Hans Rafael: Hakuna kipya alichoongea MO tofauti alichoongea msimu uliopita

Hans Rafael: Hakuna kipya alichoongea MO tofauti alichoongea msimu uliopita

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
"Binafsi nimemsikiliza Tajiri ila sijaona utofauti wa kile alichoongea msimu uliopita na leo.

1. Mo anasema ametoa zaidi ya Tsh 80b, inawezekana ni kweli Ila atwambie na Yeye Simba imemtengenezea kiasi gani?....maana kila mwaka anatumia Brand ya Simba kutangaza bidhaa zake.

2. Mo amesema kila mwaka anatoa hela ya usajili ila mambo yamezidi kuwa yale yale kila mwaka Simba wanasajili Wachezaji 17 na mwisho wa Msimu wanakata 14 je Mo haoni pale Simba kuna shida ya utendaji? Kwani asiwaondoe viongozi wote wanaosajili.....? na kuajiri watu wapya wa mpira kama (Technical Director na Drector of football) ili wasimamie vizuri project na Pesa zake? Kwanini ameendelea kuwakumbatia viongozi wale wale ambao kila msimu wanafuja pesa zake kwa kusajili Wachezaji wa kawaida?

Soma Pia: MO Dewji: Tangu 2018 nimewekeza Bilioni 87 Simba SC

Binafsi nadhani hakuna tajiri mjinga ambae kila mwaka atakubali kupoteza hela Yake Kama hapati faida......Mo amekomaa na Simba coz anapata faida, biashara zake zinaenda, Simba ni Brand kubwa ambayo kila tajiri nchini anatamani kuitumia leo asitufanye sisi kama watoto.

Ifike Muda matamko yakome, vitendo viongee, Simba kabla ya kupata hela ya Mo wanahitaji mfumo mpya wa katiba na viongozi Ila hawa wa Sasa sioni wakifanya Jambo".

Ameandika Mchambuzi Hans Rafael kupitia ukurasa wake wa Instagram.
 
Mchambuzi wako pendwa huyo na sasa ndio Fabrizio wa hapo Jangwani
 
Wenye share 51% wao wanachangia nini?

Kuendesha Club ya mpira usifananishe na kodi ya meza unayoiacha asubuhi nyumbani
Tunachohoji ni hayo malalamiko na masimango yake ya kila mwaka kuhusu hasara,kama anapata hasara kwanini asikae pembeni awaachie wengine na kingine mbona anataja hela alizotoa tuu mbona haweki mapato na matumizi?
 
Hans anawachotaga sana na nyie mnajaa as long as ana feed ego zenu

Na ndio mnaemtumia kwenye propaganda zenu za kishamba, well mta catch attention za mapimbi
Jibu hoja zake, acha porojo kama za Mwamedi
 
Inamaana yeye Kanji anatoa izo pesa kama msaada akuna faida anapata?.

Na kwanini aseme anazotoa kwenye club ya anazoingiza kupitia club hasemi?

Kama hapati faida anatoa tu pesa zake kwanini asiachane na Simba?

images.jpeg
 
Tunachohoji ni hayo malalamiko na masimango yake ya kila mwaka kuhusu hasara,kama anapata hasara kwanini asikae pembeni awaachie wengine na kingine mbona anataja hela alizotoa tuu mbona haweki mapato na matumizi?
Kabla ya kupima malalamiko tuanze na wewe, unaijua hata Bilioni inafananaje?

Huyu ni Raisi wenu hapa akilalamika kuhusu hasara na akaenda mbali akiwaita wala mihogo

Kumbuka huyu ni Chawa tu wala sio mtoaji pesa na wala hajui inatafutwaje lakini he knows the feeling of spending and get loss.

Ndio maana nakuambia huyo chawa wenu Hans anawapoteza sana kwa kuwa feed ego zenu.
 
Kabla ya kupima malalamiko tuanze na wewe, unaijua hata Bilioni inafananaje?

Huyu ni Raisi wenu hapa akilalamika kuhusu hasara na akaenda mbali akiwaita wala mihogo
View attachment 3406226

Acha porojo wewe chawa wa Mwamedi
 
Mchambuzi wako pendwa huyo na sasa ndio Fabrizio wa hapo Jangwani
Huyo jamaa uto wanamuamini vibaya mno licha ya kutoa maboko kwenye taarifa zake nyingi ila huwaambii kitu yani kwa alipofikia hata akisema yanga imekamilisha usajili wa yamal au salah uto watamuamini tu, jamaa baada ya kuona anakosa tetesi za simba kwa sababu zinafanyika kwa siri anaamua kutunga uongo wake na mashabiki wa uto wanamuamini na kumpa bichwa kama hivyo, kila mchezaji anakuambia alitakiwa na simba ila kasajiliwa uto na kwamba eti vita ilikuwa kali kati ya mo na gsm ila mwisho wa siku gsm ndio kashinda basi mashabiki wa uto wakisikia hivyo wanafurahi kweli na kujifariji
 
Kabla ya kupima malalamiko tuanze na wewe, unaijua hata Bilioni inafananaje?

Huyu ni Raisi wenu hapa akilalamika kuhusu hasara na akaenda mbali akiwaita wala mihogo
View attachment 3406226

Kumbuka huyu ni Chawa tu wala sio mtoaji pesa na wala hajui inatafutwaje lakini he knows the feeling of spending and get loss.

Ndio maana nakuambia huyo chawa wenu Hans anawapoteza sana kwa kuwa feed ego zenu.
Sawa lakini ilitakiwa iwe, "he knows the feeling of spending and getting loss" au sio jamaangu si tunaongelea uwingi na present continuous? Au loss ilitokea one time na haijatokea tena na haiwezi kutokea jalokuwa tajiri kila mwaka anasema hilo hilo?....
 
Msimu ulioisha walisema wamefanya usajili wa bilioni 7 anachofanya ni kuongeza sifuri tu.
Simba mpaka inaingia fainali ilikuwa inatangaza biashara zake hasemi Simba imelipwa kiasi gani.
Akumbuke kauli yake wakati anaingia Simba alisema Simba imekuwa inauza wachezaji wake waziri Ila yeye ataifanya Kama Al Ahly lakini tangia aingie Simba ndio imeuza wachezaji wengi zaidi huku kiasi wanachouzwa kinafichwa.
Aeleze zile kanga za Simba zinazouzwa na kiwanda chake mapato yanaenda wapi.
Kipindi chake Simba ndio inafungwa zaidi na yanga Ila anajificha kwenye mafanikio ya kimataifa.
 
Back
Top Bottom