MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba
SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba
hali ya kiuchumi si nzuri katika klabu hiyo,
kutokana na mapato katika mechi zao
kushuka kwa zaidi ya asilimia 50.
Kwa sababu hiyo, Poppe amesema wamejikuta
wanaingia kwenye migogoro ya kulipa madeni
mbalimbali, lakini hawajadhamiria
kumdhulumu yeyote.
Hakuna ambaye amekataa kumlipa Tambwe
(Amissi). Hayo ni makubaliao yetu sisi na yeye
baada ya kumuacha, kwamba tutamlipa kiasi
gani. Lakini tatizo hatuna fedha.
Mechi zetu za Ligi Kuu kwa sababu ya
kuonyeshwa kwenye Televisheni watu
wanakuwa hawaji kwa wingi uwanjani. Mgawo
wa mapato ya mechi zetu kwa kweli ni aibu.
Huwezi kufidia gharama za siku moja tu za
kambi,amesema.
Poppe ameshauri Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) lijadiliane na Azam TV waliouziwa haki
ya kurusha matangazo ya Televisheni ya Ligi
Kuu, ili waziongezee fedha klabu kubwa.
Zacharia Hans Poppe amesema pato la Simba S
limeshuka kwa asilimia 50
Ni kweli sisi (Simba na Yanga) tumeathirika
kwa sababu ndiyo tuna mashabiki wengi. Huko
nyuma kabla ya Azam TV kuanza kuonyesha
ligi, tulikuwa tunapata fedha nyingi hata
kwenye mechi ndogo tu. Lakini sasa hata
ukicheza na timu kama Mtibwa Sugar, Kagera
Sugar au Azam mambo magumu,amesema
Poppe.
Amesema si sahihi kuwapa Simba na Yanga
wenye mashabiki wengi kote nchini mgawo
sawa na klabu nyingine na akaishauri TFF,
kukutana na Azam TV na kujadili namna ya
kuzisaidia klabu hizo kongwe.
Sisi tumeathirika mno kwa kweli. Watu hawaji
mpira wanakaa tu kwenye maeneo yao
wanaangalia Azam TV,amesema.
Simba SC inakabiliwa na madeni mbaimbali
kutoka kwa waajiriwa wake iliyowaondoa
kazini kama kocha Mcroatia Zdravko
Logarusic ambaye anadai Sh. Milioni 112.
Logarusic alifukuzwa Simba SC Agosti mwaka
jana kiasi cha mwezi mmoja baada ya kusaini
Mkataba mpya na klabu hiyo, baada ya ule wa
awali wa majaribio wa miezi sita ulioanza
Desemba 2013 kumalizika.
Na mwalimu huyo ambaye kwa sasa
anafundisha AFC Leopard ya Kenya, anataka
alipwe dola 6,000 ambazo ni mshahara wake
wa mwezi mmoja, Agosti na dola 50,000 kwa
kuvunja mkataba.
Kesi hiyo ilitarajiwa kusikilizwa juzi mbele ya
Kamati Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya
Mwenyekiti Richard Sinamtwa, lakini
ikashindikana kutokana na mapungufu kadhaa
na sasa itapangiwa siku nyingine.
Upande wa Simba SC uliowakilishwa na Katibu
wake, Stephen Ally uliomba uthibitisho kwa
mwakilishi wa Logarusic katika kesi hiyo kama
kweli ameagizwa na kocha huyo, lakini
ukakosekana.
Wakili wa Loga akaambiwa aende kupata
uthibitisho wa kupewa jukumu la
kumuwakilisha Mcroatia huyo na baada ya
hapo, kesi itaanza kusikilizwa.
Aidha, kiungo wa Simba SC, Haroun Chanongo
anayecheza kwa mkopo Stand United ya
Shinyanga naye ameishitaki klabu hiyo.
Chanongo anadai wakati anapelekwa kwa
mkopo Stand United Novemba mwaka jana,
makubaliano yalikuwa ni kila klabu ilipe nusu
katika mshahara wake.
Hata hivyo, Chanongo amesema kwamba
tangu anodoke Simba SC hajawahi kupewa
nusu mshahara wake, wakati wa Stand
anaendelea kukunja kama kawaida bila
mushkeli.
Madai ya Tambwe ni jumla ni dola za
Kimarekani 7,000 (Sh. Milioni 14 za Tanzania),
kati ya hizo 1,000 zikiwa ni mshahara wa
mwezi mmoja na nyingine za kuvunjia
Mkataba.
Simba SC wamepewa hadi Aprili 30 kuwa
wamemlipa Tambwe dola 5,000 na nyingine
wamalizie Mei 10, mwaka huu- na
wakishindwa kufanya hivyo watakatwa fedha