Hapa Dodoma: Kificho njia-panda

Hapa Dodoma: Kificho njia-panda

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Mwenyekiti wa muda wa Bunge la Katiba,Ndugu Pandu Ameir Kificho, leo ataonja adha ya madaraka aliyonayo atakapowaongoza Wajumbe wa Bunge hilo kupitisha kifungu kwa kifungu Kanuni zitakazoongoza Bunge hilo. Baada ya majadiliano ya siku tatu, Wajumbe leo watapitisha au kukwamisha Kanuni za Bunge lao.

Jana jioni, Mwenyekiti Kificho aliahirisha Bunge hilo hadi leo.Ingawa hakutaja muda wa kukutana tena,taarifa toka Ofisi za Bunge hilo zinaoonesha kuwa Bunge litakutana saa kumi na moja jioni. Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanauona muda mrefu wa kuanzia asubuhi hadi jioni kama muda wa Ndugu Kificho na wasaidizi wake kutafakari juu ya namna ya kuongoza kupitishwa kwa Kanuni husika.

Katika mjadala uliojikita kwenye Kanuni hizo, Wajumbe wengi walizungumzia kura ima ya wazi au ya siri. Kwa wingi, Wajumbe wengi walipendekeza kuwa na kura za siri. Hatahivyo, Ndugu Kificho leo atapaswa kubuni na kusimamia utaratibu wa kupitisha Kanuni hizo kwakuwa hadi sasa Bunge la Katiba halina Kanuni zinaloliongoza.

Nasubiri kuona namna kura za kupitisha kifungu hadi kifungu (kama ikihitajika) zitakavyopigwa: kwa kelele,kwa kunyoosha mikono au kupiga sirini. Kila la kheri Ndugu Pandu Ameir Kificho!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodoma)
 
Kura ya siri au ya wazi inayoshindaniwa siyo ya kupitisha kanuni bali vifungu vya katiba mpya
 
Uko sahihi Mkuu Ndachuwa. Lakini,kwa mujibu wa Rasimu ya Kanuni, kura itatumika kumaliza mjadala wowote utakaojitokeza Bungeni hapo ikiwemo kupitisha Rasimu ya Katiba. Swali ni je,leo watapitisha vifungu kwa njia gani?

Mzee Tupatupa

Last edited by a moderator:
Anne Kilango Malecela Jana alipendekeza ipigwe kura ya siri ili kuamua kama hoja ya kupiga kura iwe wazi au siri. Hivyo kwa vifungu vya kanuni visivyokuwa na utata atawahoji kwa ndio au hapana na kwa vifungu vyenye utata itapigwa kura ya siri na baada ya kupitisha kila kifungu ndio mwishoni atauliza ndio au hapana.
 
Kura ya kupitisha rasimu ya kanuni iwe jina la mwenyekiti wa muda, KIFICHO.
 
Back
Top Bottom