Hapa Duniani kuna wananchi waoga kama Raia wa Tanzania na Uganda?

Hapa Duniani kuna wananchi waoga kama Raia wa Tanzania na Uganda?

Aliyeturoga siku anafukia ujasiri alikuwa mtupu kainama , sasa hapo ujasiri utoke wapi ? Halafu kafa na kaburi halionekani , tuombee Neema ya MUNGU sana.
Umefanya nicheke kwa saut
 
Tabia ya hovyo sana ambayo imeua vipaji vingi sana na inaendelea kuua imeundwa systematically kwa kitu kinachoitwa "MAADILI" na imewekewa standards za kufikirika tu zinazofanya binadamu kunyeyekea wenye mamlaka tangu utoto tunatetengenezwa hadi tunakua watu wazima tukipewa vitisho kila mahali tunapokua ambavyo kimsingi vinazuia akili kukua na kufanya kazi kulingana na uwezo na kipaji husika.

Restrictions zinaanzia kwa wazazi, zinapanda sunday schools/madrasa, shule za msingi, secondary hadi unapofika chuo kikuu mwanafunzi unakua unamuona profesa na lecturer wako ni miungu watu na wao ndio wanaamua upate degree au la, sio uwezo wako. Haya yanaendelea hadi kwa wanasiasa na viongozi kote kwenye jamii tumekuwa kondoo tusiojiamini wala kuamini kama tuna maarifa yoyote kwa sababu tu ya upumbavu unaitwa "maadili" ukitaka reference ya maadili ipo wapi hamna mwenye jibu bali ni stories tu za mapokeo.

Matokeo yake ni jamii butu, inayoogopa kuhoji, isiyo na ubunifu, inayosubiri makombo ya watawala ndio ile, inayoshi kwa kujipendekeza kuwapetipeti watawala, na wafanyakazi wote wa umma wanakua ni kama mbwa wa watawala wanatumwa muda wowote kupambana na wenye mawazo tofauti na watawala bila hata kupima kwa akili zao (kama wanazo lakini) wanakimbia mbele kulinda maslahi ya wakubwa zao na wapate vimakombo vichache, tena wengine ni wasomi wakubwa tu wasioziamini hata degree zao, hata kuzikana tafiti zao zilizowapa mapHD yao. Hopeless

Na hii imewafanya watawala kuwa na hamu na kiu ya damu muda wote na kila wanapoona mwenye mawazo tofauti, akili inawatuma kuwatupa wote waliwe na mamba mitoni kama wanavyoimba au kuwachinjilia mbali, wabaki wao na chawa tu na majority makondoo yanayoswagwa tu! Wale mema ya nchi bila bughudha...
 
Great Thinkers.

Nadhani pakitokea ranks za raia waoga dhidi ya watawala wabidhilifu Tanzania na Uganda lazima tushike seat ya mbele.

Kinachotupoanza kikubwa ni unafiki imefika mahali hadi dini zinatumika kutetea ujinga, mimi.siyo mdini lakini itoshe kusema waislamu ni binadamu wanafiki kuliko viumbe eote.duniani ndo maana nchi za kiislamu kama africa magaharibi na uarabuni migogoro na.mapinduzi haviishi na ninaamini kabisa bila unafiki wa waislamu Tanzania CCM ingekuwa imeshatoka madarakani kitambo

Same applies to uganda sijui wale viumbe wamelishwa nini. They don't care about Uganda.. imagine Uganda imewekwa chini ya familia moja afu wao wanachekelea tu wapinzani wanapoteswa kama Tanzania.

Kwa kweli sishangai sana maana hata uchumi wetu unashabihiana tupo zero kabisa and we will not go anywhere tutabaki hapahapa Tulipo.kama hatutabadilika.
View attachment 3315177
View attachment 3315178
Mtanzania aache mishe zake aje akupiganie wewe Chadomo? 😂😂

Pigana mwenyewe watakaofaidi ni Watoto wako ,mkeo na wewe.
 
Ukraine ambayo kila siku inalalama Russian aggression na invasion.

Siku Russia ikipiga jengo utaona video inasambazwa dunia nzima ione raia wanavyoteseka na kuwataka vijana wajiunge na jeshi kulinda nchi yao.

Lakini ushaona Ukraine ikisimbaza picha za maiti za wanajeshi baada ya kushambuliwa au hata upande wa pili wakifanya hivyo.

Sasa wewe uweke picha za watu waliochezea kichapo na jeshi la polisi, huyu kavunjwa mbavu, huyu mguu, mwingine damu zinavuja, ilimradi tafrani; raia gani mwenye akili timamu atajitokeza kwenda kuonja hiyo dose ya polisi na yeye.

Akili za CDM zinawatosha wenyewe, wanachofanya CDM kusambaza hizo picha ni kusaidia polisi kuwaogopesha wengine wasijaribu.
 
Back
Top Bottom