Hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya

Hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya

the numb 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2020
Posts
1,562
Reaction score
2,902
Nipo mitaa ya Osterbay kwa mbali naona mjengo wa Mo Dewji kwa mbali tena naona mjengo wa Paul Makonda kwa pembeni yangu naona mjengo wa makamu wa Rais nikapita Bongoyo road nikakutana na mjengo anaoish mtoto wa Bakhresa kwa kweli nimesikitika sana hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya kweli haya maisha hayako fear wengine tunaish tu duniani ila kuna viumbe wengine wanaenjoy life imebidi kuingia hapa simply fresh kupata hata ka kinywaji kidogo.

PESA INAUMUHIMU MKUBWA SANA KATIKA MAISHA YETU TUTAFUTE PESA JAPO AJIRA NI KIKWAZO SANA
 
Shukuru Mungu kwa kila jambo,saa nyingine Muumba anajua kuwa ungekuwa na hela saa hizi ungeshakuwa umekufa,kwahiyo ili kukunusuru ni bora uishi hivyo hivyo kiugumu...

Ni kwel mkuu kila jambo ni kushukuru Mungu ila maisha matam ni kwa watu wenye hela mzee sisi wengn bora siku zisonge tu
 
Tatizo la Bongo nyumba ikianza kuungua moto Fire Brigade mpaka watoke Bandarini au Airport wafike Oysterbay nyumba ishateketea.

Unapofananisha Bongo na Ulaya usifananishe majengo tu.

Angalia miundombinu pia.
 
Sina hakika km amejenga au alinunua ila mm nafkr itakuwa amenunua oystby kupata kiwanja duuh sidhan
Siku hizi wanakata kata viwanja.

Hiyo nyumba ya Bakhressa pale zamani lilikuwa shamba la mchicha la Shule ya Msingi Oysterbay.

Oysterbay siku hizi imekuwa ovyo sana wameweka mpaka gereji za magari, last time nilipofika nikashangaa barabara zilikuwa mbovu sana, pale shuleni.

Sijui kama sasa hivi wametengeneza.

Baada ya moratorium ya Mkapa ya kuuza nyumba kupita it will get even worse.
 
Shukuru Mungu kwa kila jambo,saa nyingine Muumba anajua kuwa ungekuwa na hela saa hizi ungeshakuwa umekufa,kwahiyo ili kukunusuru ni bora uishi hivyo hivyo kiugumu...
Imani za kijinga,yaani Mungu akunyime ukwasi kwa vile utajiua? sasa kwanini asizuie hicho kifo, na akupe mihera kibao,
Hutakiwi kushukuru kama hujatafuta
 
Back
Top Bottom