Jamaa inchi imeshawashinda hii. Kuendelea kuwaacha na kuwatazama wakikazana na tambo za kisiasa, kuongea uongo na ahadi zisizotekelezeka ni national sabotaging kwa vizazi vijavyo.
Hebu tulitazame hili kizalendo na tuamue mfumo mpya wa kuliongoza taifa hili.
CCM ilikuwa na nafasi nzuri ya kuiendesha hii inchi kwa miaka 50 ijayo ila uzembe katika kutengeneza viongozi bora ndio inawagharimu.
Wanaweka vijana waongeaji tu. Siasa wao wanaitazama kama usuperstar na sehemu ya kupatia pesa na sifa za kujulikana badala ya kuitazama kama kazi ya wito na ya kujitoa kwa jasho na akili raia wawe na maisha mazuri.
Tazama vijana wengi wanaowekwa wanakuwa ni empty kabisa vichwani. Wanaona siasa kama michezo michezo ya kukimbizana na wapinzani, kuongea ongea kwa mikwara kwenye media, kusifia viongozi wakubwa. Sasa hawa kesho ndio washike taifa kuliongoza kuelekea wapi sasa.