Hans Rafael anamuiga George Ambangile?

Ngareroo

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2019
Posts
2,123
Reaction score
2,449
Aslaam Aleykum wadau wa hapa JF.

Acha niende direct kwenye Mada.

Mimi ni mdau mkubwa sana wa michezo hasa basketball, Lakini football pia nafuatilia. Pia ni mdau mkubwa sana wa Media, Napenda Kusikiliza Uchambuzi wa Mpira wa miguu pale Sports Extra, Hili game, Sports Bar, Sports roundup kwa pale Clouds Media, Lakini pia Sports Arena na Sports Court pale Wasafi Media na wanachambua vyema na unapata Updates za sports kibingwa kabisa..

Kuna mchambuzi mmoja ananivutia sana uchambuzi wake. Ni mchambuzi wangu bora Akiwa nyuma ya The Morogoro Magic fingers "Farhan Kihamu" na Mwalimu "George Ambangile" Hawa washkaji wawili ni mafundi wa Mpira kwelikweli. Huyu jamaa si mwengine Bali ni Hans Rafael toka Wasafi media, In short chalii anavijua, Ana details nyingi sana about football, una'enjoy akiwa anachambua ball..

Kilichonifanya niandike Uzi huu niyeye Ku'sound kama George Ambangile, Sijajua kama labda ni role model wake au laa. Huwa napata ugumu sana kuwatofautisha kuwa hii sauti ya Ambangile au ni Hans mpaka watajwe majina ndio nasema Aanhaa kumbe ni Hans. Sijajua kama anamuiga Ambangile au sauti zao tu zinafanana. Au nyie mnaonaje?

@NgarenaroBoy.
 
Hii kitu nilijua ni Mimi peke yangu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hao jamaa sauti zao zinafanana balaa
 
Ambangile bado sijaona umahiri unaoimbwa. Kila ninaposikia maoni yake huwa namuona kama yupo too defensive, anajihami sana na kuogopa kufunguka, labda kwa kuogopa 'kuharibu' uhusiano na kundi la mashabiki wa upande atakaokuwa anauongelea negative. Kila mara anakuwa na kauli ya 'No comments'. Pengine silaha yake kubwa ni taaluma ya ukocha, ila anaiangusha kwa kuwa muoga kufungukia ishu mahususi
 

Yule ni kocha hawezi kuongea kiushabiki..inabidi ufahamu hilo
 
Yule ni kocha hawezi kuongea kiushabiki..inabidi ufahamu hilo
Si kwamba wanaofunguka wanaongea kiushabiki. Natolea mfano tu (sio lazima iwe hali halisi), wakati wachambuzi wengine wanaweza wakaweka wazi kuwa Tuisila Kisinda hastahili kuanza katika kikosi cha kwanza mbele ya Farid, yeye Ambangile huwa ni mzito kuongea kauli ngumu kama hizo, maybe kwa kuhofia atatafsiriwa kushiriki ukosoaji
 
Ambagile ndio ana achambua mpira. Fairly. Lakini hawa, akina Kazumari, wao wanachambua Chuki na Club zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…