VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Mwenyekiti wa muda wa Bunge la Katiba,Ndugu Pandu Ameir Kificho, leo ataonja adha ya madaraka aliyonayo atakapowaongoza Wajumbe wa Bunge hilo kupitisha kifungu kwa kifungu Kanuni zitakazoongoza Bunge hilo. Baada ya majadiliano ya siku tatu, Wajumbe leo watapitisha au kukwamisha Kanuni za Bunge lao.
Jana jioni, Mwenyekiti Kificho aliahirisha Bunge hilo hadi leo.Ingawa hakutaja muda wa kukutana tena,taarifa toka Ofisi za Bunge hilo zinaoonesha kuwa Bunge litakutana saa kumi na moja jioni. Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanauona muda mrefu wa kuanzia asubuhi hadi jioni kama muda wa Ndugu Kificho na wasaidizi wake kutafakari juu ya namna ya kuongoza kupitishwa kwa Kanuni husika.
Katika mjadala uliojikita kwenye Kanuni hizo, Wajumbe wengi walizungumzia kura ima ya wazi au ya siri. Kwa wingi, Wajumbe wengi walipendekeza kuwa na kura za siri. Hatahivyo, Ndugu Kificho leo atapaswa kubuni na kusimamia utaratibu wa kupitisha Kanuni hizo kwakuwa hadi sasa Bunge la Katiba halina Kanuni zinaloliongoza.
Nasubiri kuona namna kura za kupitisha kifungu hadi kifungu (kama ikihitajika) zitakavyopigwa: kwa kelele,kwa kunyoosha mikono au kupiga sirini. Kila la kheri Ndugu Pandu Ameir Kificho!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodoma)