Hanscana music video director "wa moto" zaidi Nchini

Hanscana music video director "wa moto" zaidi Nchini

Raymanu KE

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2022
Posts
8,611
Reaction score
16,118
Huyu director mi nahisi Kama upepo ndo kwanza umemuelekea anapiga hela nyingi Sana kutokana na demand aliyonayo kwenye music industry.

Yaani huyu jamaa ckuiz amekuwa wa Moto Sana when it comes to videography.Kuna muda huwa nakaa chini nawasha runinga na kuanza kuangalia muziki na bila Shaka hazitapita music videos 3 Kama sijaona hivi " Directed by Hanscana" kwenye screen.

Jamaa amevuma Tanzania nzima Yaani anang'ang'aniwa na Kila msanii Hadi amevuka border mpaka huku Kenya anafanya kazi na kina Otile Brown,Nadia Mukami na Masauti.

Kiukweli huyu mwamba amehusika kwenye music videos nyingi Sana katika ukanda huu wa Africa Mashariki.Mpinzani wake mkubwa alikuwa Kenny aliyekuwa anafanya kazi na Diamond Platinumz ila Cha ajabu Diamond alimtema na kumnyakua huyu Hanscana.

Nadhani hiki Ni kipindi chake na naamini ataenda mbali Sana mpaka nimeanza kuhisi hivi karibuni atakuja kuhusika kwenye action movies za akina Tonny Jaa, Iko Uwais,Donnie Yen na wengine wengi.
 
Huyu director mi nahisi Kama upepo ndo kwanza umemuelekea anapiga hela nyingi Sana kutokana na demand aliyonayo kwenye music industry.
Yaani huyu jamaa ckuiz amekuwa wa Moto Sana when it comes to videography.Kuna muda huwa nakaa chini nawasha runinga na kuanza kuangalia muziki na bila Shaka hazitapita music videos 3 Kama sijaona hivi " Directed by Hanscana" kwenye screen.
Kwanini asingetengeneza documentary ya maisha ya MBOWE, Freeman, apige hela zaidi?
 
Director Kenny alitemwa? Ndo naskia leo. So inamaana Hanscana saizi kaajiriwa kabisa na Mondi au bado anasimama mwenyewe ila anafanya kazi za Mondi?
 
Hamuwezi nisher huyo hata kidogo sema jamaa ana mashauzi mengi na yule ndo alikuwa mshindani wake halisi.
 
Ila kwenye video production ya Music na movie ni tofauti. Hapo Hanscana licha ya ubora wake ila akisnza kuhusika kwenye movie atapigwa gap mpaka na akina benloyal chipukizi huko Mbeya
 
He is already the goat kwa mambo aliyoyafanya kwenye production
 
He is already the goat kwa mambo aliyoyafanya kwenye production

Hivi ni nani alikuwa video director wa benchmark productions maana najua mmiliki alikuwa madam Ritha Ila yeye hajulikani

Kwa video kama

Nalia kwa furaha - K lyn ft Bushoke
Machozi - Lady jaydee (Best RnB video Kora awards)
Zali la mentali - Professor jay

Ukiachilia utofauti wa muda na mabadiliko ya teknolojia, video nyingi tu za leo hazizafikia kwa ubora hivyo, naamini jamaa ni one of the best video directors kuwahi tokea bongo
 
Huyu ni director mkubwa utashangaa kuna mbuzi walimfananisha na sijui Kenny yukwapi sasa? Kenny mwenyewe ni mwanafunzi wa hanscana

Naona jamaa anayemfuatia ni yule director anaitwa Elvis anajitahidi Sana.
 
Hivi ni nani alikuwa video director wa benchmark productions maana najua mmiliki alikuwa madam Ritha Ila yeye hajulikani

Kwa video kama

Nalia kwa furaha - K lyn ft Bushoke
Machozi - Lady jaydee (Best RnB video Kora awards)
Zali la mentali - Professor jay

Ukiachilia utofauti wa muda na mabadiliko ya teknolojia, video nyingi tu za leo hazizafikia kwa ubora hivyo, naamini jamaa ni one of the best video directors kuwahi tokea bongo
Aisee video karibia zote za Zamani za Profesa J zilikuwa kali halafu tena kwa enzi zile
 
Nisher alikiki Sana cjui nini kimempoteza
Aiseee
 
Back
Top Bottom