Alex Mponela
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 254
- 109
ni kweli ana point ya kuwa kuwapa simba na stendi united pesa sawa ni uonevu
ambacho tff na jamal malinzi wanapaswa kufanya ni kuwa mgao uende na position uliyomalizia last season
mfano bingwa mtetezi alipwe zaidi ya wote....anafuata namba mbili na namba tatu hadi mwisho kabisa
azam washarudisha faida sasa wanapaswa kulipa zaidi
na timu kama simba kukosa pesa nayo ni aibu sana
hawana maduka yao ya kuuza jezi?
Magazeti ya simba yanamilikiwa na nani?
Kwa nini wasiwe na tv yao ambayo watu watalipia?
Mkuu vuta subira, soon mkwanja utatua.
Ikifika hapa ndio maana uwa namshukuru Mungu kwa kuzaliwa na kuwa mshabiki wa Yanga.
Wamlipe kwanza Tambwe ndipo wakajifie huko!
Kwanza usiitaje Yanga kwa sababu sisi ni mabingwa, pili sisi hatupatimihela ya azam tatu hizo ni maumivu ya kukosa ubingwa.Aise mnachekesha eti mwakani msuva anatua simba !!!!!! aje kufanya nini?Simba Aibu tupu nafasi ya tatuuuuuuuuuuuu mpaka mwaka 2020.Mapovu mpaka mtalewa
simba walikataa mkataba mkubwa sana toka zuku kwa sababu ya aden rage tamaa zake kwa kweli ni aibu timu kama simba ikalipwa sawa na singida kitu kingine wadai uwiano wa mechi uwe sawa kwani mechi nyingi zinazoonywesha ni za simba na yanga lakini mapato sawa halafu mauzo ya jezi hayaeleweki yanaenda wapi cha ajabu mbeya city wameweza kudhibiti mauzo ya jezi zao wakati simba wanahangaika
Rudia tena kusoma utamwelewa.Mkuu hebu nielimishe zaidi hapo kwa red, Yanga wao wananufaika vipi na azam TV? manake si mechi zao wanaonyesha?
simba walikataa mkataba mkubwa sana toka zuku kwa sababu ya aden rage tamaa zake kwa kweli ni aibu timu kama simba ikalipwa sawa na singida kitu kingine wadai uwiano wa mechi uwe sawa kwani mechi nyingi zinazoonywesha ni za simba na yanga lakini mapato sawa halafu mauzo ya jezi hayaeleweki yanaenda wapi cha ajabu mbeya city wameweza kudhibiti mauzo ya jezi zao wakati simba wanahangaika
Rudia tena kusoma utamwelewa.
Sawa simba wanapata mapato madogo kutokana na perfomance kushuka,lakini kwa perfomance hiyo hiyo ya chini kuna watu wangekuwa tayari kwenda uwanjani kama mechi zisingekuwa zinaoneshw na mapato yangekuwa na ahueni....siyo mara ya kwanza simba kufanya vibaya...kuna wakati walitaka kushuka daraja na bado watu walikuwa wanajaa uwanjani kuisapoti timu yao
Mkuu hebu nielimishe zaidi hapo kwa red, Yanga wao wananufaika vipi na azam TV? manake si mechi zao wanaonyesha?
Mkuu vuta subira, soon mkwanja utatua.
Tangu Azam TV waanze kuonesha mechi za ligi kuu, Yanga haijawahi kuchukua hata senti 1 ya udhamini huo. Mechi za Yanga zimeendelea kuoneshwa bure. Ni heri mechi zioneshwe bure kuliko udhamini feki wa 100m/=, huo ndio msimamo wa Yanga.
Ni furaha iliyoje Simba kuanza kulia njaa! Naamini mwakani wataungana na Yanga kuibana TFF ili udhamini wa Azam TV uboreshwe.
Seembo...unakumbuka kipindi kile unaongelea habar ya pesa za Etoel ukaanza na kuota ndoto za alnacha kuhusu uwanja wa bunju..pole bana hizo ndo timu zetu..zina wenyewe sio mm wala ww...kuna taarifa nusu ya fedha iliishapigwa zamaaan na viongozi waliopita