambwe ni jumla ni dola za Kimarekani 7,000 (Sh. Milioni 14 za Tanzania), kati ya hizo 1,000 zikiwa ni mshahara wa mwezi mmoja na nyingine za kuvunjia Mkataba. Simba SC wamepewa hadi Aprili 30 kuwa wamemlipa Tambwe dola 5,000 na nyingine wamalizie Mei 10, mwaka huu- na wakishindwa kufanya hivyo watakatwa fedha zote mara moja katika mapato ya mechi zao.

Source: bin zubeiry blog
 
Si mnasema mtani Jembe lina hela nyingi kuliko ubingwa wa Vodacom
 
Hapo ndipo tunapoona tofauti ya viongozi wa yanga na simba, wakati viongoz wa yanga wanagomea mgao wa haki za matangazo ya live ya mpira wa miguu kuwa mdogo kwa vilabu vya yanga na simba, viongoz wa simba kutokana na umbumbumbu wao wakasema zinatosha.....
Sasa sijui wanapolalamika sasa hivi wanataka nini tena?!!!
 
Waache wafe kwa njaa si waliingia kichwa kichwa mikataba na azm tv!!!
Yanga waliona mbali, wao kwa sababu ya njaa zao wakalikoroga....
 
Mimi ni shabiki wa simba lakini viongozi wanasababisha madeni kwa kuvunja mikataba hovyo hovyo, halafu wawe wabunifu,waongeze vyanzo vya mapato badala ya kusema mapato ya mlangoni yameshuka aseme msimu huu wamepata sh. Ngapi kwa kuuza bidhaa za simba kama jezi, skafu, kalenda nk.
 
Viongozi waachane na mapato ya milangoni kabisa,waje na plank B na C namna ya kubuni mipingo ya hela sio tu mtu anataka uongozi wakati ubunifu =0
 
Hivi haya ma simba na yanga yatakuwa lini? Utoto umezidi hivi haya matimu yatategemea mapato ya milangoni mpaka lini.?swain
 
Simba tv kwenye azam tv haionekani....full uswahili,azam siwo wanamapinduzi bali wavurugaji
 
Yanga waliyaona hayo mapema wakaonekana wabaya. Sasa kiko wapi?
Ulaya kuna namna mbili tofauti kwenye mapato ya Tv. Kule Spain Barca na R Madrid wanapata zaidi kwa sababu alizoainisha Hans Pope. Lakini Uingereza mapato hufuatana na nafasi kwenye msimamo wa ligi inapoisha.

Hii ya Uingereza ingetufaa zaidi na kuifanya ligi kuongeza ushindani. Angalia Uingereza walivyogawana msimu wa 2013/13. Wa kwanza alipata mara mbili ya yule wa mwisho.

EPL 2012_13.jpg
 
Ni kweli ana point ya kuwa kuwapa Simba na Stendi United pesa sawa ni uonevu

ambacho TFF na Jamal Malinzi wanapaswa kufanya ni kuwa mgao uende na position uliyomalizia last season

mfano Bingwa mtetezi alipwe zaidi ya wote....anafuata namba mbili na namba tatu hadi mwisho kabisa

Azam washarudisha faida sasa wanapaswa kulipa zaidi

Na timu kama Simba kukosa pesa nayo ni aibu sana
hawana maduka yao ya kuuza jezi?
magazeti ya Simba yanamilikiwa na nani?
kwa nini wasiwe na TV yao ambayo watu watalipia?
 
Last edited by a moderator:
Njaa hupunguza uwezo wa kufikiri. Simba wana kipindi Azam Tv. Hawapati hela huko? Rage alishangalia sana suala hilo.
Kila timu kupewa mgao sawa sio haki. Pesa iendane na msimamo kwenye ligi.
 
Viongozi waachane na mapato ya milangoni kabisa,waje na plank B na C namna ya kubuni mipingo ya hela sio tu mtu anataka uongozi wakati ubunifu =0

Hebu toa plan b yako... nyie si ndo mnaonunua jezi feki za simba na yanga?! Kama unajua hizi timu zinapata mapato kupitia milangoni kwann uwapole hicho hicho kidogo
 
The Boss;

Hili haliwezekani, yanga na simba wanatakiwa wapate mapato zaidi bila kujali wameshika no ngapi sbb unapoonesha mechi unapunguza kiasi cha mapato walichostaili kupata....barca na real madrid wanapewa kiwango kikubwa cha pesa za tv rights kutokana na ukubwa wao..ligi tavern z na spain zinafann coz zote zina tim mbili zenye fan wengi
 
Msome Sibonike hapo juuu
 
Last edited by a moderator:
Hapo ndipo tunapoona tofauti ya viongozi wa yanga na simba, wakati viongoz wa yanga wanagomea mgao wa haki za matangazo ya live ya mpira wa miguu kuwa mdogo kwa vilabu vya yanga na simba, viongoz wa simba kutokana na umbumbumbu wao wakasema zinatosha.....
Sasa sijui wanapolalamika sasa hivi wanataka nini tena?!!!

Namshukuru Mungu kwa kuwa dhambi ya usaliti imewatafuna Simba, tena iwale mpaka waishe kabisa. Laiti wangeungana na Yanga kudai maslahi zaidi Azam TV angeongeza tu vinginevyo uwekezaji wake huo ungekuwa bure kabisa.

Hans Poppe asilie na Azam TV bali alie na Rage aliyesaliti 'move' ya Yanga kuelekea kwenye maslahi bora.
 
Waache wafe kwa njaa si waliingia kichwa kichwa mikataba na azm tv!!!
Yanga waliona mbali, wao kwa sababu ya njaa zao wakalikoroga....

Tofauti ya viongozi wa Simba na Yanga iko wazi sasa, mwenye macho haambiwi Tazama.
 
Namshukuru Mungu kwa kuwa dhambi ya usaliti imewatafuna Simba, tena iwale mpaka waishe kabisa. Laiti wangeungana na Yanga kudai maslahi zaidi Azam TV angeongeza tu vinginevyo uwekezaji wake huo ungekuwa bure kabisa.

Hans Poppe asilie na Azam TV bali alie na Rage aliyesaliti 'move' ya Yanga kuelekea kwenye maslahi bora.

Walikuwa wanajipendekeza kwa azam kutaka undugu kinguvu....na azam wamewawin na kuchukua nafasi yao kwenye ligi...asante yanga kwa kukataa undugu na hao washenzi
 
Back
Top Bottom